Karibu sana, Japo sina hakina sana na sababu zake eti aliwahi sana familia, wakati akipata mtoto wa kwanza alikua na 28 years (44 -16) na wa tatu akiwa na 41 years ambapo ni juzi juzi tu apo. Bado alikua amewahi? Labda kuna mengine, sijui! Tuyaache hayo.
Dada Shumbe tafuta muda wako mzuri wa kujitafakari mwenyewe, uangalie nini malengo yako, kwa nini unataka uolewe, kama uko tayari kuwalea watoto ambao sio wako ie watoto wa kambo (maana ukiwatesa watoto wa kambo, wa kwako mwenyewe huwa hawabaki salama hata kidogo), Japo sijui umri wako, lakini mnajiona mkizeeka pamoja na huyu? (Hahaaa, Usije ukawa mjane ukiwa bado kijana mbichi japo hatuombei hayo) wazazi wazazi wako wanalipokeaje n.k n.k.
Kuolewa kwa maana ya bahati hutokea kwa aina ya mume/mke uliempata kwamba mme -match sana karibia mambo yote. Ila kuolewa kwa maana ya kupata mke au mume sio bahati maana ndoa ni mpango wa Mungu watu waoane, kwa hiyo fikiria kwa makini sana juu ya uamuzi utakao uchukua. ''kupanga ni kuchagua'' Asante.