NFL(Super Bowl) Halftime Show

Street Hustler

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,140
4,189
Ulishawahi kusikia au kuona Moja ya show kali ya muziki hapa dunian?
Screenshot_20230108-181238_1.jpg


Najua umeona ila je ya Super Bowl Halftime Show umeshatazama, hili ndio Gumzo Kila mwaka mpya unapoanza na tamati yake huwa February ya Kila mwaka.
Screenshot_20230108-181521_1.jpg

NFL Super Bowl ni mchezo maarafu huko Amerika ya kaskazini hasa katika mataifa ya Amerika na kanada, mchezo huu umeendelea kuvuta hisia za watazamaji wengi hasa kwenye kipengele cha halftime show hapa hualikwa wanamuziki kutoa burudani fupi na ya maana kwa muda mchache lakini huvuta hisia za watu wengi sana.

Tukio kubwa mwaka huu ni kuona mdhamini mpya anaekuja Apple music atafanya nini dhidi ya mdhamini wa awali alimaliza kwa shoo Kali mwaka 2022 ya wanamuziki (Eminem, Dr Dree, Snoop Dogg, Mary j Blige, 50cent na kandrak Lamar.) Hii inatajiwa ndio show Kali na kubwa iliotumia technologia kubwa ubunifu na performance Kali iliyovutia kwa muda wote wa NFL halftime show kutokea ambapo Pepsi alisimama kama mdhamini wa kuhakikisha mchezo na muziki vinafanyika pamoja katika eneo Moja.
Screenshot_20230108-180918_1.jpg


Ubunifuu umeleta ladha kubwa sana kwa wapenda burudani hasa wa michezo na muziki kujumuika kwa pamoja na inakadiriwa tiketi Moja ya kawaida n sawa 15million kwa kichwa kimoja huku Ile tiketi ya VIP ikikadiriwa kufika Hadi Zaid ya 100million hii unaeza dhan n utani lakini unaambiwa hyo n bei elekezi kwa ambao watafata utaratibu na kununua mapema sana lakini wale wazee wa deadline na wazee wa breaking news aisee utainunua hyo tiketi kwa mara mbili au Tano ya kiwango pendekezwa hii hufanyika kuanzia tarehe mwisho za January na mpaka siku Moja kabla ya mchezo husika kufanyika.

Kutokana na Pepsi kufanya show Kali sana hapa miaka 10 iliopita na kuwaweka kwenye list wasanii wote maarufu wakubwa kwenye stage ya NFL halftime show kama kina Eminem, Dree, Snoop, Michael Jackson, Shakira, J loo, Mary j Blige, Katy Perry, 50 cent, pitbull, na wengine wengi ambao waliliwakikisha jukwaa vyema.

Sasa ni muda wa Apple music 2023 mwaka huu 12 February katika viwanja vya State Farm Stadium in Glendale Arizona kufanya maajabu yake na msanii wake wa kwanza ambae amemuweka kwenye list n mwanamama Rihanna ambapo tayari ameshathibitisha kuwepo katika tamasha hilo la historia ya Apple music kwenye michezo hapa dunian. Ni kawaida kuona mwanamuziki akisindikizwa na Lebo yake kama ilivuokuwa kina Eminem na Dree walivyofanya na aftermath Record je mwaka huu Rihanna atapanda na Roc nation?
Screenshot_20230108-182149_1.jpg

Je wewe unafahamu nini kuhusu NFL HALFTIME SHOW karibu utujuze.
 
Back
Top Bottom