Jana nilikuwa naangalia Kipindi cha malumbano ya hoja kinachorushwa na kituo kimoja maarufu cha TV nchini ambacho kwa sasa kinajiita Super Brand Afrika ya Mashariki na kati
.Katika malumbano yale kuna Bwana mmoja ambaye nilimuona kama mambo ya uchumi anayafahanu vizuri.Akashusha nondo za kutosha halafu mwishoni akawa anasema kwa sasa tuna uchumi uchwara akarudia maneno haya.Baada ya kumaliza mwongozaji wa kipindi akawa anajaribu kulikataa neno uchwara kiaina akidai ni mapema kuuita uchumi wa Tanzania "Uchumi Uchwara" (obvious kwa kuogopa kituo kufungiwa) Nikawa najiuliza neno Uchwara ni tusi au?