Ngasongwa, Sumaye, Mkapa na Angel Hurst Industiries

Habarindiyohiyo

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
263
13
"Kambi ya Upinzani ilikuwa inajiuliza hivi hawa wawekezaji wenye Hisa 0.006% kila mmoja ni kweli wawekezaji, na wanaweza kukifufua kiwanda kama kweli kiko kwenye hali mbaya kama Serikali inavyosema. Utafiti wetu umeonyesha kuwa kumbe mwenye mali halisi wala siyo Rai Brothers kama walivyo kwenye Sale agreement, bali ni Angel Hurst Industries ya Uingereza yenye hisa 99.988% kama ilivyosajiliwa kwenye Kituo cha Uwekezaji kama inavyoonekana kwenye Certificate of Incentives no 00021049 iliyotolewa TIC tarehe 19 April, 2004 kwa Mufindi Paper Mills Ltd ambayo ndiyo Kampuni iliyosajiliwa baada ya kununua Kampuni ya Southern Paper Mills (SPM) ambayo ilikuwa asili mia 100% mali ya Serikali na hivyo mali ya Watanzania wote na kusimamiwa na NDC ikiwa na Hati ya Industrial Licence na .0907. Isitoshe, kiwango cha Fedha kilichotajwa kwa TIC ni Dola za Marekani 52 Millioni (Foreign) na Tshs billion 9.251 fedha za ndani yenye jumla ya Dola za Marekani 61.251 na siyo 25.Millioni walioyotaja kwenye Nyaraka mbalimbali za Sale Agreement. Kwanini kuwe na udanganyifu huu mkubwa? "

Angel Hurst Industries ni Mkapa, Ngasongwa na Sumaye

.....ndiyo hiyo
 
Jamani sasa hawa watu nadhani wanahitajika kuchwapa bakora za chuma,
inaniuma sana mimi hv watz tunadanganywa kiasi hiki!
Kumbe ndio maana mr. prezidenti ameogopa kukanyaga huko wakati akiwa ziarani iringa.
Sasa tunaelekea kubaya jamani.
Mungu atuokoe na huu ufisadi mwe!!!
 
HabariNdiyoHiyo,

..calm down....tupe habari nzima katika mtiririko unaoeleweka.

..umeileta habari hii kana kwamba kila mtu hapa ni insider and can easily connect the dots.
 
JF sauti ya Umma, watayaficha hapa yanaanikwa. Ila sooner or Later wataanza kunyukana wenyewe kwa wenyewe, maana Sasa tumejua kwa nini hii nchi ni masikini na Itaendelea kuwa masikini Mpaka yatokee Mapinduzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kigawanyike na ushindi uende kwa Watanzania wazalendo ili Warudishe mali za Umma mikononi mwa Umma. Tutasikia mengi sana, vita ya Ufisadi na Wataanza kutajana very soon. Tutawajua hata wakiwa makaburini tutaenda kuweka alama ya pingu juu ya makaburi yao, kwa mauaji ya watanzania. Naam huu ni uuaji, Watanzania life expectancy imeshuka shauri ya Umasikini, watu hawana ajira, hawamudu huduma muhimu za afya Shauri ya Waroho wanaojiita VIONGOZI.
 
Ndio hivyo tukiambiwa tumeuzwa tutakata, Maana tulio wakabidhi nchi watuongoze , wao ndio wanatuuza, eg ni issue ya Kagera Sugar, na mkopo wa Bot, Tax exmption wanazo pewa baadhi ya makampuni ya wahusika ( Viongozi) kama Mtibwa, Vodacom, TTCL etc
Eg ya BOT na Mkopo wa Kagera Sugar
BoT to ditch Mwananchi Gold, non-core functions
GOVERNOR NDULU: Exercise will be carried out carefully ``to avert any problems.``
-Part of ongoing efforts to clean up its act

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE Bank of Tanzania (BoT) is in the process of withdrawing from various non-core functions of a central bank, including involvement in the controversial Mwananchi Gold Company Limited in which it has a 35 percent stake, it has been revealed.

