Kagera, Ngara: Magari ya Mizigo 5 na Trekta 1 yateketea kwa moto Rusumo

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi

ITV Breaking News, imetangaza ajali mbaya ya lori la mafuta mpaka wa Rusomo, ambapo lori hilo limegonga gari nyingine na kulipuka, hivyo kulipua magari mengine na hivi sasa yanateketea kwa moto.

Kamanda polisi eneo hilo ameeleza hivi sasa moto unaendelea kuteketeza magari!.

Sijui kama tuna magari ya fire kule mipakani.

Taarifa zaidi kuwajia.

P

======

UPDATES:

Magari matano ya mizigo na Trekta moja, yanateketea kwa moto katika kituo cha forodha Rusumo wilaya ya Ngara, mpakani mwa Tanzania na Rwanda, baada ya gari moja la mafuta ya petroli kuligonga gari jingine, polisi yathibitisha.

Mtu mmoja amefariki dunia kwa kuungulia ndani ya gari, na mwingine ni majeruhi yupo mahututi. Kapelekwa Hospitali ya Nyamiaga kwa matibabu zaidi.

Mkurugenzi wa Idara ya Mahusiano wa Makampani ya Said Salim Bakhresa, Hussein Sufiani amethibitisha kuteketea kwa moto magari manne kati ya matano yaliyokuwa yakitokea Rwanda kwenda bandari ya Dar es Salaam.

IMG_20180819_114603.png

Helkopta ya jeshi la Rwanda ikiwa angani eneo la rusumo wilaya ya Ngara mkoani Kagera ikizima moto ulioteketeza magari saba ya mizigo yaendayo Rwanda na DRC yakitokea hapa nchini. Moto huo ulisababisha pia kifo cha dereva na utingo kujeruhiwa
FB_IMG_1534691214546.jpg



Ngara. Dereva aliyeteketea kwa moto katika ajali ya gari katika kituo cha forodha Rusumo wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda ametambulika kuwa ni Abdalah Salimu (37) mkazi wa Dar es Salaam.

Pia, utingo aliyejeruhiwa ni Hajji Mohammed (22) naye mkazi wa Dar es Salaam baada ya gari aina ya scania mali ya kampuni ya Lake Oil kufeli breki na kugonga magari mengine saba yaliyosababisha kuteketea kwa moto pamoja na trekta moja leo asubuhi.
Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Amesema magari ya zimamoto kutoka Karagwe yalifika na kusaidiana na helikopta ya kijeshi ya Rwanda ikionyesha mahusiano ya ujirani mwema na kwamba shughuli za wananchi zimerejea kama kawaida.

"Juhudi zilizofanywa na kikosi cha zimamoto Karagwe na wenzetu kutoka Rwanda zimesaidia kwa haraka kuepusha madhara zaidi kwani ungeweza kusambaratisha hata nyumba kama moto ungezigusa nyaya za umeme" Amesema Olomi
Naye mkuu wa mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewashukuru viongozi wa Serikali ya Rwanda walioungana kutoa helikopta kuzima moto huo wakiwa na kikosi cha zimamoto kutoka wilayani Karagwe.

Kesho mkuu huyo wa mkoa atakuwa na ziara ya siku moja wilayani Ngara kujitambulisha kwa wananchi na watendaji wa Serikali baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu aliyestaafu
39664870_2084403218475268_6440543768067178496_n.jpg

Dereva aliyefariki kwenye ajali
 
Wanabodi

ITV Breaking News, imetangaza ajali mbaya ya lori la mafuta mpaka wa Rusomo, ambapo lori hilo limegonga gari nyingine na kulipuka, hivyo kulipua magari mengine na hivi sasa yanateketea kwa moto.

Kamanda polisi eneo hilo ameeleza hivi sasa moto unaendelea kuteketeza magari!.

Sijui kama tuna magari ya fire kule mipakani.

Taarifa zaidi kuwajia.

P
Mungu wangu :eek:
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom