Neno La Leo: N'na Tui Jikoni!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu Zangu,


KWANZA, kama Watanzania, tupeane pole kwa msiba mkubwa ulotufika; milipuko ya mabomu Gongo La Mboto.


Nimeona picha za kwenye runinga, magazetini, mitandaoni. Nimesoma magazetini na kuwasikiliza watu mitaani. Hakika, ni huzuni kubwa kwetu sote. Huu ni wakati wa kuizunguka bendera yetu, kuwa wamoja kama Watanzania. Huu si wakati wa kuziangalia bendera za vyama na kutafuta mitaji ya kisiasa katikati ya msiba huu.


Na kila tukio lina tafsiri yake. Miye ninayo, inakuja, panapo majaliwa kesho au keshokutwa. Maana wakti huu nimetingwa sana kibaruani kwangu. Jamani mwenzenu n'na tui jikoni. Si tui la nazi, watu wa pwani mnaijua hulka ya tui. Yanibidi n'kae karibu nalo. Nalikorogea lisije katika ati. Wali wangu ukishaiva n'tawajulisha, inshallah.


Alaa, sina maskhara miye, na mchele n'shauchagua, nimeupeta pia. Ungo mmoja, chenga nyuma, mchele mbele. Na nimeshauloweka kitambo, nasubiria tui lichemke, lisikatike, ndo salama ya wali wangu.



Maana, kuna tofauti ya mpunga, mchele, ubwabwa na wali. Pale Nairobi niliwahi kuulizia wali nikaambiwa hakuna, hapo palikuwa na mchele! Nikaagizia ' mchele'. Walahi radhimu, nikaletewa 'ubwabwa'!


Tuje ya Gongo La Mboto na tafsiri yangu subiriwa. Miye hiyo kesho au keshokutwa nitaanza tafsiri yangu na kisa cha Bwana Habib Makolokolo. Mliokulia Ilala, Dar miaka ile ya 70 katikati mtamkumbuka Bwana huyu, Habib Makolokolo.



Bwana Habib Makolokolo alikuwa akifanya biashara zake mlango wa pili baada ya ilipo Afisi ya Posta pale Amana.


Habib Makolokolo alikuwa mtu maarufu sana, kwanini? Mtajua kesho au keshokutwa. Ndio, Ilala ilikuwa ni makazi ya watu wa tabaka la Wafanyakazi. Si mnajua, ndo maana NUTA JAZZ Band ilikuwa na makao yake pale pale Amana Club. Kuwaburudisha Wafanyakazi na Msondo wa NUTA, ngoma ya Asili, wakitaka kufurahi!


Jamani, nisiwamalizie uhondo, isubirini tafsiri yangu na mwone ni vipi Bwana Habib Makolokolo ameingia kwenye tafsiri yangu ya kilichotokea Gongo La Mboto. Inshallah, panapo majaaliwa. Ngoja kwanza niendelee kukorogea, si n'shawaambia; ' N'na Tui Jikoni!' Na hili liwe Neno La Leo.
Maggid
Iringa,
Jumapili, Februari 20, 2011
mjengwa
 
Hakika nimeshindwa kuelewa lengo lako hasa ni nini kaka Maggid.
Maybe acha nisubiri hilo tui lako ulitoe hapo jikoni kisha umalizie hii hadithi
 
Back
Top Bottom