Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,956
- 22,148
Newcastle na Middlesbrough zashuka daraja ligi ya Uingereza
Kevin Nolan wa Newcastle akiwa haamini kama wameshuka daraja Sunday, May 24, 2009 9:04 PM
Ligi ya Uingereza imeisha leo kwa timu ya Newcastle kushuka daraja baada ya miaka 16 katika ligi kuu ya Uingereza na sasa Newcastle itaungana na Middlesbrough na West Bromwich Albion kucheza ligi daraja la kwanza mwakani. Newcastle United ilishindwa kuwika mbele ya Aston Villa na kukubali kipigo cha bao 1-0 na hivyo kuhitimisha miaka yao 16 katika ligi kuu ya Uingereza.
Newcastle iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kubaki ligi kuu ya Uingereza ikitegemea Hull City itafungwa na Manchester United na wao kushinda mechi yao na Aston Villa.
Mambo yalikuwa si mambo pale Hull City ilipobanjuliwa 1-0 na Manchester na Newcastle nayo kushindwa kuitumia nafasi hiyo na matokeo yake na wao pia wakalala 1-0 kwa goli la kujifunga la Damien Duff katika dakika ya 38.
Damien Duff alijifunga baada ya kumpoteza maboya golikipa wake Steve Harper wakati akijaribu kuzuia shuti la Gareth Barry.
Middlesbrough nayo iliingia uwanjani ikiwa na matumaini duni ya kubakia ligi hiyo mwakani na kuonyesha kiwango duni mbele ya West Ham kilichopelekea walale 2-1.
Hakuna mtu aliyekuwa na furaha leo baada ya filimbi ya mwisho ya kumalizika kwa ligi ya Uingereza kama kocha wa Hull City, Phil Brown .
Pamoja na kwamba Hull City ilikuwa imelala 1-0 kwa Manchester United, Phil Brown alishangilia utadhania amechukua kombe la ligi ya Uingereza baada ya kupata uhakika kwamba timu yake itacheza kwa mara nyingine ligi kuu ya Uingereza mwakani.