John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 113
- 222
Neno Amina linatofautisha matamko ya Yesu na wengine
Maandiko, katika kitabu cha Ufunuo 3:14, yanasema, kama ifuatavyo:
“Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye ‘ALIYE AMINA’, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu”.
Neno Amina maana yake ni “Na iwe hivyo”. Neno hili kwa lugha ya kiingereza ni “Amen”. Hivyo, po pote panapotajwa “Amina” au “Amen”, maana yake ni “na iwe hivyo”. Ni sawa na kusema “ni thabiti”, au “hakika” au hata kusema “confirmed”.
Kwa nini Yesu ajitambulishe kwa neno hilo?
Ni kuyatofautisha maneno yake na ya wengine. Kwamba maneno yake ni thabiti.
Ili ieleweke vizuri, turejee pale Yesu aliposema kuwa “Mimi ndimi Njia, na Kweli na Uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu mimi (Yohana 14:6)”.
Tukiuchambua huo mstari vizuri, tunapata sentensi mbili. Ya kwanza inayosema "Yeye ndiye Njia". Ya pili inayosema "Mtu haji kwa Baba ila kwa njia yake Yeye ".
Hapo Bwana anajiita kuwa Yeye “Njia”; anajifananisha yeye na kitu kisicho na uhai. Lakini anazidi kufafanua ni kwa jinsi gani yeye ni njia kwa kuendelea kusema “mtu hafiki kwa Baba isipokuwa kwa njia yake yeye”, ikiwa na maana kuwa, kwa maneno ya Yesu na maisha yake, tukiyafuata hayo, tutafika mbinguni (hayo, ndiyo njia). Njia zipo nyingi, lakini zote hizo hazimpeleki mtu mbinguni, isipokuwa njia ya Yesu tu, ambayo ni Neno lake.
Tukirejea hapo Bwana aliposema yeye ni “Amina”, utaona mbele kidogo anaendelea kufafanua ni kwa namna gani yeye ni “Amina”:
Ufunuo 3:14 “Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, SHAHIDI ALIYE MWAMINIFU NA WA KWELI, MWANZO WA KUUMBA KWA MUNGU”.
Anasema yeye ni Amina, Shahidi aliye mwaminifu, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.
Maana yake ni kuwa maneno yake ni hakika. Akisema amesema, ni lazima iwe hivyo. Amina yake ni Amina kweli. Wengine wanazo amina, lakini zinaweza zisitimie kama walivyosema. Lakini yeye Yesu maneno yake ni hakika. Akisema, ni lazima “ITAKUWA HIVYO KAMA ALIVYOSEMA”. Ndiyo maana anaitwa Shahidi mwaminifu. Hajawahi kusema jambo halafu lisitimie. Ni mwaminifu kwa maneno yake siku zote.
Hebu turejee kwenye vitabu vya Marko na 2Wakorintho:
Marko 13:31: “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe”.
2Wakorintho 1:20: “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi”.
Je umemtumainia huyu ambaye Maneno yake hayapiti? Alisema “Aaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16)”. Je unadhani kutakuwa na kanuni nyingine zaidi ya hiyo? Alisema wadhalimu, na wachawi, na wazinzi, na walevi hawataurithi ufalme wa mbinguni. Je unadhani Yesu anadanganya au anatania?
Ni kweli itakuwa hivyo. Maneno yake kamwe hayapiti. Amina yake ni Amina kweli.
Kwa hiyo, neno Amina maana yake ni NA IWE HIVYO. Hiyo ina maana kuwa iwe hivyo, ni thabit, na haibadiliki.
Yesu anajulikana kama Amina. Hivyo, lo lote asemalo ni thabit, halibadiliki, na litatimia.