Hivi nyie mnaotoa mapovu bila hoja zaidi ya "ni dili zuri", mnatambua Ngasa alilalamikia nini? Alipohongwa kwa Simba hakuhusishwa, si mwajua kuwa wachezaji wa Tanzania ni kama bidhaa? Alilalamikia kitendo hicho, akahongwa gari. Kabla hata hajasahau kitendo kile kisicho cha kiungwana, ghafla anasoma magazetini kuwa amepigwa mnada kwenda bucha za Sudan, si amekuwa ng'ombe yule? Unapomuuza ng'ombe utamuuliza kama anaridhia? Tena bila aibu tunasikia eti msomali "ame-negotiate" mshahara wake kuwa ni dola 4,000. Mwe! Inamaana msomali amekuwa wakala wake? Huu upuuzi lazima ukomeshwe. ALICHOFANYA NGASA NI KUPIGANIA UTU WAKE, NA SI TAMAA YA PESA KAMA WATOKWA MAPOVU WEEENGI HUMU JAMVINI WALIVYO. Utumwa kitu kibaya sana. Hongera Ngasa, you are setting new standards kwenye soka letu linaloongozwa na waroho wa pesa kama walivyofanya Azam na Simba. Ujinga huu hatuuoni kwenye nchi zilizo serious na soka.
Mnakumbuka Ngasa alipokwenda Simba ilitangazwa kuwa eti amepewa mkataba mrefu ili kuipotezea Yanga? Sasa suala la tamaa ya dola limewaumbua mbaya. AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU!
Bado mtu yeyote mwenye akili timamu na asiyepumbazwa na ujinga wa kishabiki hawezi kufagilia uhuni wa aina hii. Ngassa mwenyewe alikiri kuongea na wasudani na akawaelekeza wafanye mazungumzo na timu yake Simba. Sasa Simba na Azam walichokosea ni nini? Kukubali kuuzwa kwa Ngassa?
Alichopaswa sio kujificha, ni kumtumia wakala wake kunegotiate deal la kumfaa au kuweka wazi kuwa hayuko tayari kwenda Sudan kwa muda huu, na sio kufanya maigizo ya kitoto kwa watu wazima na shughuli zao. Tujifunze kutoa ushauri wa maana kwa wachezaji wetu na sio kufagilia upuuzi ambao ambao hauna maana ktk dunia ya kisasa.
Mbona ni nchi hii tu mambo ya usajili ndio yana kelele kila siku??????????????