NECTA Kuweni makini na usimamizi wa mitihani wilayani Tarime

Supu ya kokoto

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
3,731
6,786
Baraza la mitihani NECTA ongezeni macho katika usimamizi wa mitihani ya darasa la Saba wilayani TARIME.
Kuna mbinu chafu zimebainika zitatumiwa na baadhi ya wamiliki wa shule za binafsi ili kufaulisha kwa kiwango kisicho Cha kawaida ili mwakani wapate wanafunzi wengi.
Baadhi ya shule hizo ziko maeneo yafuatayo

1. Tarime mjini
2. Sirari
3. Nyamwaga
4. Nyamongo
Kutoka chanzo changu Cha taarifa baadhi ya mbinu kuu zinazotumika ni hizo:
( a) kubadilishana karatasi kwenye vyumba vya mitihani.
(b) kuwapa rushwa wasimamizi waliopangwa kwenye vituo husika.
(c) kuonesha watoto majibu
(d) kupanga madawati kwa ukaribu kwa ajili ya wanafunzi kuibiana.
Na mbinu zingine nyingi.
Narudia tena shule hizo zimetenga vyumba maalum kwa baadhi ya walimu wanaoaminika kuokoa jahazi pindi inapohitajika.
Baraza la mitihani fanyeni ukaguzi kwenye mazingira mnayoweza kuyahisi kuwa maficho ya mamluki hao.

Niwatakie maandalizi mema kuelekea mitihani ya darasa la Saba

FAIR PLAY.
 
Huu ni wivu tu..acha watoto wafaulu pia watu wapate pesa..Maisha yenyewe ndo haya kuungaunga halafu unakuja kuwachoma humu JF.
 
Acha wivu ww hii tabia ipo level zote wewe mwenyewe kuna sehem ulifanya huo mchezo jifikirie kwanza ndiyo uhukumu
 
Sisi tulioko kwenye elimu tunaona elimu ishajifia hakuna la ziada ,kama hakutatikea mkombozi wa elimu akabadilisha mtaala hakuna la ziada.Sisi huku wengne tusolve mtihani mzima hata asiejua kusoma na kuandika ili mradi anaweza kushade anapata kingereza 40/50 maisha yanaendelea na hilo ni agizo toka juu kila mwanafunzi afaulu kwa means yoyote .Waache hao wafanye hata serikali inafanya
 

Ahaa kumbe ni sawa au sio....basi hamna haja ya kupeleka wasimamizi kutoka Baraza.
 
AGIZO KUTOKA JUU 🤔🤔🙄
I love you Tanzania.
 
Ni sawa lakini sio kuhalalisha WIZI WA MITIHANI kwa lengo la BIASHARA.
Kumbuka hii ni taarifa Kama zingine zinazohusu
Rushwa, wizi na uvunjifu wowote ule wa sheria ya nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…