Mziki unabadilika kulingana na soko linahitaji nini..? Ndio maana unakuta tz kipindi hiko nyuma tulikuwa tunazielewa sana flavour za South, ila sikuhizi huwaambii watu kuhusu flavour za Nigeria..
Wa zamani upo poa, ila wa sasa upo poa zaidi..
Kuhusu kukaa sana kwa wimbo inakuwa tufauti kwasababu ya maendeleo ya teknolojia. Mpaka mtu uisikie au kuangalia wimbo source inaweza kuwa simu, computer, TV, radio, na mitaani clubs, pikipiki, mabasi n.k kitu kinachofanya wimbo uliohit sana kwa siku hizi kutokukaa sana masikioni sababu karibu kila sehemu unaweza ukausikia, at the same time umeweka ringtone, unasikia kwenye ringback tune, youtube unaangalia muda wowote, unao kwenye simu audio na video, na simu ina redio na redio zipo nyingi saana inakuwa rahisi wimbo kusikika zaidi kwa wadau, automatically utazoeleka tu....!!