Ndugu zangu,
Nimesoma juu ya Mabadiliko Makubwa kuhusiana na Mitihani ya Sekondari hapa nchini.
Kwamba mfumo umebadilishwa. Na kuwa kuanzia sasa hakutakuwa na division ziro. Naam, hakuna sifuri.
Habari hiyo imenikumbusha dada huyo pichani, anaitwa Mariam, ni muhudumu kwenye moja ya ofisi za mjini Dar es Salaam. Si kawaida kuwakuta Watanzania wakisoma vitabu. Na nilipomwona akiwa ameshika kitabu cha mwandishi Edwin Semzaba kiitwacho ' Marimba ya Majaliwa' ilibidi niongee nae kuhusiana na maudhui ya kitabu hicho ambacho mimi pia nimeshakisoma.
Kwa maneno yake mwenyewe, na si ya kuyasoma kitabuni, aliweza kutumia dakika kumi nzima kunisimulia yaliyo kitabuni. Mariam amemaliza Kidato Cha Nne na sikumwuliza alipata daraja gani. Yawezekana naye alitoka na sifuri.
Lakini, tukubali, mwanadamu hawezi kumaliza miaka minne shuleni halafu atoke na sifuri. Na kama ni hivyo, basi, ama alikuwa akiudhuria darasa lisilo na mwalimu au mwalimu wake alikuwa ni punguani.
Mimi kama Mwalimu pia, na kwa kumsikiliza Mariam akinisimulia yaliyomo kwenye kitabu alichosoma, na ningekuwa ni mwalimu wake wa fasihi, basi, isingewezekana kabisa Mariam atoke na sifuri shuleni.
Na akina Mariam wako wengi. Mifumo yetu ya elimu inawakatisha tamaa. Na laiti wangepimwa uwezo wao kwa namna nyingine, basi, wangefika mbali pia kielimu.
Nachukua fursa hii kuipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kuchukua hatua hii ya kubadilisha mfumo wa mitihani.
Ingawa changamoto inabaki kama ilivyoelezwa na Dk. Joyce Ndalichako, kuwa tuna ukosefu wa uadilifu miongoni mwa walimu. Kwamba wanadanganya pale wanapotoa ripoti za maendeleo ya mwanafunzi. Na kama asilimia 40 ya ufaulu itatokana na Continious Assesment ( CA) kwa maana ya maendeleo ya mwanafunzi. Basi, mkazo utiliwe kwenye uadilifu wa walimu.
Vinginevyo, kila mwanadamu ana uzoefu na maarifa anayoyakusanya tangu kuzaliwa. Kuna anayoyapata shuleni ( Episteme) na kuna yale ya maishani ( Fronesis).
Hivyo, hakuna anayekufa na sifuri.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa.
Iringa.