Ngassa Asaini Simba

Ngassa Asaini Simba

Kucheza mpira ni ajira kama ajira nyingine, mchezaji pia anayo haki ya kuonesha mapenzi kwa klabu anayoipenda kama alivyofanya Ngassa. Azam wanashindwa kuelewa uhuru huo, huwezi kumlazimisha mchezaji apende klabu yako wakati yuko hapo kwa ajili ya ajira. Hata Kaseja alipojiunga Yanga hakuna mtu aliyeamini kuwa Kasejea anaipenda Yanga zaidi ya kufuata maslahi, alivyorejea Simba hakuna pia aliyeshangaa. Kaseja akiwa Yanga alicheza kwa nguvu zake zote na kwa uaminifu mkubwa isipokuwa katika mechi ya mwisho ya ligi ambapo mchezo huo uliisha kwa matokeo ya Yanga 2-2 Simba, siku hiyo alifungwa na Simba mabao ya kitoto sana hata kuibua hisia kwamba anawaachia Simba makusudi. Ngassa akiwa Azam kafanya hivyo hivyo.

Ngassa kwenda Simba ni haki yake pia maadam maslahi yapo, hii haiondoi mapenzi yake makubwa kwa klabu yake adhimu Young Africans Sports Club, Simba waelewe kuwa hiyo ni ajira kama Yanga walivyomuelewa Kaseja. Siku Simba akifungwa na Yanga wasianze kulalama kama ilivyokuwa kwa Kelvin Yondan.

Kijana Ngassa nampa pole kwa masahibu yaliyompata huko Azam FC., lakini pia niwapongeze Simba SC kwa kumpa nafasi ya kuboresha kiwango chake cha soka.

Nampa pole pia kijana Sureboy kwa masahibu ya jinsi hiyo. Sioni kama huyu dogo anastahili kuhukumiwa jinsi hii maana hata siku ya mechi ya Yanga aling'ara maridhawa, sasa sielewi kama Azam FC kwa mawazo yao finyu walidhani wataifunga Yanga kila siku kama walivyofanya huko nyuma wakati wa migogoro lukuki ndani ya klabu. Endapo Sureboy ataendelea kunyanyapaliwa ni vyema akajiunga na klabu nyingine na kuachana na hao Azam FC na huu ndiyo utakuwa mwisho wao (The rise and fall of Azam FC), klabu gani inaongozwa kifamilia, hii lazima ife amini usiamini hakuna good governance hapa ni ubabe na majungu tu.

Msomaji sitaki nikuchoshe, naomba niishie hapa kwa sasa.
 
Wapeni vijana mapesa na nafasi bongo footbal ndio hilo hakuna ulaya wala cha zaidi hapa hapa tu!!
 
huyu Ngasa wanataka kummaliza washenzi hawa.si bora wangemuacha bure aende zake yanga.!
 
Habari za uhakika zilizotekea mida ya saa 2 asubuhi ni kwamba Ngassa amesaini Simba kwa ofa ya 25m Kaburu kafanya mambo...more to follow!!!!

Do you really know what you are writing?,hlf unatuambia habari za uhakika....nikurekebishe tu....Azam wamempeleka Ngassa kwa mkopo wa hela...kwanza uliona wapi mchezaji anapelekwa kwa mkopo wa kununuliwa eti Mil 25 na mshahara atakuwa analipwa na Simba hao hao,is that a loan or what? nimeamini hela siyo kila kitu wakati mwingine ni afadhali ujaliwe akili kuliko mahela ya Bakhresa ambaye anashindwa ku'employ watu wenye akili wakamfanyia mambo ki'proffesional,that's 1........2....
Ngassa haja'sign karatasi yeyote ya kuidhinisha kukipiga Msimbazi,nimemsikia kwa kauli yake kuwa hizo habari za yeye kupelekwa Msimbazi anazisikia kwenye media tu,hajashirikishwa wala hajataarifiwa rasmi...upo hapo?
Mimi naichukulia Simba kama sehemu ya Azam otherwise ningewashauri waachane na hiyo deal ksbb itawaingiza hasara,lkn ksbb ni kama hela inatoka mfuko huu inaingia mfuko ule waache waendelee nayo.
Kama vp atarudi Yanga bure mwakani,Yanga ina akili siyo kama kina Kaburu wenu
 
Namkubali ngasa ila alijuvunjia heshma kwa kile kitendo!
Hakukua na ulazima wa kufanya yote yale!!
 
