Hizi CPU mpya kama sikosei wanaweka Transistor zenye nguvu sana na hivyo zinatumia nguvu kidogo ya umeme ila hiyo haimaanishi kuwa hazitumii FAN. Ni lazima zitumie FAN na hiyo fan ikisimama, hata sekunde moja haiishi, inazima Computer yote ili kulinda CPU isiungue.
HP zina matatizo sana inavyokuja kwenye Cooling System. Usubiri mwaka ukiisha, basi njoo hapa tuongee maana utaanza kukaanga Mayai kwenye Computer yako. Dawa pekee inayobaki ni kuwa kila baada ya mwaka, ni vema kuipeleka Service na wanaisafisha. Labda kama unakaa sehemu safi sana, basi itadumu kidogo, vinginevyo, vumbi ndani litakuwa kubwa na kuifanya Fan isifanye kazi vizuri na hapo heating inaanza ya nguvu sana.