Neno la Prof.. Joseph Mbele.. Kuhusu CCM na Membe

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,793
NENO KUHUSU CCM NA MEMBE

Mengi yamesemwa kuhusu suala la CCM na Membe. Mambo yanayowahusu CCM wabaki nayo wenyewe. Ila ninaona wanavuka mipaka. Mtu wa CCM anapotoa ujumbe kuhusu suala la Membe na katika ujumbe huo anawalenga sio wanaCCM tu, bali waTanzania kwa ujumla, anapaswa awe makini.

Tunawasikia wakielezea utaratibu wao ndani ya CCM, kwamba rais aliyeko madarakani anakuwa mgombea kwa kipindi cha pili. Wanatueleza kwamba suala la Membe ni kuwa anasemekana anawania kugombea mwaka 2020, kinyume na utaratibu wa CCM.

Nasema kwamba wanaCCM wawe makini. Huu utaratibu wao ni wao. Sisi wengine hautuhusu na hauna maana yoyote kwetu. Tunaitambua katiba ya Tanzania, ambayo inasema kwamba kipindi cha urais ni miaka mitano. Inapoisha miaka mitano, unafanyika uchaguzi upya. Kama CCM wanamweka rais aliyeko agombee tena, hiyo ni hiari yao.

Ila kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mTanzania yeyote mwenye vigezo anaruhusiwa kugombea. Kwa hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, sisi tukimwona mtu tofauti kutoka CCM akitangaza nia ya kugombea, tunaona ni sawa tu, kwani anatumia haki yake ya kikatiba.

Kwa hivyo, mtu wa CCM anapotoa ujumbe kuhusu suala la Membe, akumbuke kuwa anapoteza muda anapodhani tuna haja na ujumbe wake. Aishie huko huko CCM.

Huu utaratibu wenyewe wa CCM sikuufahamu kabla. Ila sasa baada ya kuufahamu, nimeushangaa. Je, iwapo rais katika awamu yake ya kwanza akionekana kuwa hawezi kazi, kwa nini CCM wasimchague mgombea tofauti? Je, iwapo katika awamu ya kwanza ya rais, wakajitokeza watu ndani ya CCM ambao wanaonekana kuwa bora zaidi ya rais aliyeko, CCM watang'ang'ania tu kwamba wafuate utaratibu wao, yaani nchi ikose rais bora kwa sababu tu ya utaratibu ndani ya CCM?

Kuna mtu mmoja wa CCM amekuja na ujumbe wake mtandaoni ambamo anaelezea kuchukizwa kabisa na mambo yanayosemekana amefanya Membe. Amesema kwamba Membe kuongelea kugombea urais mwaka 2020 ni kumvuruga mawazo Rais Magufuli, ambaye anapaswa aachwe aendelee na utekelezaji wa ajenda yake.

Ujumbe wa mtu huyu ni wa ajabu na wa kipuuzi. Je ni kweli kwamba mtu kutangaza nia ya kugombea mwaka 2020 kutamkwaza Rais Magufuli? Yaani Rais Magufuli hafahamu kuwa kwa mujibu wa katiba, kipindi chake kinaisha mwaka 2020? Huko ni kumdhalilisha Rais Magufuli. Rais Magufuli hayuko hivyo. Pale Rais Magufuli aliposema shughuli za siasa zisubiri hadi mwaka 2020 alionyesha wazi kuwa anafahamu kwamba kuna uchaguzi mwaka 2020.

Watu wa CCM wanavyoongelea suala hili la Membe napata picha kwamba kuna kitu nyuma ya pazia. Inakuwa kwamba wamepania kuwa mgombea wao, ambaye ni rais aliyeko madarakani, ataendelea kuwa madarakani. Hiyo ni hisia niliyo nayo kutokana na jinsi watu hao wa CCM wanavyojieleza.

Nikizingatia kuwa kuna tuhuma nyingi dhidi ya CCM kuhusiana na chaguzi, hasa tuhuma za kutumia tume ya uchaguzi, na nguvu za dola, ninazidi kupata wasi wasi kuhusu nia ya CCM.

Mimi sijui kama Rais Magufuli atataka kugombea tena. Nimemsikia mara kwa mara akisema kuwa kazi ya urais ni ngumu kuliko alivyotegemea. Nimemsikia akisema alisukumizwa huu wadhifa. Nimemsikia akisema kuwa wakati mwingine anakuwa na "frustrations." Kwangu hivi ni viashiria kuwa huenda asitake kugombea tena. Je, akiamua hivyo, CCM wanataka wamsukumize tena?

Sina uhakika. Lakini lazima nijiulize, je, akiamua kwamba awamu moja imetosha, kwa nini asiwe huru kabisa kujiweka pembeni na akina Membe au wengine huko CCM wakachukua fomu na wapate mgombea ambaye atachuana na wenzao wa vyama vingine?

Narudia hoja yangu. CCM wawe makini na kauli zao. Mgogoro wao hauna uzito kitaifa wanavyodhania. Ni sawa na migogoro katika vyama vingine. Tanzania ni kubwa na ina uzito kuliko chama chochote. Tunafuata katiba ya nchi, si utaratibu wa chama. Mgogoro wa CCM na Membe si chochote kwa msingi huo, bali ni "a storm in a teacup," yaani dhoruba katika kikombe cha chai.
 
Hii ni propaganda tunatengenezewa yaani kufanya katiba ya CCM ndio iwe kama katiba ya Taifa zim
Alafu kugombea kwa Membe au kutangaza kwake nia kuna mnyima vipi Raisi usingizi? Kama Raisi Yuko fair kwa wAtu wake hata aje Nani agombee tutamtetea mpaka arudi madarakani,Mke anayetoka vizuri wajibu kwa mme wake haogopi mke mwenza maana anajiamini
 
Koryo2 yaani clasmate mwaka 1978? Are you still alive? Mmmmh
Hongera sana Prof.Mbele kwa kusema ukweli usiopingika.nakufahamu vizuri sana kama classmate wangu pale UDSM mwaka 1978 mpaka 1981. Hata darasani ulikuwa mtu wa msimamo sana. Maprofessa endeleeni kusimamia ukweli.
 
Huyo profesa kasikia wapi hayo anayosema?
Halafu ni profesa wa nini?
 
Kazi na Bata
IMG-20181207-WA0156.jpeg
 
Hii ni propaganda tunatengenezewa yaani kufanya katiba ya CCM ndio iwe kama katiba ya Taifa zim
Alafu kugombea kwa Membe au kutangaza kwake nia kuna mnyima vipi Raisi usingizi? Kama Raisi Yuko fair kwa wAtu wake hata aje Nani agombee tutamtetea mpaka arudi madarakani,Mke anayetoka vizuri wajibu kwa mme wake haogopi mke mwenza maana anajiamini
Musiba anakereketwa
 
Back
Top Bottom