Ndugu zangu,
Tumeingia mwaka 2017. Maisha binafsi na ya taifa lazima yasonge mbele.
Ni kwa kutekeleza kwa vitendo yale tuliyoazimia, kwa binafsi yetu na kama taifa.
Kuna ya kujifunza kutoka maisha ya tembo. Msafara wa tembo huwa na kawaida ya kutorudi nyuma. Ndio maana porini huzioni nyayo za tembo zenye kwenda mbele na kurudi nyuma.
Ni ukweli, kuwa tembo ni mnyama mkubwa na ndiye mfalme wa pori. Lakini, hufika mahali tembo akasumbuliwa na siafu kiasi cha kuweweseka na hata kutamani kulihama pori.
Ni kwa kosa la tembo kukanyaga kichuguu cha siafu.
Naam, siafu mia tano ni wengi kuliko tembo mmoja, pamoja na ukubwa wa tembo.
Adili ya jambo hili ni ukweli kuwa hapa duniani mkubwa anapaswa kumuheshimu mdogo, na mdogo pia kumuheshimu mkubwa. Hivyo, wanadamu tunapaswa kuheshimiana.
Kwenye ngazi ya taifa tuwe na mtazamo wa timu ya mpira. Timu bora ni ile yenye uwezo wa kushindana. Maana, timu inaweza kushindana ikiwa haina uwezo wa kushindana kuweza kushinda na kupata inachokitaka. Duniani hapa kuna tofauti ya kushiriki kushindana na kuwa na uwezo wa kushindana.
Ndio maana kwenye Fifa kila nchi mwanachama hupewa nafasi ya kushindania kucheza kombe la dunia. Hata hivyo, ni timu zile zenye uwezo wa kushindana ndizo hufika hatua za mbali kwenye kushindania kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia. Nyingi hupukutikia hatua za mwanzoni tu za mtoano.
Tanzania ni nchi yetu. Tuna wajibu, bila kujali tofauti zetu za kiitikadi na kimitazamo. Bila kujali ni Serikali ya chama gani iko madarakani, kufanya yote kuhakikisha tunaisadia Serikali iliyo madarakani ifanikiwe katika kuifanya nchi yetu kuwa yenye uwezo wa kiushindani kwenye dunia ya ushindani.
Huko ni kutimiza wajibu wetu wa kizalendo kwa nchi tuliyozaliwa na tunayoipenda.
Tuendelee kutekeleza wajibu huu kwenye mwaka huu wa 2017 na inayokuja.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania.
Happy New Year!
Maggid Mjengwa.
Iringa.