Well-placed sources say this is part of a strategy by the new BoT management under incumbent governor Prof Benno Ndulu to clean up the image of the key financial institution that was long dogged by widespread corruption allegations under former governor Daudi Ballali (now deceased).

It is also in line with a recommendation made by auditors Ernst & Young for the bank to drop all non-core functions and ''be left to perform only functions which are stipulated in the BoT establishing Act.''

The recommendation is contained in the final report of the special audit on payments made from the external payment arrears (EPA) account during 2005/06, conducted by Ernst & Young and endorsed by the Controller and Auditor General (CAG).

Among other things, the BoT is reviewing the credit guarantee facilities it provides to private companies, its investments in various business undertakings, and other operations that are not pure central bank functions.

Apart from its 35 percent equity in Mwananchi Gold Company Limited, the bank also provided an interest-free loan to the privately-owned firm amounting to $6,062,220.57 (approx. 7bn/-).

Located in the Vingunguti Industrial Area on the outskirts of Dar es Salaam, Mwananchi Gold started its operations on January 1, 2006.

Auditors uncovered that mortgages for loans to Mwananchi Gold were not duly registered with the registrar of companies in accordance with the prevailing laws of the country, which may render the mortgages void.

Among the dubious BoT guarantees are a massive 72bn/- loan issued to Kagera Sugar Limited in 2004 by a group of lenders comprising several local banks and pensions funds.

The central bank has found itself in serious liability due to its long-term, 80 per cent guarantee of the huge loan to Kagera Sugar, which has experienced difficulty in repaying the credit.

On the strength of the BoT guarantee, the company went ahead and secured loans amounting to 72.178bn/- from various local financial institutions for rehabilitation and expansion of the formerly state-owned sugar factory.

Records show that the lead bank in the lending consortium, Stanbic, by itself gave out 17.178bn/-. Other financiers in the deal were Barclays Bank (10bn/-), NSSF (12bn/-), PSPF (12bn/-), PPF (12bn/-), CRDB Bank (8.5bn/-), and the Tanzania Investment Bank (5bn/-).

At the time of receiving the loan, Kagera Sugar was given a two-year grace period to start servicing the principal loan and interest, but the company's management failed to honour these obligations despite frequent reminders from the lenders.

Other past BoT operations that raised serious queries from auditors were the decision to purchase a five-year special treasury bond worth 155 billion/- from the government.

It is understood that this money was later used by the BoT to make highly dubious payments in favour of the associated Meremeta, TANGOLD and Deep Green Finance companies.

When contacted for comment yesterday, Governor Ndulu confirmed that the BoT was in the process of ditching operations that are not purely functions of a central bank.

He said the exercise would be carried out carefully ''to avert any problems.''

Prof. Ndulu said the function of administering credit guarantees would be taken up by another government institution once the BoT fully withdraws.

He said in future, the central bank will focus on its principal functions, which include to formulate, implement and be responsible for monetary policy; to issue currency; to regulate and supervise banks and financial institutions; and to manage the country's gold and foreign exchange reserves.

Other core functions of the BoT include to promote sound money, credit and banking conditions conducive to the development of the country's economy.

The primary objective of the central bank is to formulate and implement monetary policies directed to the economic objective of maintaining price stability conducive to a balanced and sustainable growth of the national economy.

Under the provisions of the BoT's establishment Act, the board of directors is responsible for determining policies, approving the administrative budget, and ''other functions specifically conferred or imposed upon the board by the Act or any other written law.''

The management of the bank and direction of its business and affairs are vested in the governor, while the deputy governor, subject to the general supervision of the governor, is responsible for the day-to-day bank business.
 
Mwaka wa Shetani huu ni wendawazimu kwendelea kuwakumbatia na hao wanao uza haki zao kwa tshirts na kofia wanastahili kuchapwa viboko wanauza utu wao kwa vitu vyenye thamani ya 2000.
 
