QUALITY
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 853
- 115
Polisi wilayani Ngara wamevamia kijiji cha Mgoma, kata ya Mgoma na mkamata ndugu Peter Safari wa Kijiji cha Mgoma, kata ya Mgoma saa 8 za usiku wa kuamkia leo na kuondoka naye kusikojulikana. Wakati huo huo, walifika nyumbani kwa William Marco, ambaye walikuta hayupo nyumbani kwake usiku huo hivyo wamechukua pikipiki yake. Mpaka sasa Polisi wilayani Ngara haijatoa taarifa yoyote.
Tangu lini polisi wanakamata raia katika makazi yao saa 8 za usiku? Vibali walivipata wapi vya kukamata raia saa 8 za usiku? Huo ndio ulinzi wa amani au uhalifu wa amani? Taarifa hizi zinasikitisha. Ni dalili kuwa serikali kupitia kwa polisi inawanyanyasa raia jambo ambalo linaweza kuleta mchafuko. Ikumbukwe kuwa katika wiki mbili zilizopita, raia mmoja na Polisi wawili waliuawa katika kata ya mgoma na kituo cha polisi kuchomwa moto.
Tukipata taarifa zaidi, nitawaletea.
Source: Mimi mwenyewe nikiwa Ngara