Neema ya ajira yazidi kuwafuata walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neema ya ajira yazidi kuwafuata walimu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Neema ya ajira yazidi kuwafuata walimu


  Na Benjamin Masese

  WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewapa matumaini ya ajira nyingine wanafunzi waliohitimu mafunzo ya ualimu mwaka 2009/2010 na kuachwa kutokana na sababu mbalimbali mbali ya wale 9,226 waliotangazwa na
  Waziri wa wizara hiyo, Dkt. Shukuru Kawambwa.

  Katika tangazo lilitolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Hamisi Dihenga liliwataka wanafunzi wote ambao wamefaulu na majina yao hayakuonekana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi kuandika barua kwa Katibu Mkuu na kuambatanishwa vyeti halali na taarifa ya matokeo ili zifanyiwe kazi.

  Hata hivyo alitoa onyo kwa waombaji na wahitimu kwamba wizara haifanyi mabadiliko yoyote kwa wale walimu waliopangiwa vituo vya kazi.

  Kutolewa kwa ajira hiyo kumetokana na wanafunzi waliohitimu mafunzo yao kuvamia wizara hiyo juzi wakitaka kuelezwa vigezo vilivyotumiwa na serikali kutoa ajira 9,226 huku wakiachwa wanafunzi walio na sifa.

  Hata hivyo wanafunzi hao jana waliendelea kufika hapo wizarani mbali ya viongozi juzi kuwaeleza kuwa suala lao linafanyiwa kazi

  Kwa mujibu wa maelezo ya wanafunzi hao walisema kuwa wameahidiwa kufanya mazunguzo na viongozi wa wizara hiyo leo ili kujua hatma ya ajira yao.

  Juzi Wanafunzi hao kutoka vyuo mbalimbali vikiwemo cha Mtwara, Marangu, Morogoro na vinginevyo walifika wizarani hapo na kuzua tafrani getini baada ya kuzuiwa na walinzi huku wakitaka kuonana na Waziri wa Elimu Dkt. Kawambwa kitendo kilichosabisha ulinzi kuimarishwa.

  Walisema kuwa tangu wahitimu masomo yao Mei mwaka jana wamekuwa wakipewa ahadi ya kuajiriwa na serikali lakini hadi leo ajira hakuna kilichofanyika zaidi ya hali ya sasa inayoanza kuonesha ubaguzi kwenye suala hilo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Our educational policy has always been a trade off of quality to placate quantity..............this is why we will always be in a jam.............
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Wizara ya Elimu yaomba walimu waliokosa ajira kuvuta subira
  Wednesday, 19 January 2011 21:40

  Gedius Rwiza
  WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imewataka walimu waliokosa ajira kuendelea kuwa na subira kabla ya Januari 24, watapewa taarifa na kwamba, hivi sasa wizara inaendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo lao kukosa ajira.

  Akizungumza na walimu hao jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, alisema tatizo hilo linaonekana kubwa hali ambayo inawafanya kuendelea kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo hilo.

  "Inaonekana tatizo hili ni kubwa, maana kuna walimu ambao wamefaulu na wamekosa ajira na wengine wamefeli masomo mawili lakini wamepewa ajira, kwa hiyo suala hili linahitaji tukae na wataalamu waweze kubaini chanzo kilichosababisha hali hiyo," alisema Mulugo.

  Mulugo alisema wizara yake inataka kutenda haki kwa kila mwalimu, ili anayestahili apate ajira na kwamba, hivi sasa kuna upungufu mkubwa wa walimu kwenye shule zote na kuongeza kuwa, hakuna mwalimu mwenye sifa atakayekosa ajira.

  "Wizara haina nia mbaya na walimu, ila tunataka haki itendeke kwa kila mmoja, maana inaonekana tatizo ni kubwa halihitaji kwenda haraka bila kufanya utafiti na kubaini chanzo cha tatizo, kwa hiyo kuanzia sasa wataalamu watakaa na kufanya uchambuzi kabla ya Januari 24 mtapewa majibu juu ya muafaka wa ajira zenu, nawaomba mvute subira," alisema Mulugo.

  Mulugo alisema kuna baadhi ya walimu wanaodaiwa kupangiwa vituo zaidi ya kimoja na kwamba, huenda hata idadi ambayo imetolewa kwa walimu walioajiriwa sio sawa.

  Baadhi ya walimu waliofika wizarani walisema wanasikitishwa na kitendo cha wenzao walioshindwa baadhi ya masomo, wameajiriwa lakini wao wameachwa.

  "Tunasikitika kuona wenzetu tena ambao wamefeli masomo zaidi ya mawili wameajiriwa, lakini sisi tumeachwa hali ambayo inatufanya tushindwe kuelewa vigezo walivyotumia kutoa ajira," alisema mmoja wa walimu waliokosa ambaye hakutaka kutajwa.