WAKUU STORI HII IPO TANZANIA DAIMA NAWASILISHA"

Wapinzani waja na ufisadi tena
na Ratifa Baranyikwa, DodomaSERIKALI imetakiwa kutoa ufafanuzi wa juu ya ubinafsishaji wenye utata wa Kiwanda cha Karatasi cha Mgololo, kinachodaiwa kuuzwa kifisadi kwa Kampuni ya Rai Group Ltd, ya nchini Kenya.

Hayo yalibainishwa jana bungeni na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Lucy Owenya, wakati akisoma hotuba yake ya kujibu ile ya bajeti ya wizara hiyo iliyosomwa na Waziri wake, Mary Nagu.

Katika hotuba hiyo, Owenya alisema, kambi ya upinzani, inakusudia kuwasilisha hoja binafsi bungeni iwapo serikali itashindwa kutoa taarifa kamili juu ya kiwanda hicho sambamba na kueleza mchakato wa ubinafsishaji wake kwa kampuni hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku tano tu zimepita, tangu Waziri Nagu, alipotoa ufafanuzi juu ya ubinafsishaji wa kiwanda wakati akijibu swali la Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, (CHADEMA).

Katika majibu yake hayo ya wiki iliyopita, Nagu alisema kuwa, kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa kufuata taratibu zote.

Katika hotuba yake ya jana, Owenya alisema serikali haikuwa makini katika ubinafsishaji huo, kwani kumbukumbu zinaonyesha kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa Kampuni ya Rai Group, lakini utafiti wa kambi ya upinzani umebaini kuwa hakimilikiwi na kampuni hiyo kama ilivyo kwenye makubaliano ya uuzwaji.

Alisema utafiti huo umebaini kuwa kiwanda hicho kimeuzwa kwa Kampuni ya Angel Hurst Industries ya nchini Uingereza, inayodaiwa kumiliki hisa asilimia 99.9.

“Kampuni ya Angel Hurst Industries inaonekana kwenye Certificate of Incentives No. 00021049 iliyotolewa na Kituo cha Uwekezaji (TIC) Aprili 19, 2004 kwa Mufindi Paper Mills Ltd, ambayo ndiyo kampuni iliyosajiliwa baada ya kununua Kampuni ya Southern Paper Mills (SPM) ambayo ilikuwa na asilimia 100, mali ya serikali na hivyo kusimamiwa na NDC,” alisema.

Katika ufafanuzi alioutoa Waziri Nagu mwishoni mwa wiki, bungeni alisema Kampuni ya Angel Hurst Industries, inamilikiwa kwa asilimia 100 na Rai Group, na hivyo kutokuwa na tatizo lolote kwani kampuni zote mbili ni wamoja.

Kambi ya upinzani inaielezea kauli hiyo ya Nagu kuwa iliyozidisha utata kuliko majibu na kusisitiza kuwa inahitaji taarifa kamili.

Aidha, akielezea mchakato mzima wa ubinafsishaji wa kiwanda hicho, Owenya alisema kwa mujibu wa kifungu cha mkataba wa mauziano, kinatamka bei ya mauziano ya kiwanda kuwa ni dola za Marekani milioni 26 lakini cha kushangaza ni kwamba, mkataba huo unaeleza serikali italipwa dola milioni moja tu za Marekani siku ya kuwekeana saini na dola 3,000,000 zitawekwa kwenye Escrow Account ambazo mwekezaji atazichukua atakapokuwa ametimiza masharti, ikiwemo kukarabati kiwanda chake.

“Maana yake ni hela zake na si malipo ya ununuzi wa kiwanda, mambo haya yanahitaji ufafanuzi na kauli ya waziri haikutoa ufafanuzi kabisa wa hali hii tata. Fedha nyingine dola za Marekani milioni 22 atazitumia mwekezaji kwa kufanyia kiwanda ukarabati, nazo zinabaki kwake kama lengo lilikuwa kuhakikisha kiwanda kinaendelea, kwanini serikali haikusema hivyo wazi katika mkataba,?”

