NENO HILI 'MHESHIMIWA'

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,681
Niliichukia siku ile Bunge la Tanzania lilipopiga kura kwa wingi ya kuondoa neno 'ndugu' wawe wanaitwa 'waheshimiwa'!
Neno 'ndugu' lilikuwa linakufanya uhisi uko karibu zaidi kwa uhusiano na mwingine. Lilisaidia sana kuondoa tabaka katika jamii. Inapokuja kwa hawa watunga sheria wetu, kwa uchache liliwafanya wahisi kuwa binadamu kama wengine na kupunguza kiburi.
Neno hili 'ndugu' liko 'very disarming' (laondosha makali) kiasi polisi wetu walikuwa na aina ya ubinadamu walipokuwa wakiitwa hivyo.
Bado hadi sasa hakuna tafsiri iliyotolewa kwa raia, au binafsi sijaisikia, juu ya sababu ya kufuta neno hilo. Nahisi ni jitihada za kuondoa kabisa mabaki ya Ujamaa. Lakini, hata kama Ujamaa ulishindikana, si kila kitu ha Ujamaa kilikuwa kibaya.
Si hayo ninayotaka kuyajadili hapa. Najadili tatizo kubwa lililozushwa na neno hili 'mheshimiwa' kwa Watanzania hivi sasa.. Watanzania hivi sasa wanaamini kila mtu aliye serikalini ni wajibu aitwe 'mheshimiwa' na kwamba usipofanya hivyo unamkosea heshima au umefanya kosa la jinai vile...

La hasha! Hili ni neno ambalo limekusudiwa kutumika tu ndani ya Bunge, na baina ya Wabunge wenyewe, ili wakijadili hoja zao huko ndani wasidharauliane na kuitana majina mabaya. Sisi wa nje huku haituhusu chochote.

Ni kama Bunge la Uingereza wanavyoitana 'My Rt. Honourable friend. Huwezi kumsikia Mwingereza barabarani, au anapoandika gazetni akimwita Rishi Sunak, Honourable Sunak!

Ni aina nyingine ya ushamba na kuchelewa; kutukuzana kupita kiasi. Unaliita jitu 'Mheshimiwa' kesho linakuibia mamilioni, unafiki mtupu!
Tuachane na mambo haya ya kipuuzi.

Waandishi wa habari; maadili yetu yanakataza kabisa kuwa 'deferential' kwa yeyote. Naam, hata rais, wakati tukizungumza naye tumwite tu 'rais Samia'
Hii imewekwa kwa sababu maalum na muhimu sana (kwa wale waliosomea uandishi). Mtu unayemtukuza hivyo kupita kiasi utawezaje kumkosoa?

Tuwe na heshima za kawaida tu, Rais Samia, Mama Samia......Mbunge Msukuma, bwana Jamhuri...tosha. Si Mheshimiwa mtukufu.........

Hamuifanyii uadilifu hii tasnia ambayo kwa nchi nyingi duniani ndiyo iliyosababisha mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na kuheshimu haki za binadamu.
 
Wivu tu!
 
Umezungumza kitu cha kiuungwana sana;
 
Kiukweli wanaotakiwa kuitwa waheshimiwa ni wananchi maanake ndio waajiri wa hao wote wanaojifanya waheshimiwa na hao wanafaa waitwe tu Ndugu.
 
Back
Top Bottom