Goli lingine hili simba wanafungwa baada ya lile la kelvin Yondan.
 
Hapa Simba wamejikoroga mtu ana mapenzi na Yanga wao wameamua kumchukua kichwa kichwa yatakuwa yale yale ya Yondani
 
Nimesikia dogo alikuwa hataki kwenda Simba ni vile Yanga hawana shida naye hivo hawakufika dau la kuiridhisha Azam, katika gazeti la Tanzania Daima wameandika hali ya kujua kuwa anakwenda Simba imemfanya mpaka akatoa machozi kwa uchungu coz yeye anaizimia zaidi Yanga, sasa swali ninalojiuliza kama Azam wamemtimua kwa yeye kuonyesha mapenzi kwa Yanga hao Simba si watamla nyama siku wakicheza na Yanga halafu dogo acheze chini ya kiwango chake.
 
Mrisho-Ngassa.jpg


Yanga Watakiwa Kumkomboa Ngassa Simba Kwa Milion 80
AZAM FC imetoa nafasi ya pili kwa Yanga, kumrejesha nyota wake wa zamani, Mrisho Ngassa- ambayo ni kutoa dola za Kimarekani 50,000 (zaidi ya Sh. Milioni 80) ili irejeshewe mchezaji huyo, ambaye kwa sasa ametolewa kwa mkopo Simba SC . Soma taarifa hii ya Azam, ambayo BIN ZUBEIRY imetumiwa na Meneja wa klabu hiyo, Patrick Kahemele,
**
Ufafanizi juu ya suala la mchezaji Mrisho Halfani NgasaKlabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa ya ufafanuzi juu ya sakata la mchezaji Mrisho Ngasa ambalo linaonekana kupotoshwa

  1. Azam FC ilitangaza kuwa biashara ya mchezaji Mrisho Ngasa ingefungwa siku ya Jumatano 1/08/2012 saa saba mchana na ilivitaka vilabu vyenye interest na mchezaji huyo kufika makao makuu ya Azam FC ofisi ndogo zilizopo kwenye kiwanda cha unga cha Azam-Mzizima zikiwa na pesa taslimu. Bei ya mauzo iliyopangwa ilikuwa ni Dola 50,000. Lakini katika mawasiliano ya email kwa makatibu wakuu wa Simba na Yanga, Azam FC iliweka bayana kuwa ilikuwa tayari kushusha bei ya mauzo na ingemuuza Ngasa kwa timu ambayo dau lake lingekuwa kubwa zaidi ya mwenzake.

Kwa maana hiyo biashara ya mchezaji mrisho ngasa ilifanyika kwa uwazi. Lengo la Azam FC lilikuwa ni kutoa haki kwa kila klabu yenye uwezo wa kifedha kuweza kupata huduma ya Ngasa.

Pia tunaomba ifahamike bayana kuwa mchezaji Mrisho Ngasa alipewa taarifa kuwa anauzwa na aliombwa asaidie kushawishi klabu anayoitaka ifike kwetu na ofa yake. Ngasa alitamka bayana kuwa yupo tayari kwenda klabu yoyote ambayo Azam FC itaona imekidhi mahitaji yake kwa masharti kuwa maslahi yake ya kimkataba kati yake na Azam FC yazingatiwe.