   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Walimu kujengewa nyumba 1,200

  Wednesday, 19 January 2011 21:43


  Fredy Azzah

  RAIS Jakaya Kikwete amezindua awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES-II), ambao pamoja na mambo mengine nyumba za walimu 1,200 ambapo kila nyumba itakuwa na sehemu ya kuishi walimu wawili na familia zao.

  Uzinduzi huo ulifanyika jijini hapa jana ambapo alikata utepe maalumu kuashiria kwake na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wahisani.

  Mambo mengine yatakayotekelezwa katika mpango huo kati ya mwaka 2011 mpaka 2015, ni ujenzi wa maabara kamili katika shule za sekondari za serikali, kuongeza idadi ya walimu wenye sifa, kuendelea kutoa ruzuku (capitation) ya Sh25, 000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi.

  "Malengo makubwa katika awamu hii ni kuboresha elimu tuliyonayo," alisema Rais Kikwete.
  Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, alisema Benki ya Dunia (WB) imekubali kutoa dola 150 milioni za Marekani, kwa ajili ya utekelezaji wa mpango huo na kuwa mpaka sasa dola 49 milioni zimeshatolewa.

  Mbali na WB, pia Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), imekubali kuchangia ili kufanikisha mpango huo wa miaka mitano.

  Dk Kawambwa, alifafanua kuwa WB imekubali kukarabati shule 500 ambazo tayari zimeshajengwa kwa nguvu za wananchi, kuchangia kuwapa walimu wapya motisha pamoja na kuchangia katika utoaji ruzuku kwa wanafunzi.

  "Baada ya miaka mitatu kuanzia sasa, ubora wa elimu unatakiwa uonekane kwenye majengo, walimu wa kutosha na wenye sifa pamoja na ufaulu mzuri na hasa katika masomo ya sayansi na hesabu," alisema Dk Kawambwa.

  Katika hotuba yake Rais Kikwete, mbali na kusisitiza kuwa mradi huo unatakiwa kuinua ubora wa elimu, pia alisema serikali itatia mkazo zaidi katika kuboresha elimu ya sayansi.

  "Wote sisi na fani zetu ni muhimu, lakini wanasayansi ni muhimu zaidi kwa kuwa ndio wanatakiwa kutusaidia kututoa hapa tulipo ili tuende sehemu nyingine, kwa hiyo tutaweka zaidi mkazo katika elimu ya sayansi," alisema Rais Kikwete.

  Pia alisisitiza kwamba, pamoja na wadau wa maendeleo nchini kukubali kusaidia mpango huo, pia serikikali itaendelea kuongeza fedha katika bajeti ya elimu kila mwaka.

  "Kuwekeza katika elimu ni lazima, siyo anasa, ndo maana tunasema kuwa tutaendelea kuongeza fedha katika bajeti ya elimu kwa sababu tunaelewa kwamba, gharama ya ujinga ni kubwa mno, kuliko kuwekeza sasa katika elimu," alisema Rais Kikwete.

  Alisisitiza kuwa, elimu ya sekondari ni muhimu kwa kuchochea maendeleo ya taifa lolote, huku akifafanua kwamba tabaka la uchumi hutengenezwa na watu wenye angalau elimu ya sekondari.

  "Elimu ya msingi ni msingi tu, mtu anapata, lakini tabaka la kati hujengwa na watu hawa wenye elimu ya sekondari, na tabaka hili ndio kichocheo cha maendeleo," alisema Rais Kikwete.

  Aliwataka pia wananchi kuendelea kuchangia katika elimu huku akieleza kuwa, watawapuuza na kuwaepuka watu wanaobeza mafanikio yaliyofikiwa katika elimu.

  Balozi wa Canada nchini, Robert Orr ambaye alikuwa akiziwakilisha nchi wahisani wa elimu katika uzinduzi huo, alisema nchi wahisani zitaendelea kuchangia katika kuboresha elimu nchini.

  Alieleza kuwa wanachotamani kuona ni Watanzania wote wakipata elimu bora ya sekondari.

  "Njia ya kufikia malengo hayo ni kuimarisha miundombinu ya kujifunzia, kusomesha walimu wengi walio bora, kuboresha mitaala na kuhakikisha vifaa vya kusomea vinapatikana," alisema Orr.

  Naye Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), alisema ofisi yake imejipanga kuhakikisha kuwa fedha zitakazotolewa zitafanya kazi zilizokusudiwa.

  Pamoja na mambo mengine, (MMES I) ilisaidia kuongeza shule za sekondari kutoka 828 mwaka 2004 mpaka kufikia shule 3,397 Juni 2010.

  Uandikishaji wa wanafunzi uliongezeka kutoka 264,888 mwaka 2004 mpaka kufikia wanafunzi zaidi ya wanafunzi 1.5 milioni.

  Pia kupitia mpango huo nyumba za walimu 4,152, madarasa 4,265, maabara 490 zilijengwa huku walimu 31,742 walisomeshwa.
   
Loading...