Nembo ya taifa

kamkoda

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
396
71
Wadau tunajadli katiba mpya kipindi hii ila naomba kuwasilisha hoja ja kuona ile nembo ya taifa nayo kama inahitaji mjadala naona kama haiendani na karne hii, naomba kuwasilisha!:embarassed2:
 
Nembo hiyo ya taifa lipi la Zanzibar au Tanganyika?...Kama sisi Zanzibar tunayo nembo yetu na kma haujui pole sanaaaaaaaaaaaaaaa
 
Sasa wewe unataka tujadili nembo ya taifa ambalo limeuzwa?Au jamaa alivovaa gauni yeye na mke wake unaona kama kijima vile?kwa taarifa yake hata huko ulaya gauni ni vazi la heshima sana tena jamaa wanava na sketi kumbuka wakati fagason wa Man U alipokuwa anapewa U sir na malikia alitinga na sketi yake safi na baadaye kwenye hafla akavaa gauni la zambarau!!!But all in all hujakosea kualika mjadala wa kitu kama hicho
 
Mimi naona bado inafaa hata kwa karne zijazo. Labda kama tutavunja Muungano ni kuondoa hiyo karafuu hapo tu na kuweka kingine kama Kahawa ama Korosho.
 
Mimi naona bado inafaa hata kwa karne zijazo. Labda kama tutavunja Muungano ni kuondoa hiyo karafuu hapo tu na kuweka kingine kama Kahawa ama Korosho.


Hata karafuu unaiacha tu manake hata bara tunaweza kuilima
 
Back
Top Bottom