NEC yatoa ratiba Uchaguzi Mdogo Ubunge Arumeru Mashariki na Udiwani Kata 18

Yote hii ni siasa ya Upepo unakoelekea kuna Diwani alivuta Hapo Arusha siku sio Nyingi, Kwani imekuwa na shida gani kwa kata yake Kutangazwa ipo wazi?? Au Wanafikiri atafufuka? Pia zile Kata Tano za Arusha ambazo Madiwani wamekosa sifa Arusha? Naona Yote poly tricks!!!
 
Natafuta uwezekano wa kugombea pale Arumeru mashariki kama Nassari ataamua kutogombea. Vinginevyo tumuunge mkono (Nassari) mwanaJF mwenzetu huyu
 
...hayaa hayaa tena wale wapenda ubwa ubwa wa bwerereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
sogeeni Arumeru...
 
Kama daftari halifanyiwa marekebisho vijana wapinge kwa court kudai haki
 
Sijaona kata yoyote ya mkoani Arusha, hata ile ya daraja mbili ambayo diwani wake alifariki (marehemu Msangi)

Zile nne za waasi wa chadema nafahamu wamefungua kesi mahakama kuu, je daraja mbili nako kuna nini hadi uchaguzi usiitishwe?
​Vipi uchaguzi kata ya Mwawaza shinyanga?
 
KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI NA CHAGUZI NDOGO ZA MADIWANI KATIKA KATA ZA HALMASHAURI MBALIMBALI NCHINI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, imepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye kuiarifu kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jeremiah Solomon Sumari, aliyefariki dunia tarehe 19 Januari, 2012. Baada ya Tume kupokea taarifa hiyo ya kuwepo nafasi wazi kwa Jimbo la Arumeru Mashariki, Tume imepanga kufanya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo hilo kwa mujibu wa sheria ili kujaza nafasi hiyo ya Ubunge iliyoachwa wazi.

Ratiba ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ni kama ifuatavyo:-

NA TUKIOTAREHE
1.Uteuzi wa Wagombea08 Machi, 2012
2.Kampeni za Uchaguzi09 Machi, 2012 hadi 31 Machi, 2012
3.Siku ya Upigaji Kura 01 Aprili, 2012

Aidha, Tume inapenda kuwataarifu wananchi kuwa itafanya Chaguzi Ndogo za Madiwani katika Kata nane (8) zilizoko katika Halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za Viti vya Madiwani ambazo zimetokana na vifo vya Madiwani husika.

Ratiba ya kufanyika kwa Chaguzi Ndogo hizo za Madiwani ni kama ifuatavyo:-

NA TUKIOTAREHE
1.Uteuzi wa Wagombea05 Machi, 2012
2.Kampeni za Uchaguzi06 Machi, 2012 hadi 31 Machi, 2012
3.Siku ya Upigaji Kura 01 Aprili, 2012

Kata zitakazohusika katika Uchaguzi huo na Halmashauri zake ni kama ifuatavyo:-

NAHALMASHAURI HUSIKAKATA ITAKAYOFANYA UCHAGUZI
1.TemekeVijibweni
2.BagamoyoKiwangwa
3.KirumbaMwanza
4.BariadiLogangabilili
5.DodomaChango’mbe
6.RungweKiwira
7.SongeaLizaboni
8.TangaMsambweni

Ifahamike kwamba, hakutakuwa na kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Chaguzi hizo. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ndilo litakalotumika katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki na Chaguzi zote Ndogo za Madiwani. Vituo vitakavyotumika kupiga kura ni vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.

Tume itaweka orodha ya Wapiga Kura katika Vituo vya Kupigia Kura kwa muda wa siku saba (7) kuanzia tarehe 25/03/2012 hadi 31/03/2012. Wananchi wote wa Jimbo la Arumeru Mashariki na Kata zote ambazo Chaguzi Ndogo zitafanyika mnaombwa kwenda katika vituo vyenu vya Kupiga Kura na kukagua majina yenu ili kujua Vituo mtakavyo pigia Kura.

Tume inapenda kuwasisitizia wananchi na Vyama vyote vya Siasa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia siku ya Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi, kukagua orodha ya Wapiga Kura wakati itakapobandikwa kwenye Vituo na kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura tarehe 01 Aprili 2012. Vituo vya Kupiga Kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 alasiri.

Tume inawakumbusha wananchi wote katika maeneo husika kutunza vizuri Kadi zao za kupiga kura na kuzitumia siku ya upigaji Kura. Aidha, ikumbukwe kwamba kama Mpiga Kura hutakuwa na kadi ya Kupiga Kura hutaruhusiwa kupiga kura. Hakikisha unatumia haki yako ya kikatiba kushiriki katika Uchaguzi na kuchagua viongozi unaowataka.


Damian Lubuva
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Jamani mbona jimbo la Arusha mjini hawakutangaza nafasi zilizo wazi? au wanakwepa nini? au ni mimi ambaye sijui tarehe ya uchaguzi wa madiwani waliofukuzwa Arusha?
Naomba kufahamishwa!!
 
Ifahamike kwamba, hakutakuwa na kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Chaguzi hizo. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ndilo litakalotumika katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki na Chaguzi zote Ndogo za Madiwani. Vituo vitakavyotumika kupiga kura ni vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.

Kosa kubwa sana.

Nakumbuka kwenye uchaguzi mdogo pale Igunga, vyama pinzani vililipigia kelele sana hili suala; na kusema kwamba haki na sheria zilivunjwa!!

Sasa kama mambo yanakuwa kama yalivyokuwa, napendekeza kwa vyama pinzani kuungana katika hili na kususia uchaguzi.
Haiwezekani raia wenye kustahili kupiga kura wasipewe haki yao.
Hakika nitavishangaa sana vyama pinzani kama vikienda tena kushiriki uchaguzi ambao yale walioyalalamikia kwenye uchaguzi uliopita hayajabadilika!

Susieni hizo chaguzi kama daftari halitaboreshwa.
 
Nafikiri kwa sababu kuna kesi mahakamani iliyofunguliwa na madiwani waliofukuzwa
 
Mgomo wa madaktari + posho za wabunge + uchaguzi mdogo = Kifo kwa wagonjwa. Msisahau mgonjwa nambari moja ni CCM.
 
Ivi arusha hasa daraja mbili kunani? That commcion is not yet independent,arusha mtawaua ila mwisho wenu 2015.najua kata 4 wale 'madem' waliapirl ila MNASUBIRI LABDA MSANGI AKATE RUFAA
 

Aidha, Tume inapenda kuwataarifu wananchi kuwa itafanya Chaguzi Ndogo za Madiwani katika Kata nane (8) zilizoko katika Halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za Viti vya Madiwani ambazo zimetokana na vifo vya Madiwani husika.


Damian Lubuva
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Vipi ule uchaguzi wa madiwani wa Arusha?
 
Hivi kwa nini kura ipigwe siku ya wajinga duniani? Ili hata kura zikiibiwa tuambiwe ni siku ya wajinga eti? Loh.........kweli mwenyekiti wa tume ni nouma. Fools day watu wanavote? Mamaaaaaa
 
Back
Top Bottom