figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,175
- 64,552
Nesi Maria (kushoto) mara baada ya kunaswa na OFM
yamekuwa hayaripotiwi kutokana na usiri wa wahusika kutaka mambo yao yasiwekwe hadharani lakini
Oparesheni Fichua Maovu (OFM), inaendelea kufichua unyama huo na kuumwaga hadharani.
Mara kadhaa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, chini ya Waziri Sophia Simba imekuwa ikikemea
tabia mbaya ya baadhi ya manesi kutumia vibaya taaluma yao na kuendeleza mauaji hayo.
SAFARI HII NI MBAGALA
Baadhi ya wazazi wanaoishi Mbagala Kizuiani jijini Dar waliochoshwa na tabia ya manesi kuua vichanga,
walipiga simu OFM na kulalamikia vitendo vilivyokithiri vya utoaji mimba katika dispensari iliyopo maeneo yao.
OFM iliambiwa kuwa dispensari hiyo ina manesi wengi wenye ujuzi na fani yao lakini shughuli kubwa
wanayoifanya ni kutoa mimba ili kujipatia fedha kwa njia haramu.
Manesi wa kike wanafanya shughuli za kuua vichanga ambavyo bado havijapata ruhusa ya kuingia duniani, kwa
kweli inauma sana, alisema mmoja wa wazazi hao.
Taarifa
Nesi Maria akiwa katika harakati za kuandaa sindano ya ganzi na vifaa vingine kufanikisha zoezi la kutoa mimba
zikasema kwamba manesi hao wapo wengi lakini anayefahamika zaidi ni Maria ambaye amejizolea umaarufu kwa
kazi hiyo katika eneo lote la Mbagala.
Ni muda mrefu amekuwa akifanya mchezo huo, tena anafanya shughuli zake bila ya hofu utadhani vitendo hivyo
vimeruhusiwa na mamlaka husika, aliongeza mzazi mwingine.
OFM IMEJENGA HESHIMA
Wazazi hao wamesema kuwa wanaamini kuwa Maria atanaswa kama alivyonaswa Dokta Mambo wa Kawe jijini
Dar ambaye naye alikuwa maarufu kwa shughuli kama hizo lakini OFM ikamshikisha adabu.
Baada ya kutoa maelezo hayo, mmoja wa wazazi hao alitoa namba ya simu ya Maria kwa kamanda mkuu wa
OFM.
MTEGO WAANDALIWA
Kamanda Mkuu wa OFM alimpigia simu Maria na kumwambia kuwa alikuwa akitaka huduma ya kumtoa mimba
mke wa mtu aliyempa kwa bahati mbaya kabla mumewe hajarudi kutoka safarini.
Maria: Hakuna shaka wee njoo tu dispensari kwetu, si umeelekezwa?
Kamanda: Ndiyo.
Maria: Njoo basi tumalize kazi leoleo.
Kamanda: Hiyo kazi inaweza kufanyika kwa ufasaha?
Maria: Miye huwa sishindwi na chochote, wee njoo utafurahi kwa huduma yangu lakini wahi kwani namaliza
shifti jioni.
OFM YAJIPANGA
Baada ya maelezo hayo, kamanda wa OFM akaanza kuwapanga vijana wake kwa ajili ya kumnasa Maria katika
mtego huo siku hiyohiyo ya Machi 15, mwaka huu.
Mmoja kati ya vijana waliopangwa katika zoezi hilo ni mwanamke mjazito ambaye alitolewa hofu kwamba mimba
yake haitatolewa na OFM watakuwa wameshavamia katika chumba cha utoaji mimba.
Pia, OFM iliwasiliana na polisi wa Kituo cha Mbagala Kizuiani kwa lengo la kumkamata Maria.
MCHEZO MZIMA
Saa tisa mchana, OFM walikuwa wametanda katika dispensari husika wakiwa na askari waliokuwa wamevaa
nguo za kiraia.
KAMANDA ATINGA FRONTI
Baada ya kupeana ishara za kikazi, OFM na baadhi ya polisi waliingia ndani ya dispensari hiyo kwa nyakati
tofauti huku wakijifanya ni wagonjwa.
Baadhi yao walijidai wamefika hapo kwa ajili ya kupima malaria huku wakimuacha kamanda mkuu wa OFM
akisonga fronti akiongozana na binti anayetakiwa kutolewa mimba.
NESI MARIA AITWA MAPOKEZI
Kamanda wa OFM alipofika mapokezi ya dispensari hiyo, alipokewa na kusema shida yake ilikuwa ni kuonana
na nesi Maria.
Bila ya kinyongo wafanyakazi wa mapokezi waliwasiliana na Maria ambaye naye alimtuma msaidizi wake
aitwaye Maimuna kuwapokea wageni hao kisha kuwapeleka katika chumba maalum.
Maimuna alizungumza na kamanda na kuanza kuelewana kuhusu malipo ya kazi hiyo ya utoaji mimba.
Maimuna: Huwa tunatoa huduma hiyo kwa shilingi 80,000.
Kamanda: Dah! Miye nina shilingi 50,000.
Maimuna: Ongeza kidogo maana ni kazi ngumu sana.
Kamanda: Naomba mnisaidie tafadhali.
Baada ya maongezi ya muda mrefu, Maimuna alikubali kupokea shilingi 50,000 na kuanza kumpima mjamzito
baada ya kumuelekeza kupanda kitandani kwa ajili ya maandalizi ya zoezi zima la utoaji mimba.
MIMBA YA MIEZI MIWILI
Vipimo vya dispensari hiyo vilionesha kuwa ujauzito ulikuwa na umri wa miezi miwili, Maimuna akatoka na
kwenda kuchemsha vifaa vya kazi.
SINDANO TATU ZAANDALIWA
Katika chumba maalum cha kutolea mimba, Maimuna aliweka vifaa vyote zikiwemo sindano tatu za ganzi
alizokuwa achomwe mjamzito huyo ili asisikie maumivu.
MARIA AINGIA MZIMAMZIMA
Baada ya Maimuna kukamilisha kazi yake, aliendelea kubaki kwenye chumba maalum, ndipo Maria akaingia
chumbani humo mzimazima akitaka kukamilisha kazi yake.
Kamanda wa OFM alipiga hesabu zake na kutoa ishara maalum kwa wenzake waliokuwa nje ili wavamie kwa
kuwa mtego ulikuwa umeshakamilika.
Nesi Maria akijuta mara baada ya kunaswa na OFM
MARIA APIGWA NA BUTWAA
Akiwa haelewi kilichokuwa kikiendelea, Maria alipigwa na butwaa alipoona amevamiwa chumbani humo na watu
asiowajua.
Taharuki yake ikamfanya ahisi kuwa alikuwa amenasa kwenye mikono ya OFM baada ya kuona kamera zikifanya
kazi yake.
ALIJUA ATANASWA
OFM na askari walijitambulisha lakini Maria aliomba sana asitolewe gazetini.
Chondechonde msinitoe gazetini kwani yatakuwa ni kama yale ya Dokta Mambo, alisema akiwa ametahayari.
Alipoulizwa kama alikuwa akifahamu kilichomkuta Dokta Mambo, Maria alisema aliposoma habari ya dokta huyo
alijua kuwa naye kuna siku angenasa ila hakujua ni lini.
Ama kweli nimepatikana, yaani kama mlivyomnasa Dokta Mambo, nilijua tu kwamba lazima siku moja na mimi
nitanaswa na OFM, kweli sitarudia tena, alisema Maria akiomba mambo yaishe palepale.
Baada ya OFM kumaliza kazi yao, waliwaachia polisi ambao waliwachukua Maria na Maimuna na kuwapeleka
kituoni.
DAKTARI WA MUHIMBILI ATAJWA
Hata hivyo, Maria alimtaja daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (jina tunalo) kuwa ndiye
anayehusika na dispensari hiyo.
Alipotakiwa kumpigia simu na kumtaka afike dispensari hapo, daktari huyo alikubali kufika kabla ya saa 11 jioni
lakini hadi saa mbili usiku hakuwa ametia mguu wake.
Uchunguzi umebaini kuwa huenda alipenyezewa taarifa za kilichotokea na kushauriwa kutofika kwenye
dispensari kukwepa msala huo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Engelbert Kiondo hakupatikana kuzungumzia tukio hilo, ingawa
mmoja wa wasaidizi wake ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.
KUTOKA KWA MHARIRI
Bado OFM iko kazini na kamwe haitalala, Maria alijua iko siku atanaswa ila hakujua siku wala saa, bado wewe
ambaye unadhani hatutakukamata! Itafika zamu yako, acha kufanya uovu na mambo yasiyokubalika katika jamii.
source;Habari5