Neo wazalisha battery ya gari inahimili kilometres 1000+

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,938
Kampuni ya magari ya umeme ya China imetengeneza betri ambayo inawezesha gari kutembea zaidi ya Kilomita 1,000 bila kuhitaji chaji.

Umbali huu ni sawa na kutoka Dar mpaka Shinyanga bila kuchaji gari. Au ni sawa na kusafiri Dar mpaka Arusha; au kutoka Dar na kwenda Dodoma, na kurudi tena Dar bila kuchaji gari.

Kampuni ya Neo, ni kampuni ya China ambayo inashindana na Tesla, wiki hii CEO wake ambaye pia ndio muanzilishi wa kampuni hiyo Ameifanyia majaribio kwa kuendesha gari ya Neo ET7 kwa masaa 14 na kutembea Kilomita 1,044 kutoka Mji mmoja wa China kwenda katika mji mwingine bila kuichaji na ikabaki 3% ya charge akiwa amefika katika mji mwingine.

Neo pia ni kampuni ambayo inatumia betri ambazo unaweza kuitoa na kuweka battery nyingine, swapp betri iliyochajiwa, zinabadilishika bure; na inaruhusu mtu binafsi kununua aina mbalimbali za betri ambazo zina aina mbalimbali za uwezo. Tofauti na Tesla ambayo hauwezi kubadilisha betri yake. Pia ina gari ya umeme inayoongoza kwa speed.

China inaongoza katika teknolojia za betri za magari ya umeme na Neo imekuwa ni mfano mkubwa wa maendeleo yake. Neo itaanza uzalishaji wa betri hiyo ya 150kWh kuanzia April 2024.

Gharama ya betri hiyo ni dola 42,100$ ambayo ni sawa na gharama ya Tesla Model-Y nchini China.

______________
#Teknolojia #Neo
FB_IMG_1704111939630.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona Jana kampuni ya Tesla wanafanyia majaribio gari ya Kwanza itakayotembea KM 650 bila kuchaji kumbe wenzao china wameshavuka Huko na wako mbali zaidi..
China kwenye ishu za magari umeme ataiteka dunia Sana hasa magari yake ya bei cheeee!
Niliona kituo cha kuchaji Gari kwa kutumia umeme wanatumia Jenerata kurecharge ile system yao umeme ulikatika sijui... ndo nkaamini mwarabuu hakwepeki
 
Niliona kituo cha kuchaji Gari kwa kutumia umeme wanatumia Jenerata kurecharge ile system yao umeme ulikatika sijui... ndo nkaamini mwarabuu hakwepeki
Mfumo wa kuchaji Una faults nyingi ikiwemo battery zenyewe kuzingua Kwa muda mfupi hata warranty ya hizo battery ni miaka michache Sana..
Haya magari yakiingia kama used tutakuwa tunachaji zaidi ya mara 4 Kwa siku yaani ukitoka kariakoo Hadi ubungo unachaji na ukirudi Hadi buguruni unachaji
 
China kwenye ishu za magari umeme ataiteka dunia Sana hasa magari yake ya bei cheeee!
China wako serious sana na magari ya umeme (EV)

Mpaka makampuni ya kutengeneza simu kama HUAWEI na XIAOMI wameingia kwenye EV

HUAWEI wao wameinvest zaidi kwenye kuuza teknolojoa ya AI driving system kwa makampuni ya kutengeneza magari ya umeme China

XIAOMI Dec 28, 2023 walizindua gari yao ya kwanza ya umeme hivi karibuni wataanza production rasmi
 
Mfumo wa kuchaji Una faults nyingi ikiwemo battery zenyewe kuzingua Kwa muda mfupi hata warranty ya hizo battery ni miaka michache Sana..
Haya magari yakiingia kama used tutakuwa tunachaji zaidi ya mara 4 Kwa siku yaani ukitoka kariakoo Hadi ubungo unachaji na ukirudi Hadi buguruni unachaji
Na mengine si hutengenezwa kulingana na hali za hewa za huko?

Vipi hizo betri haziathiriwa na mabadiliko hayo, maana hizi simu tu nyingine huku kwenye joto ni kipengele.
Na ikiwa used si ni balaa kabis hilo.
 
Kenya wameanza kutumia mabasi ya umeme ya kampuni ya BYD kutoka China, hawalalamiki

250km in a single charge

Wabongo tuna ujuaji mwingi sana
 
Gharama ya betri hiyo ni dola 42,100$ ambayo ni sawa na gharama ya Tesla Model-Y nchini China.

Sent using Jamii Forums mobile app
42,100 usd tu GT? Nampango wa kuzinunua hizo betri kama elfu moja hivi.

Elon Musk namchukia sana anajifanyaga kama Mungu mtu. Halafu hana fadhila kwa bara lililomleta duniani na kumtoa. Acha sasa wachina wamfundishe adani na siyo China tu Korea kusini Kia na Hyundai watatoa magari ya umeme yenye bei nafuu.
 
Back
Top Bottom