NEC yatoa ratiba Uchaguzi Mdogo Ubunge Arumeru Mashariki na Udiwani Kata 18 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC yatoa ratiba Uchaguzi Mdogo Ubunge Arumeru Mashariki na Udiwani Kata 18

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mike Mushi, Feb 7, 2012.

 1. Mike Mushi

  Mike Mushi JF Founder

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 253
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  KUFANYIKA KWA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI NA CHAGUZI NDOGO ZA MADIWANI KATIKA KATA ZA HALMASHAURI MBALIMBALI NCHINI

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa, imepokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yenye kuiarifu kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jeremiah Solomon Sumari, aliyefariki dunia tarehe 19 Januari, 2012. Baada ya Tume kupokea taarifa hiyo ya kuwepo nafasi wazi kwa Jimbo la Arumeru Mashariki, Tume imepanga kufanya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo hilo kwa mujibu wa sheria ili kujaza nafasi hiyo ya Ubunge iliyoachwa wazi.

  Ratiba ya kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ni kama ifuatavyo:-

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]NA[/TD]
  [TD] TUKIO[/TD]
  [TD]TAREHE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1.[/TD]
  [TD]Uteuzi wa Wagombea[/TD]
  [TD]08 Machi, 2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2.[/TD]
  [TD]Kampeni za Uchaguzi[/TD]
  [TD]09 Machi, 2012 hadi 31 Machi, 2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3.[/TD]
  [TD]Siku ya Upigaji Kura[/TD]
  [TD] 01 Aprili, 2012[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Aidha, Tume inapenda kuwataarifu wananchi kuwa itafanya Chaguzi Ndogo za Madiwani katika Kata nane (8) zilizoko katika Halmashauri mbalimbali nchini kufuatia kuwepo wazi kwa nafasi za Viti vya Madiwani ambazo zimetokana na vifo vya Madiwani husika.

  Ratiba ya kufanyika kwa Chaguzi Ndogo hizo za Madiwani ni kama ifuatavyo:-

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]NA[/TD]
  [TD] TUKIO[/TD]
  [TD]TAREHE[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1.[/TD]
  [TD]Uteuzi wa Wagombea[/TD]
  [TD]05 Machi, 2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2.[/TD]
  [TD]Kampeni za Uchaguzi[/TD]
  [TD]06 Machi, 2012 hadi 31 Machi, 2012[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3.[/TD]
  [TD]Siku ya Upigaji Kura[/TD]
  [TD] 01 Aprili, 2012[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kata zitakazohusika katika Uchaguzi huo na Halmashauri zake ni kama ifuatavyo:-

  [TABLE]
  [TR]
  [TD]NA[/TD]
  [TD]HALMASHAURI HUSIKA[/TD]
  [TD]KATA ITAKAYOFANYA UCHAGUZI[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]1.[/TD]
  [TD]Temeke[/TD]
  [TD]Vijibweni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]2.[/TD]
  [TD]Bagamoyo[/TD]
  [TD]Kiwangwa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]3.[/TD]
  [TD]Kirumba[/TD]
  [TD]Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]4.[/TD]
  [TD]Bariadi[/TD]
  [TD]Logangabilili[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]5.[/TD]
  [TD]Dodoma[/TD]
  [TD]Chango’mbe[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]6.[/TD]
  [TD]Rungwe[/TD]
  [TD]Kiwira[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]7.[/TD]
  [TD]Songea[/TD]
  [TD]Lizaboni[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]8.[/TD]
  [TD]Tanga[/TD]
  [TD]Msambweni[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Ifahamike kwamba, hakutakuwa na kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Chaguzi hizo. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita ndilo litakalotumika katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki na Chaguzi zote Ndogo za Madiwani. Vituo vitakavyotumika kupiga kura ni vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2010.

  Tume itaweka orodha ya Wapiga Kura katika Vituo vya Kupigia Kura kwa muda wa siku saba (7) kuanzia tarehe 25/03/2012 hadi 31/03/2012. Wananchi wote wa Jimbo la Arumeru Mashariki na Kata zote ambazo Chaguzi Ndogo zitafanyika mnaombwa kwenda katika vituo vyenu vya Kupiga Kura na kukagua majina yenu ili kujua Vituo mtakavyo pigia Kura.

  Tume inapenda kuwasisitizia wananchi na Vyama vyote vya Siasa kuzingatia na kufuata ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi kuanzia siku ya Uteuzi wa Wagombea, Kampeni za Uchaguzi, kukagua orodha ya Wapiga Kura wakati itakapobandikwa kwenye Vituo na kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura tarehe 01 Aprili 2012. Vituo vya Kupiga Kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 alasiri.

