NGAO - PRINCIPLE OF FIGHTING

Jenerali Ken

Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
81
Reaction score
71
1. NYEGERE - moyo wako lazima uwe imara na jasiri sana kama nyegere, usimuogope adui wa aina yoyote hata kama atakuwa na silaha ni kosa kubwa kumuogopa adui katika uwanja wa vita.

2. NYOKA - mapigo yako lazima yatoke kwa kasi na nguvu kama nyoka anavyo shambulia.

3. CHUI - 90% ya mapigo yako lazima yalenge katika shingo la adui kama chui anavyo shambulia, kisha maeo mengine ya kupiga ni koromeo, ubavu wa shingo, nyuma ya shingo, macho, pua, spinal code na korodani. Lengo la kanuni hii ni kumpatia shujaa wepesi wa kudhohofisha nguvu za adui, kumlemaza adui, kumshinda adui kwa muda wa sekunde 3 -5 tu, na ikibidi kumuua adui kabisa.

4. CHUMA - mwili wako, kuanzia miguu, mikono, tumbo, mgongo, mikono na mapigo yako lazima yote viwe imara kama chuma cha reli.

5. PAKA MWITU - macho yako lazima yawe makali kama ya paka mwitu anaevizia kitu.

6. SIMBA - kamwe usikubali kukaa katikati ya adui 2 - 3 - 4 - 6 wala zamani chini au kushughulika na adui mmoja kwa muda wa sekunde 2 - 3, shambulia geuka nyuma au upande au hama ulilopo na kumshambulia adui mwingine kwa kasi na nguvu zaidi kama simba anavyo pigana dhidi ya adui wengi.

7. TUMBILI - linda maeneo yako ya mwili ambayo ni dhaifu kwa kukwepa na kuzuia mashambulizi ya adui kama tumbili anavyolinda mwili wake dhidi ya mashambulizi ya nyoka.

8. MAZINGIRA - tumia mazingira uliyopo kama silaha au ngao ya kujikinga dhidi ya mashambulizi ya adui.

9. ADui - tumia adui mmoja ambaye ni dhaifu kama ngao ya kujikinga dhidi ya mashambulizi ya wenzake au njia ya kupita na kukimbia kama unaona hauna uwezo wa kukabiliana nao.

10. KIONGOZI - anza na adui kiongozi , ukimjeruhi wenzake wataingiwa na hofu na kuishiwa nguvu na watakimbia, wasipo kimbia basi watapunguza mashambulizi, watahofia kukushambulia. Hii itakutia nguvu ya kusavaivu na kukimbia hataro.

11. SILAHA - Tambua kila kitu katika uwanja wa vita ni silaha, kwa mfano kisu, shoka, mchanga, vumbi, mwavuli, unga wa pilipili, aridhi, miti, ukuta, nguzo za nyumba, nguo, pen, handbeg, mkanda na vitu vyote ni silaha.

12. ROHO YA SHUJAA - Kiai ni roho ya mpiganaji huongeza nguvu za mapigano, mori, ujasiri, humtia hofu adui na kumchanganya adui kisaikolojia. Kwaio nilazima shujaa utoe mlio wa vita kila utapo shambulia au kuzuia mashambulizi ya adui. Hakikisha unapo zuia shambulio anatoa mlio wa ( YAAAHHH !!! ) naunapo shambulia toa mlio wa ( HAA!! ) hii pia kiai ndio ufunguo wa kuifungua ki/chi ile nguvu ya ndani ya mpiganaji ambayo inatokana na sayansi ya mwili wa mwanadamu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…