“Ni nini tafsiri ya purchase price, Mheshimiwa Spika, hivi anadanganywa nani? Kwa dola milioni moja kwa nini isielezwe hivyo waziwazi? Kama tatizo ni kukosekana kwa mnunuzi kama serikali inavyotaka kueleza, kwanini hakikuuzwa kwa sh moja, yaani ‘Nominal Value’?”

Kwa mujibu wa maelezo ya kambi ya upinzani, Kampuni ya Rai Group inadaiwa kumilikiwa na Wakenya wawili waliotajwa kwa majina ya Jaswant Singh na Sarbjit Singh kila mmoja akiwa na hisa 0.006.

Kambi ya upinzani imesisitiza kuwa inataka kujua hao wawekezaji wenye hisa asilimia 0.006 kama ni kweli wawekezaji na wanaweza kukifufua kiwanda.

Owenya alisema kuwa serikali itamke ndani ya Bunge kama jambo hilo kisheria ni sahihi na hao wenye hisa zaidi ya asilimia 99 wanaonekana wapi katika mkataba na kama mkataba wa mauzo hauwataji kukitokea tatizo wao watawajibikaje na mkataba ambao si washiriki.

“Kwanini kuwa na mkataba kama kuna weza kuwa na watu waliojificha nyuma na mkataba kusainiwa na watu wasio na kitu? Je, Rai Group waliosajiriwa kwa mujibu wa sheria Tanzania ni wamiliki wa MPL Ltd kwa pamoja wakati wa kuuziana wanamiliki tu asilimia ya 0.01?” alihoji.

Aidha, kambi ya upinzani imelalamika kiwanda hicho kuuzwa kwa bei ya kutupa ukilinganisha na thamani halisi ya kiwanda.

Akinukuu hukumu iliyotolewa na mahakama ya kazi juu ya uchunguzi wa mgogoro wa kazi Na 80/2006 ya chama cha wafanyakazi TUICO na PSRC na wenzake, inadaiwa kuwa ilitamkwa “ si rahisi kuamini kuwa mali zote za Southern Paper Mills Ltd (Kiwanda cha Mgololo) za thamani ya soko la mabilioni si chini ya bilioni 500 kwa makisio yangu na si ile ya bilioni 85 iliyotumika kuuzia tunaona hii ni “token/book price value” tu ambayo mathalani flat rate ya trailer Scania linalofanya kazi lilithaminiwa kwa sh 300,000 kwa kila trailler ambayo ni chini ya bei halisi hata ya tairi lake moja tu…”

Owenya alisema hali hiyo ni ya kutisha kama gari la tani 60 tena “heavy duty” liliuzwa kwa bei ya 600,000 bei inayofanana na bei ya tairi moja tu la gari hilo na kuongeza kuwa “ hapa kunahitajika maelezo ya kutosha,” alisema.

Alizitaja rasilimali za kiwanda hicho zilizouzwa kwa bei ya kutupa kuwa ni pamoja na nyumba, zikiwemo za daraja la kwanza, kijiji kizima cha wafanyakazi kama ilivyorekodiwa katika mashauriano ya kamati ya “FAST TRACK” ya Baraza la Mawaziri Agosti 4, 2003 .

Kambi ya upinzani pia imeitaka serikali kueleza juu ya eneo la hekta 28,000 ambazo hazikulipwa kitu kabisa na kutaka tathmini ifanyike upya kuangalia bei halisi ya maeneo yote hayo au mkataba uvujwe.

Aidha, NGO inayoitwa ICOMET inayodaiwa kupewa hekta 2,000, lakini ikapewa hatimiliki ya hekta zote 28,000 na kuhoji kuwa NGO hii ni ya nani.

Aidha, kambi ya upinzani imeitaka serikali kusimamia utaratibu unaoeleweka kuwalipa waliokuwa watumishi wa kiwanda hicho zaidi ya 760 ambao bado wanadai haki zao pamoja na hukumu iliyotolewa mahakamani, wakitakiwa kulipwa zaidi ya sh 2,647,255,816.