  Tume inawakumbusha wananchi wote katika maeneo husika kutunza vizuri Kadi zao za kupiga kura na kuzitumia siku ya upigaji Kura. Aidha, ikumbukwe kwamba kama Mpiga Kura hutakuwa na kadi ya Kupiga Kura hutaruhusiwa kupiga kura. Hakikisha unatumia haki yako ya kikatiba kushiriki katika Uchaguzi na kuchagua viongozi unaowataka.


  Damian Lubuva
  MWENYEKITI
  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
   
 2. d

  dotto JF-Expert Member

  #2
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kipimo cha bosi mpya wa nec
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Feb 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  CDM haya sasa mmepata nafasi za bure kabisa
   
 4. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #4
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  kipindi cha kuteketeza mabilion kimewadia
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Sijaona kata yoyote ya mkoani Arusha, hata ile ya daraja mbili ambayo diwani wake alifariki (marehemu Msangi)

  Zile nne za waasi wa chadema nafahamu wamefungua kesi mahakama kuu, je daraja mbili nako kuna nini hadi uchaguzi usiitishwe?
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  HIVI WANA nec HAWAONA KUNA MGOMO WA MADAKTARI???utatuumbua wana ccm,
   
 7. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  wakati wa kusahau shida umefika
   
 8. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #8
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Peoplesssssssssssssssssssssssssssssss
   
 9. G

  GINHU Member

  #9
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa na hatua ya Tume ya uchaguzi kwa kukataa kufanya review ya dafutari la wapiga kura.
  1. ikumbukwe kuwa kuna vijana wengi sana ambao wana qualification za kuwa wapiga kura ambapo 2010 hawakuwa nazo. so kwa kutoreview daftari hilo kutawnyima haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.
  2. pia kuna watu wengi wamefariki dunia, ama kupoteza uwezo wa kupiga kura kutokana na matatizo mbalimbali, hivyo kuathiri pia takwimu halisi za daftari hilo.

  Ni vyema NEC wakaliangalia suala hili kwa mtazamo mpana zaidi. kwani wanahofia nn kureview daftari hilo? Hawana hela au vp?

  Asanteni wanaJf, naomba kuwasilisha.
   
 10. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #10
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ngojea nirudi arumeru muda wa pesa za bure umefika
   
 11. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 7, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Godless Lema na Mwita Waitara waleeeeee, Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye wale paleeeeee!Duh,sipati picha hali itakavyokuwa kule Arumeru Mashariki,ni full kivumbi.
   
 12. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #12
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ndio hapo sasa inabidi serikali ya chama chenu iwalipe madaktari haraka. Haiwezi kuingilia akilini mnakuwa mabilioni ya kuwahonga wapiga kura halafu mnashindwa kutatua matatizo yanayo wakabili madaktari. Lakini pia ni wakati mzuri kwa wananchi kutofanya makosa tena ya kuichagua CCM!
   
 13. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #13
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  CDM, huu ni muda wa kuwasha taa ya kijani kuonyesha 2015 yenu.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Si matakwa yao bali wanatekeleza sheria. Kama yangekuwa ni mapenzi yao huenda uchaguzi usingeitishwa mapema kiasi hiki.
   
 15. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mbona siku waliyoichagua ya Uchaguzi ni Sikukuu ya Wajinga! Au wanatudanganya? CCM bana!
   
 16. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Vp kata za Arusha Mjini au mpaka 2015?
   
 17. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  muda wa kufungia wanaume gesti na kuwanunulia vipaja vya kuku unawadia,
   
 18. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hiyo Ratiba ni ya kweli au ndiyo Judge Damiani Lubavu ameamua kuazimisha siku ya wajinga mapema?!

  Siku ya kupiga kura 01/04/2012, Siku ya wajinga duniani! wananchi wa maeneo hayo open your eyes
  mnaweza kufika vituoni, msikute kitu, lakini kesho yake mkatangaziwa wagombea wa CCM wameshinda
  Wajinga ndiyo waliwao. Hapa Lubuva anataka kutuchezea karata tatu kekundi na keusi!
   
 19. R

  RUTARE Senior Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ni nani aliwaambia nec kwamba lazima uchaguzi ufanyike jumapili? Huyu mwenyekiti mpya naye amekuja kuendeleza yale yale ya makame hivi nyie nec hamsikii hoja za watu kwa maneno matupu mpaka watu waingie mabarabarani?
   
 20. l

  loiluda Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizo fedha za kufanyia uchaguzi zitapatikana wapi,wakati serikali yalia haina fedha?mgomo wa madaktari unaoendelea ni matokeo hayohayo ya serikali kutokuwa na fedha tuambieni hzo zitatoka wapi?ni kweli uchaguzi ni muhimu sana lakini si kama ilivyo maisha ya watu.
   
Loading...