  1. Hadi kufikia siku ya Jumatano 01/08/2012 saa saba mchana. Ni klabu ya Simba pekee iliyojibu kwa maandishi na kuonesha nia ya kumchukua Ngasa. Yanga wao hawakuwahi kujibu email, ingawa kwa majibu ya simu Mjumbe wao wa Kamati ya usajili Bw Sefu Magari alitangaza kuwa Ngasa hana thamani ya zaidi ya milioni 20. Na Yanga haikuwa tayari kuboresha ofa yake.
  2. Muda wa kufungwa kwa biashara ya kumuuza Ngasa ulipofika, ni simba pekee kupitia kwa makamu Mwenyekiti wake Bw Geofrey Ngange na Mhasibu wake ndiyo waliofika wakiwa na pesa taslimu shilingi milioni 25. Yanga hawakuonekana na hawakutaka kupokea hata simu walizokuwa wakipigiwa kuulizwa kama wana interest.
  3. Kikao cha dharura cha Azam FC kilikaa na kuamua kuwa biashara ya kumuuza Ngasa ilishindikana kutokana na kutokupatikana kwa mnunuzi mwenye dola 50,000. Kwa maana hiyo Azam FC iliamua kumpeleka Ngasa kwa mkopo kwenye klabu iliyofika na kuonesha nia ya kumhitaji (Simba)
  4. Simba walipewa sharti la kuhakikisha wanamlipa Ngasa mshahara wake kamili (TZsh 2,000,000) pamoja na stahiki zake nyingine zote za kimkataba
  5. Sababu za kumpeleka Ngasa kwa mkopo ni kumuepusha na adhabu ambayo klabu ya Azam FC ingetoa kwa Ngasa kama angebaki.
  6. Azam FC inapenda kuweka wazi kuwa haijamlazimisha Ngasa kwenda Simba kama inavyopotoshwa. Kama Ngasa anataka kuvunja mkataba wake au kama Yanga bado wanamhitaji basi waje na dola 50,000 na Azam FC itawauzia kwani licha ya kwamba amepelekwa kwa mkopo simba lakini Ngasa bado ni mali ya Azam FC
  7. Tunaomba kuweka msimamo wetu kuwa hatupo tayari kumlipa Ngasa na kuvunja mkataba wake na hatuna sababu ya kufanya hivyo. Kama Ngasa hataki kwenda tunakompeleka Azam FC inamruhusu kubakia klabuni na kutumikia adhabu.
  8. Lakini Ngasa na washauri wake waelewe kuwa akiamua kubaki Azam FC atakaa nje ya uwanja kwa muda wote uliosalia kwenye mkataba wake, kwani Azam FC haipotayari kumvisha jezi mchezaji anayefanya vitendo vya utovu wa nidhamu.
  9. Kwa Sakata hili limeanza kuhusishwa na sakata la Mchezaji ramadhani Chombo. Naomba nitoe ufafanuzi kama ifuatavyo. Redondo alipewa option tatu za kuchagua baada ya kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu timu ilipokuwa safarini Mwanza.
    1. Kupelekwa kwa mkopo Moro United?
    2. Kupatikana kwa mnunuzi mwenye shilingi milioni 40
    3. Kukubali adhabu ya kufungiwa kwa miezi mitatu na kulipwa nusu mshahara wahati akitumikia adhabu.
Redondo alithibitisha kuipenda Azam FC kwa kukataa kuuzwa au kupelekwa kwa mkopo. Alikubali kutumikia adhabu yake na ilipoisha alirudi na kuomba msamaha na sasa ni mmoja kati ya wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu sana. Azam FC inajivunia kuwa na mchezaji kama Redondo na bila kupepesa macho wala kung'ata maneno. Azam FC inamchukulia Redondo kama mtu spesho na mwenye mapenzi ya dhati na klabu yake na inamtaka aendelee kuwa na moyo huo.


Imetolewa na utawala.

Azam FC
 
mkuu Candid Scope umetoa mwanga kidogo azam Fc wanachohitaji ni mchezaji mwenye commitment na team ..! Rooney ni mpenzi na mshabiki wa everton .. kukiwa na match kati ya everon na man utd jamaa huwa anweka mapenzi yake pembeni..! sijawahi kumuona roney akishangilia bao na kubusu jezi ya everton mbele ya medias sababu ana mapenzi na hiyo club! roney ana akili akijua mpira ni biashara na yeye ni brand ya man utd for the time being ...

huyu ngasa mapenzi yake hakutakiwa kuonesha hadharani mbele ya uma esp akiwa anatumikia azan Fc uwanjani... ni maamuzi magumu wameyafanya azam lakini nawapongeza kwa hili dogo atajifunza..
 