Wakati huo huo kambi ya upinzani pia imeitaka serikali kutoa ufafanuzi juu ya kuuzwa kwa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kinachodaiwa kuuzwa kwa bei ya kutupa ya sh bilioni 116 kwa mwekezaji anayejulikana kama ILLOVO.

Kambi ya upinzani imesema kuwa imeshtushwa na bei hiyo mara baada ya kubaini kuwa Kilombero ilikuwa na viwanda viwili, yaani K1 ambacho kina eneo la hekta 6,214.5 na K2 hetkat 3,153.
 
WAKUU NAPENDA PIA KUWASILISHA MAONI YA BAADHI YA WASOMAJI WA TZ-DAIMA THEN TUTAONA MUELEKEO WAO NA WETU KTK THREAD HII"

Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 11 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Wa waaaaa wapinzani,mambo gani wanafanya kila kitu wauza kwa bei ya chee hivi wanafikiri baba wa taifa alipewa bure?mambo yameiva tena tunataka mpaka kieleweke wakati huu,zama za ujinga basiiii!!!!!!!!!!!!!!!kama walikula warudishe hela za watu,na huyo atakuwa Mungai tu kwani nae ni fisadi mkenya,

na kocha wa dunia, MBINGUNI, - 12.08.08 @ 02:20 | #29771

Napenda kupongeza jitihada hizo za kambi ya upinzani.Muhusika mkuu anajijua na ni mmoja wa mawaziri waandamizi(ati mstaafu)mwenyeji wa hukohuko ambaye kwa kiasi kikubwa ndiye alishinikiza ubinafsishaji wa mgololo na kipindi hicho alitumia ushawishi wake alipokuwa nje ya baraza lakini akiwa na nguvu za ushawishi aliojijengea ndani na nje ya serikali.Ni kigogo huyohuyo ambaye akiwa mwenyekiti wa Bodi ya Sao Hill Timber alishinikiza kwa kampuni hiyo kupewa upendeleona yeye kunufaika zaidi.
Na ubinafsishaji huo wa mgololo ni moja ya mikataba yenye harufu mbaya na chafu za kifisadi mingine pia ni uangaliwe pia umiliki wa kiwanda cha Kagera Sugar inadaiwa kuna kigogo mkubwa tena mstaafu aliye nyuma yake na wanaosemwa(Mtibwa's) ni wasimamizi tu.
Uangaliwe pia umiliki wa Hotel ya Mt.Meru huyo aliyeinunua alitumiwa tu na mmoja wa kiongozi mstaafu mwandamizi ambaye hivi karibuni anajifanya kutaka kujisafisha na kujiita MR.CLEAN.Je zile 5 Bilion zililipwa? Rubambe anaijua siri hiyo tumechoka sasa ni vizuri mtuachie nchi yetu tuishi kwa amani.
Nawaonya na kuwakumbusha pia kule Nishati ununuzi wa zile jenereta za kupeleka mikoani thamani ya soko haizidi dola milion 2.5 kama mmeishazinunua kwa hiyo bei ya USD 5.milion msiwaingize hao vijana waziri na Naibu wake nawshauri muwe macho sana na wakurugenzi wenu na wasaidizi wao hususani hao wa Nishati na madini.
Hivi inakuwaje hata nyie viongozi wetu wengine mshindwe ujanja na hao wanaojiita waqtaalamu akiandika na kuleta maoni yake pokea na kisha yafanyie kazi ingia kwenye mtandao dunia nzima ipo mkononi ukimaliza andaa paper au maoni yako utafautiane na huo upuuzi.
Leo tukae tunacheka na kuchezeana shere lakini hii nchi hatima yake tutagwana vipande huu ni ushauri wa bure tu.

na msongareli, tz, - 12.08.08 @ 02:46 | #29773

Kwanza wapinzani big up,mnatufumbua macho kweli!
Jamani fuatilieni tarehe za mauzo mtaona mambo yote yamefanyika wakati wa benny. Huyu jamaa aliuza nchi hasa.
Ndiye huyu alikyewekwa mbele ya kanisa na kuambiwa 'ahsante kwa kuliongoza taifa kwa uadilifu' mara baada ya kustaafu.Sijui uadilifu ni upi maana uchafu wote umeanzia kwake.

