Kagera: Kuna ajali mbaya ya moto imetokea Ngara,Malori mawili yateketea kwa moto huu huko ngara mpakani.
Chanzo cha ajali ni generator iliyokua inatumika kusukuma mafuta. Mpira ulichomoka ukasababisha moto.
Gari iliyoharibika ni ya Rwanda, iliyokuja kufaulisha mzigo ni ya Tanzania.
Kwenye ajali ya gari mtu mmoja ameungua na kunusurika kufa. Moto ulipolipuka, alikimbilia kwenye gari kutoa mizigo moto ukamzidia akashindwa kifungua mlango. Kwa bahati nzuri watu waliokuwa eneo la tukio wamemuokoa na kukimbizwa hospitali, alikua ni dereva wa moja ya gari kati ya hayo yaliyoungua.
Moto ulitokea Benaco-Rusumo mpakani mwa Rwanda na Tanzania