Ngassa is like Danny Mulwanda they have nothing special, i cant expect much from them.
 
Nimesikia dogo alikuwa hataki kwenda Simba ni vile Yanga hawana shida naye hivo hawakufika dau la kuiridhisha Azam, katika gazeti la Tanzania Daima wameandika hali ya kujua kuwa anakwenda Simba imemfanya mpaka akatoa machozi kwa uchungu coz yeye anaizimia zaidi Yanga, sasa swali ninalojiuliza kama Azam wamemtimua kwa yeye kuonyesha mapenzi kwa Yanga hao Simba si watamla nyama siku wakicheza na Yanga halafu dogo acheze chini ya kiwango chake.

Ili wasitafute sababu siku ya game yao na Yanga wasimchezeshe kabisa Dogo,bila shaka Milovan atakuwa amejifunza kwa Stewart
 
Ngassa wa nini na kwa lipi alilofanya hivi karibuni?Nimemuona kwenye CECAFA akishindwa kufanya lolote la maana uwanjani na sikushangaa yeye kukaa benchi.Effectiveness yake uwanjani kwa sasa ni ndogo mno.Dribbling zake nyingi kwenye empty spaces uwanjani akikutana tu na adui anapoteza mpira au kutoa blind pass.Kiukweli hata Jan Poulsen aliliona hili na kuanza kumweka benchi.Sidhani kama Jan Poulsen na Stewart Hall wanamchukia ila kiukweli kwa sasa dogo ana kazi sana ya kurudisha kiwango.Cha ajabu 'wachambuzi' wetu wanamdanganya kuwa anaonewa kutopangwa.

Siku ile alipotoa pasi kwa Sure Boy na kutiliwa tena na kufunga ilikuwa blind pass...........???????????? Kiujumla Azam walishaanza kumdis dogo, hakuwa na amni pale na wanaojua ni kwa nini ni Azam na Ngasa, kumbuka Chombo na bifu zake na Azam. Napata wasiwasi na Azam kuna viongozi wanapika majungu ya kutisha pale na matokeo yake ni wachezaji wengi toka bara kutoswa na kuwapendelea Wazanzibar. Tatizo wazanzibar hawabebeki, yaani viwango vibovu na hawakazi ndo maana unaweza ona hawapangwi kwa sasa, hivi waweza mfananisha Mcha na Ngassa...? kwa kipi au Murad kwa Joseph Owino? Hata Mushi kwa Mwadini na zengwe la kuwa kacheza chini ya kiwango siku ya CECAFA fainali utasikia anachoma mahindi.
 
Ili wasitafute sababu siku ya game yao na Yanga wasimchezeshe kabisa Dogo,bila shaka Milovan atakuwa amejifunza kwa Stewart

Ngasa ndo atakuwa amejifunza kwa Stewart!!
 
mkuu Candid Scope umetoa mwanga kidogo azam Fc wanachohitaji ni mchezaji mwenye commitment na team ..! Rooney ni mpenzi na mshabiki wa everton .. kukiwa na match kati ya everon na man utd jamaa huwa anweka mapenzi yake pembeni..! sijawahi kumuona roney akishangilia bao na kubusu jezi ya everton mbele ya medias sababu ana mapenzi na hiyo club! roney ana akili akijua mpira ni biashara na yeye ni brand ya man utd for the time being ...

huyu ngasa mapenzi yake hakutakiwa kuonesha hadharani mbele ya uma esp akiwa anatumikia azan Fc uwanjani... ni maamuzi magumu wameyafanya azam lakini nawapongeza kwa hili dogo atajifunza..

Ni Kweli Kabisa Ngasa alikosea ila bila shaka amejifunza sasa kuwa mpira ni kazi mapenzi yako weka mfukoni.
 
Back
Top Bottom