Tunataka tujue wamiliki wa kiwanda,waliohusika kupiga mnada.
Wafadhili na Nyerere wlihangaika lakini Big B. akanadi kila kitu,sina hakika kama hakuna mkoa uliouzwa na hatujajua.

sasa macho yetu kwenye: EPA,RICHMONDULI,KIWIRA,MEREMETA,BUZWAGI,TICTS n.k. Wasituletee mambo ya kutuondoa katika mada kama kutumia msiba wa Wangwe kuleta mfarakano.
Tukomalie issue hizo.

Hivi jamani hakuna uwezekano wa kuondoa kinga benny apande kisutu japo kwa siku.!!!!!!

na wireless - 12.08.08 @ 03:51 | #29777

CHADEMA ni ******* na ni wauaji hao hawajui kitu chochote naomba msajili wa vyama vya siasa MHE TENDWA akifute hicho chama haraka sana

na dani, dar, - 12.08.08 @ 08:09 | #29788

wireless ufisadi ulipita kote tena walikula bila hata kufuta midomo na huo mchezo ulizoeleka sana wa kula jasho la walala wima
1.fedha za Gapex wadaiwa wote wazirejeshe orodha ipo hazina na vigogo wengi wamo kuanzia wa Mwanza, Iringa,Rombo na Dar
2.Mhe Rais ulifanikiwa kuzima mtandao wa ujambazi kwa kuwaondoa IGP na timu yake ya RPC'S na RCO's lakini walibaki akina Zombe na akina Tiba ambao leo hii kila corner ya Dar alijenga Hotel na fedha alikuwa anakusanya usiku
3.Mkataba mwingine wa kifisadi ni wa Mlimani City uchunguzwe na Mamvi na Ole nko wanahusika hadi zawadi za ALPHA
4.Ununuzi wa Helcopter na ndege za jeshi uchunguzwe la sivyo vijana wenzetu watazidi poteza maisha ni kazi nzuri za MTWARA corridor na mstaafu wa huko waziri wa ulinzi.
5.RICHMOND na NETWORK SOLUTION muasisi ndani ya B.O.T ni maganga na timu yake na aliwashirikisha watoto wa Chemkapa na Yona (Network) kisha akamchukua mtoto wa Mamvi baba tamaa(Richmonduli)Je si huyohuyo Maganga aliomba likizo bila malipo B.O.T ili wachote fedha za Network na wenzie ndani ya Tanesco.
6. B.O.T wakaanzisha uchafu tena mbaya wa kuwahonga warembo magari mekundu na meusi wakiongozwa na mkurugenzi wa Utawala.
7.Utazamwe pia usiri wa mkataba wa mgololo ulishinikizwa kwa watendaji wa idara ya misitu na vipengele vilipotoshwa ili huyo mkenya wa Bongo ajimilikishe kiwanda kama alivyofanya viwanda vya Chai na Pareto vyote amehusika.
8.Bw.Ngeleja na Bw.Adamu hamtoipata amani ya utawla wenu kama bado wapo watendaji Mkurugenzi na Naibu wake wa Nishati wanaijua sana siri ya RICHMOND na yale ya Msabaha kudhalilika na hadi kuitwa msemaji wa Tanesco kwa manufaa ya wachumia tumbo.
9.EPA iwekwe wazi tu wahusika chanzo ugomvi wa wahindi JITESHI, JEATU PATEL, ROSTAM NA MANJI wengine walionjeshwa tu na chanzo ni dau kubwa la KAGODO zile Bilion 40.wewe Rostam hata ukijifanya wataka kwepa na ulitaka hadi kumbambikizia Manji ili wewe unusurike ****** type.Na fedha zenu mlipitishia London kwa DK.Lipokola aliyewafungulia account na kuandaa michoro mkamlipa commission leo naye ananyea mtondoo.
11.RICHMOND ndiyo DOWANS na DOWANS ndiyo CASPIAN na hii kampuni ya Caspian inaendeshwa na mdogo wa ROSTAM aliyopo Dubaia miaka 5 iliyopita ilikuwa ndogo tu leo hii ni moja ya makampuni makubwa ya ujenzi kwa fedha za watanzania tena za kifisadi na hivi tujiulize huyo ROSTAM anafanya kazi gani haswa kazi kuzurura tu kwenye ofisi na kuwatishia viongozi ati yeye ndiyo LOWASSA na KIKWETE wa AWAMU YA NNE.
12.Mkataba mwingine wa kuuzwa hadi sehemu ya ardhi yetu ni ule wa kumgawia TUDOR JONES kile kipande cha Hifadhi ya serengeti na leo hii hadi ameweka jeshi lake na Kikewte anafumbia macho kwani BEN alijirekebishia na sasa hakuna mwenye uwezo wa kumzuia kuwanyanyasa ndugu zetu wa Mugumu.JE MKATABA HUO NAO?
13.Mkataba wa Ubinafsishaji wa Kagera Sugar tusidanganywe tu hao akina Super DOLL ni wasimamizi tu Kiwanda chao ni Mtibwa tuamke watanzania shime na harambee mie msongareli nilikaa kimya nikiwaangalia yepi mengine bado safari bado ndefu ila tutafika
14.Mzee Sumaye we pumzika kwa heshima na hizo njozi zako za urais we haya bwana asiyejua kata pua huunga wajihi tuachieni nchi yetu tutulize akili zetu.
TUMECHOKA KUNYANYASWA NA UNYANGAU HUU.WATU GANI MSIOWAZA WALA KUFIKIRI SOTE NI VIUMBE WA MUNGU NA TU MAVUMBI TU NA HUO UTAJIRI UTWASUTA MILELE.MNAKULA NA KUVIMBIANA KAMA NUNDA HUKU MWALA MIZOGA YA BINADAMU JE UWAPI WEWE BEN NA WAPAMBE WAKO HATA SURA MWAZIFICHA JE MWENYEZIMUNGU?

