Neno la Leo: Kwa Wadada na Wakaka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno la Leo: Kwa Wadada na Wakaka.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sizinga, Aug 14, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mungu katuumba wanadamu na kutupatia akili kumiliki na kutawala viumbe vyote vilivyopo ardhini. Mwanadamu katika uumbaji alikuwa mwa mwisho na baadae Mungu akapumzika na kuangalia vitu vyake vilivyo vyema machoni pake. Uumbaji huu wa aina yake, wa kufanana na yeye aliye juu umetukuka na yeye Mungu akaona vyema na akasema zaeni mkaongezeke mkaiijaze dunia.

  Sasa cha kushangaza tunachokiona hapa duniani sasa hivi, wanadada wengi na wakak pia, wanabadilisha ngozi zao zilizoumbwa na mwenyezii Mungu kwa kemikali za kujipaka kwa hiari,wamezifanya ngozi zao kupauka na kuzifanya nyeupe si nyeupe, nyekundu si nyekundu ilimradi tu ni vichekesho huku mishipa ya damu ikionekena bayana. Loh Mungu wangu tuhurumie.

  Kutokana na mikorogo, ngozi zao zimebadilika, ngozi ya kenge si kenge ni mabaka mabaka tu mwili mzima, tazama paji la uso jeupe,macho meusi mithili ya miwani ya jua, vifundo vya mikono na miguu vyeusi, ili mradi ni mikorogo tu ya rangi. Eti kisa ni mwenyezi Mungu kakosea kuwapa hao rangi nyeusi.

  Achana na ngozi, nywele nazo kazi ni moja tu, unamwangalia msichana au mvulana inakuwa kama ni kichekesho, nyani si nyani, komba si komba, mbega si mbega, basi ilimradi yupoyupo tu. Watu wanahangaika na maisha, kwao mwenyezi Mungu amekosea.

  Na ukiwaambia jamani mikorogo hii ina madhara kubwa kwa afya zao, hapo ndipo utapomjua mwanamke wa kibongo/mwanaume..."mwanga we, unanionea wivu we. Kama umefulia, tulia, na kwanza unikome kabisa" Watu hawa sasa hivi wamevuka mipaka na maadili.

  sasa hivi wanatafuta uzuri eti wafanane na malaika wa Mungu, wanatumia vidonge na sindano, na hata kemikali za kukuza matiti na makalio..'toba' walah, hivi tunakwenda wapi jamani?? Yale waliyojaliwa hawaridhiki nayo, Mi naona kama wanamtusi Muumba wao.

  Sasa maumbile yao yamewageuka na yanakuwa hayana tofauti na matairi ya nyuma ya trekta, yanakuwa ndembendembe, yanakuwa kama kinyago cha m-makonde uchwara.

  Sasa hembu sikiliza hii ya firauni, baadhi ya wanaume wa kibongo licha tu ya mavazi yao ya kuvalia nguo mapajani a.k.a kata K-almaarufu, wao sasa wapo wanataka kujibadili ili wawe kama wasichana kimuonekano na nina uhakika kwamba wakipata fursa watatamani kuwa wanadada kamili.

  Kuna wanakaka wengi licha ya nywele tu, wanapaka wanja na lipstick, na wengine kuchonga nyusi achilia mbali kubadili sauti na kutembea mithili ya kinyonga kama watoto wa kike.

  Ili kujulisha ukweli huu wamedhihirisha kwa kujiita "MASHAROBARO". Hii ni nomino maana yake halisi ni msichana MREMBO. Anajipenda na kujisikia huku akitafuta kwa hamu KUPENDWA KWA HALI NA MALI. Hawa ni masharobaro wa kiume na si wa kike. Bora wangejiita MABAROBARO, Hali kidogo ingekuwa shwari.

  Sasa cha kujiuliza uasi huu unatokana na nini?? Ee wabongo, ni ufinyu wa fahamu juu ya kile wanachokitenda ama?? Huu ni ulimbukeni wa kuiga hata visivyoigika, ni kasumba ya kuthamini vya wenzetu kuliko vyetu, ni ukosefu wa uzalendo, ni lack of confidence, ni utovu wa maadili na ushenzi uliopiliza.

  Hii sio kazi ya shetani , ni utashi wa matunda ya wabongo wenyewe kwa jinsi maisha yanavyotubadilikia. Ni ukosefu wa shukrani kwa Mungu dhidi ya uumbaji wake. Ni dhambi na ni kufuru ya wabongo. hatujui tulitendalo.

  WABONGO TUBADILIKE. wIKEND NJEMA!!
   
Loading...