Neno kuu la leo: Upendo haugawanyiki kamwe wana jf! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno kuu la leo: Upendo haugawanyiki kamwe wana jf!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KIDUNDULIMA, Feb 27, 2011.

 1. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Wana JF nemeona ni vizuri tushilikiane neno kuu la leo ambalo linasema Upendo kati ya wapendanao haugawanyiki kamwe. Hii ni kutokana kwamba wivu ambao mwanaume unao ndio uleule alionao mwanamke. Mfano kama una mke na mke huyo anakwenda kufanya mambo yale ya kiutu uzima nje ya uhusiano wenu, wivu utakaokuwa nao ndio huohuo atakaoupata mwanamke pale mwanaume utakapoamua kuasi na kwenda nje ya ndoa au mahusiano yenu kuanzisha nyumba ndogo,ya kati na kubwa.

  Hivyo wana JF tusigawanye upendo maana haugawiki. Mwisho wake utauzidisha kwa mmoja na kuupunguza kwa mwingine na kuleta migongano katika nyumba na kukosa mwelekeo.

  Ni hayo tu kwa leo.
   
 2. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mie naona kichwa cha habari na paragraph ya pili vinajichanganyana,kitendo cha kukubali kwamba unaweza kuuzidisha au kuupunguza kwa mmoja wao,unathibitisha kwamba upendo unagawanyika.Ebu rudi tena uweke maelezo yako sawa kabla infidelities hawajaamka.
   
 3. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 775
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hakuna kujichanganya bali inadhihirisha kuwa huwezi kuwapenda watu wawili sawasawa bali kitakachotokea ni kuuondoa kwa mmoja na kuuhamishia kwa mwingine
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mi nafikiri unachanganya tamaa na upendo...huko nje wanaongozwa na tamaa na hawaendi kupenda au kugawanya upendo.....ila upendo utabaki kuwa kwa yule mmoja ambaye moyo umeridhia zaidi na si mwili na matamanio yake....:rain:
   
 5. J

  J Lee Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uko sawa kabisa mpendwa. Ila je wale wanafunga ndoa na wake zaid ya mmoja inakuaje?
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa Michelle hapa ndo watu wanapopotoka kwani wanashindwa kutofautisha kati ya tamaa na upendo!!!
   
 7. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nafikiri ni kukidhi haja za mwili na kutafuta satisfaction ya matamanio ya moyo.....ila nachelea kuamini kuwa kuna upendo unagawanywa....pale inatumika hekima,busara na uwajibikaji tu wa wanandoa wote ila yawezekana anapendwa mmoja .....
   
Loading...