na m.msongareli, tz, - 12.08.08 @ 09:02 | #29797

DANI NI ********* WEWE TENA NI MAALAAAYA WA KIUME MBWAAAA WEWE.UNAZUNGUMZA UTUMBO WATU WANATOA TAKWIMU ZA UHAKIKA KUKOMBOA NCHI WEWE UNALETA MZAHA PUMBAFUUUUU KABISA WEWE.

na MTANZANIA, TANZANIA, - 12.08.08 @ 09:56 | #29809

Msisahau General Tyre ilichotewa fedha $10,000,000/= [12.5 bilioni] na NSSF kwaajili ya kununua mashine za kisasa lakini hakuna hata mashine moja iliyonunuliwa zaidi ya kupakwa rangi mashine za zamani.Basil Mramba alichotewa $1.5 milioni kwaajili ya kumalizia ujenzi wa hotel yake Kibo Palace.Kinachokera ni NSSF kuidai fedha General Tyre wakati wanajua aliyechota fedha ni Mramba na Kibo Palace Hotel.

na Halfan M, Sanawari,Tz, - 12.08.08 @ 10:15 | #29817

Nashukuru kwa namna ya kipekee swali alilouliza mtu mmoja aliyejiita PENDING'ULA akitaka maelezo ya jinsi kiwanda cha Mgololo kilivyouzwa kupitia mtandao moja wa jambo forum,Sasa limenoga! pamoja na maelezo ya utangulizi aliyopatiwa nadhani sasa ni wakati wa kutega masikio na kufuatilia mambo kwenye vyombo vya habari. Yote tisa Kumi serikali ya Awamu ya TATU imefanya mambo ya kinyama katika nchi hii hasa katika swala la ubinafsishaji. Walichokifanya jamaa hawa ndo kile kwa "Kinyalu" wanakiita "MAPALANGO". Hili ni tendo la kugawana mali baada ya mwenye mali kufariki. Taratibu za nani achukue nini hutegemea Nguvu za ushawishi tu na wala si uwezo wa kuendeleza mtaji.Katika tendo hilo kila mtu anatafuta faida binafsi. Serikali ya Awamu ya NNE mnatumia muda wenu mwingi kuwasemea mafisadi hawa. Bora muwaache watoe maelezo yao wenyewe. Iwe Kizimbani Poa! Iwe popote,Kuliko kujaribu kuwaosha hawa! Hawatakati hata sabuni nyingine wakiinywa! Kumbukeni hukumu yenu iko AROUND THE CORNER!

