New York: Imamu na Imamu msaidizi wauwawa

New York: Imamu na Imamu msaidizi wauwawa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,277
Polisi mjini New York, Marekani, wanachunguza mauaji ya Imamu wa kiislaam pamoja na msaidizi wake katika eneo la Queens.

Imamu Mualama Akonjee pamoja na Tharam Uddin walipigwa risasi nyuma ya kichwa, wakati wakielekea nyumbani baada ya swala hapo jana.

Maimamu hao walipigwa risasi kichwani kwa karibu na mshambulizi aliyewavizia kutoka nyuma.

Walipelekwa hospitalini japo waliaga dunia muda mfupi baadaye.

Imamu Mualama Akonjee, 55 aliwasili New York miaka mawili iliyopita kutoka Bangladesh.

Shambulizi hilo lililotokea mchana, limeshtua jamii ya waislamu katika eneo hilo.

Baada ya waumini wa dini ya kiislaam wametaja shambulizi hilo kuwa la chuki dhidi ya dini ya kiislaam, na kumlaumu mwaniaji wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwa kuchochea chuki dhidi ya waislamu.

"Maimamu hao walikuwa wanapendwa sana walikuwa viongozi wa jamii " Afaf Nasher, afisa wa baraza la uhusiano mwema wa Marekani na waislamu ameambia shirika la habari la Reuters." Kuna maombolezo na kilio kikubwa cha haki.

Hata hivyo maafisa wa polisi wanasema kwamba bado hawajadhibitisha nia ama lengo la shambulizi hilo, na kwamba hawawezi kudhibitisha kwa uwazi kwamba waliuwawa kutokana na imani yao.

Chanzo :BBC
 
'Wanaanza kumshutumu muwania urais mtata DONALD TRUMP kueneza chuki dhidi ya waislamu'?
Kwahivyo Matamshi tata ya Trump dhidi ya waislamu sio tatizo kwako..!?
 
Mkuu, yanaweza kuwa tatizo lakini yasiwe chanzo cha haya mauaji.
Moto mkubwa huanza na cheche..!

Kuuliwa kwa watu weusi marekani chanzo ni ubaguzi wa rangi.

Na sasa kama maimamu wanauliwa kwa risasi hivyo na wala sio wanasiasa, bila shaka chanzo ni chuki dhidi ya waislamu.
 
Back
Top Bottom