na mpulikage, iringa, - 12.08.08 @ 10:28 | #29819

DANI HAPO JUU ANAONYESHA JINSI GANI ANASHIKISHWA UKUTA. ANAGAWA KIUNO HUYO MBWA.


na nyumbu, TANZANIA, - 12.08.08 @ 10:48 | #29830

tena ikiwezekana hata wakifa mafisadi wakifa wasizikwe wawekwe mikumi waliwe na tai ili wasiwe na uhakika wa kwenda peponi.

na ramson, tz, - 12.08.08 @ 08:34 | #29857

Kwanza niungane na wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii ambayo Mwenyezi Mungu kwa utashi wake aliamua iwe yetu sote kwa asilimia mia moja.

Nawapongeza Wazalendo wote ambao kwa Uzalendo wao waliamua kutufumbua macho ili tujue jinsi nchi yetu hii inavyoporwa bila huruma na Watanzania wenzetu. Hapa nawapa pongezi nyingi waandishi wa habari pamoja na baadhi ya Waheshimiwa Wabunge waliyoamua kujitoa muhanga kwa kuupigia kelele ufisadi unaofanywa na baadhi ya viongozi wetu waliyoamua kutusaliti kwa manufaa yao binafsi.

Nawapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri kazi inayofidia gharama za masomo yaliyogharamiwa na taifa hili. Ninaridhika, kumbe rasli mali ya taifa hili iliyotumika kuwasomesha haikupotea bure.

Mimi ninawadai wanasheria wetu wote ukiondoa wachache kama akina Tundu Lisu. Mimi siyo mwanasheria lakini najiuliza hivi, hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoweza kutumiwa na wanasheria wetu katika umoja wao, kuwashtaki mahakamani kwa niaba ya Watanzania wote baadhi ya mafisadi waliyothibitika?

Ufike wakati wanasheria nao kama walivyo waandishi wa habari, kwa kutumia taaluma yao waliyopewa na taifa hili wajitoe muhanga kwa niaba yetu sote kuwafungulia mashitaka mafisadi wote waliyothibitika kama mchango wao kwa taifa letu lililotumia raslimali nyingi katika kuwasomesha. Akina Dr Slaa na wengine wanazo data zote muhimu kama ushahidi kilichobaki ni kwa wanasheria wetu kukusanya ushahidi ule na kufungua mashitaka mahakamani pale wanapoona inafaa kufanya hivyo.

Waandishi wa habari wamefungua njia basi wanasheria wetu nanyi mtuonyeshe umahili na Uzalendo wenu kwa nchi yetu.

na Mtemi E.J, Dodoma, - 12.08.08 @ 08:42 | #29861
 
wakuu ifikie wakati jipu hili lipatiwe uzito wa aina yake na litumbuliwe tuuu. Kila mwenye uchungu na taifa hili asiutazame bure uozo huu inatishaaa!
 
Nimejikuta Nafsi yangu imejawa Maneno ya kikatiri juu ya hii mijitu. Najizuia kutamka ama kuandika chochote!
Nanyi wapinzani hili suala liliishia wapi?
Mmeliacha njia panda madhara yake wastaafu wa SPM zaidi ya 70 wamepoteza uhai.
Magufuli tumbua hili licha ya kuwa ikulu ya magogoni inaingia lawamani kwa hili moja kwa moja
 
Thread zenye mashiko kama hzi huwa hazijadiliwi sijui kwanini aise
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom