NEC yapinga waraka wa Jaji Bomani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC yapinga waraka wa Jaji Bomani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Injinia, Mar 18, 2010.

 1. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimekuta hii habari kwenye gazeti la Mwananchi. Habari yenyewe ni ndefu kidogo hivyo nimefupisha na kusisitiza mambo muhimu.  Hivi kwa nini NEC/ CCM wanatabia ya kupuuza maoni yoyote ambayo yanaitakia mema nchi? Huyu mzee ni wa kusikilizwa kwani na yeye aliwahi kuwa sehemu ya serikali na ana uzoefu wa muda mrefu.


  Angeongeza pia na sababu ya kutokuongeza majimbo kuwa hii: hakuna pesa za kulipa mishahara ya mamilioni ya hao wabunge wa ziada!  UGAWAJI WA MAJIMBO NI SUALA LA KIKATIBA


  James Magai na Hussein Kauli  TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesisitiza kuwa itaendelea kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi kwa kuwa hilo ni suala la kikatiba.  Kauli hiyo ya NEC inapinga maoani ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani aliyoitoa katika waraka wake kwenda kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake akielezea udhaifu katika nfumo wa sasa wa uchaguzi kwamba unachagia kuwepo kwa vitendo vya rushwa.  Ndani ya waraka huo, pamoja na kuelezea faida na athari za mfumo wa uchaguzi ambao ni mfumo wa majimbo pia alipinga hatua ya serikali ya kuongeza idadi ya majimbo kwa kutumia kigezo cha idadi ya watu katika majimbo husika.
  Akizungumza na Mwananchi jijini jana baada ya mkutano kati yake na viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya mkoa jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisisitiza “Katiba inatutaka kila baada ya miaka 10 kuangalia mipaka ya majimbo na kuona kama kuna mahitaji ya kuongeza idadi ya majimbo au la. Tunavyo vigezo 13 ambavyo tunaviangalia kabla ya kuongeza majimbo, kama majimbo yatakizi vigezo hivyo, basi tutaongeza kulingana na maombi yaliyowasilishwa kwetu.”
  Alisema moja ya vigezo hivyo, ni ukumbi wa Bunge kuweza kuhimili idadi husika ya wabunge.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu wa Bunge), Philip Marmo aliwahi kutoa tahadhari kuhusu shinikizo la kuongezwa majimbo kwa madai kwamba nafasi katika ukumbi wa bunge mjini Dodoma zimejaa.
  Jaji Bomani alisisitiza hakuna ulazima wowote wa kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi kila kukicha kwa kisingizio cha kuongezeka kwa idadi ya watu na kueleza kuwa miaka ya nyuma wilaya nzima ilikuwa na jimbo moja tu la uchaguzi na uwakilishi ulikuwa wa kuridhisha.


  "Marekani yenye wakazi 300 milioni ina wabunge (House of Representatives) 435, na wastani wa wakazi ni zaidi ya 700,000 kila mbunge. Uwakilishi mzuri si wingi wa wawakilishi.
  Kuhusu mfumo mzima wa uchaguzi wa sasa ambao ni wa majimbo alisema una faida kwa wapiga kura kwa kuwa wanapata nafasi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka, lakini pia akasema mfumo huo hutumia gharama kubwa na kuchochea rushwa na ufisadi kwa jumla.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Aghhhh wananichefua tu
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Of course lazima waupinge maana siku hizi waraka zinaandikwa kila upande sasa wataegemea upande gani.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kugawa majimbo wanatumia vigezo 13, ina maana mpaka vyote hivyo kuvikidhi ndio jimbo/majimbo hugawanywa, sasa hapo ni mpaka Bunge lijae ndio wataacha kuongeza majimbo, ama likijaa watataka kujenga ukumbi mpya. KWELI MASIKINI HUTUMIA ZAIDI YA TAJIRI.
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Alichosema Bomani ni sawa kabisa. matatizo ya watanzania ni yale yale yanahitaji utatuzi ule ule. Hatuhitaji kuongeza majimbo. Alichokisema Bomani pia kiliandikwa siku nyingi na Msomi anaitwa Walter Rodney How europe under developed africa.

  Sababu moja ndio Hii ya kuwa big industry kwenye nchi zetu ni Administration( Bunge , Jeshi ,etc.)


  But so far Nec haina makosa . JK aliangalie hili kama alivyoangalia matumizi ya uchaguzi
   
 6. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Haiwezekani watu wawe wanakwepa wajibu wao kwa kufikiri JK ataingilia kila kitu, kwa hili ndugu yangu MTAZAMAJI NEC wanawajibika kufikiri ulazima wa kuongeza hayo majimbo, ni kwa faida ya nani? haya tuseme wataongeza hayo majimbo ili kujaza viti poale dodoma, vikishajaa na baada ya miaka kumi watanyaje? hawatongeza majimbo sababu viti vimejaa dodoma? mbona sikumbuki kama mwaka 2000 waliongeza majimbo? Hii yote ni mbinu ya CCM ili kuokoa baadhi ya mawaziri na wabunge wake wanaobanwa mbavu sasa!
   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndahani tatizo si kuegemea upande iangaliwe mantiki ya huo waraka haijalishi umeandikwa na nani hata wewe ukiandika waraka wenye kuleta tija utaangaliwa chukulia hii ya kuongeza majimbo kuna wabunge wengine wanachaguliwa kwa kura 500 huko Visiwani wengine 250,000 kama Ukonga sasa mantiki iko wapi na wabunge hao utakuta wanalipwa mishahara sawa haijalishi unatumikia wananchi wangapi huo ni mfano mmoja tu kuna mifano mingi ya bunge kuwa mzigo kwa taifa bila msingi
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  "Tanzania zaidi ya uijuavyo"
  Kwa kweli huwa nalaumu sana mganga aliyeturoga halafu immediately akafa... pengine huwa nahisi alijiua. Siasa...siasa...siasa...bla...bla...bla. Kila kukicha new drama...
  Haya tusonge tu...
   
 9. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hii tume isifanyekazi kama robot mradi imepewa vigezo 13 tu basi ndiyo iwe excuse mfano nafasi bungeni zimebaki 16 majimbo yaliyotimiza vigezo vyote ni 47 ina maana wataongeza majimbo kwa excuse ya kufuata sheria hapa lazima busara itumike kama wameambiwa nafasi kwenye ukumbi finyu watalazimisha? au wabunge wengine watasimama au waende na viti vyao kama wanafunzi wa shule za kata

  kwa mfano wanasema sheria ni kuangalia mgawanyo wa majimbo kila baada ya miaka 10 ina maana mwaka 2020 kama idadi ya watu itaongezeka kwenye majimbo say 50 na yametimiza vigezo vyote 13 wakati ukumbi umejaa watafanyaje ndiyo maana nasema wasifanye kazi kama robot lililosetiwa hata likikuta ukuta haliwezi kukata kona hadi lisetiwe upya
   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mpwa nami nadhania hivyo hivyo yani hujakoseeea,

  Me siwaelewi hawa viongozi wa NEC/CCM na serikali yake nikuwa hawana wataalamu wakujua wapi twatoka na wapi twaenda ni kwamba vision zao ni zero? hawa viongozi si watu kabisa sijui ni waaina gani na ndio maana hata kile kitabu cha Mwl.JK hakipatikani, hii inamaanisha kuwa hawa viongozi hawapendi kukosolewa wala kuambiwa hapa sipo na hapa ndipo.
   
 11. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama kugawa majimbo kuna maslahi binafisi kwa viongozi wa NEC, piga, ua yataongezwa kama hakuna hoja ya Judge Bomani inaweza kuzingatiwa. Mambo mengi hapa nchini yanakwenda kwa personal motives. Ni kama swala la mgombea binafsi. Upinzani juu ya jambo hili ni selfish through and through!!
   
 12. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Uchumi wa nchi yetu ni hoi sana kwasababu matumizi yetu ni mara mbili ya mapato yetu; thamani ya sarafu yetu inazidi kushuka siku hadi siku na mfumuko wa bei ya vitu vyetu uko kwenye double digits toka single digit aliyoiacha Mkapa!! Hizi sababu ni vigezo tosha kuwa hali ya wananchi wa Tanzania ni mbaya na uamuzi wowote utakaoongeza matumizi ya serikali lazima utaongeza machungu ya maisha ya wadanganyika !! Jaji Bomani ni mmoja kati ya wazalendo waliobaki wanaoipenda nchi yao na wasio na woga wala uchu wa madaraka, waraka alioundika kuhusu busara ya kutoongeza majimbo ya uchaguzi ni katika kufikilia uwezo wa uchumi wetu kuhimili ongezeko la matumizi linaloendana na kuongezeka kwa idadi ya wabunge bila kuongeza tija!! Kuongeza idadi ya majimbo ya uchaguzi hakumletei mwananchi maisha bora bali maisha duni kwani hizo pesa zitakazotumika kuwalipa stahili hao wabunge wa ziada zitatokana na ongezeko la tozo za kodi na sio hivyo tu hizo pesa watakazolipwa zingeweza kutumiwa kuimalisha shule na zahanati kwenye kata huko vijijini. Kuongeza idadi ya majimbo kwa utashi wa kisiasa wakati huu ni sawa na kuwaweka KIBRA watanzania!! Mawazo ya jaji Bomani ni ya busara lazima yapewe uzito yanayostahili.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Sijausoma huo waraka kwahiyo siwezi kusema sana nini kimo ndani yake. Lakini inawezekana nao ni ukweli mtupu ambao wana siasa wengi hawataki kuusikia.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  tutasema yoooote lakini hitimisho ni kwamba mchawi wa tanzania ni CCM.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unajua wakati mwingine wanakuwa kama hawajui hata hesabu za seti!
   
 16. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yaani badala ya kukurupuka wangemuomba Mzee Bomani wakutane kwa faragha na kupata maoni yake.

  Tanzania si kisiwa. Mi nshaanza kuingia na wasiwasi tunakoelekea. Mambo yanayoendelea Uganda sasa hivi si kwamba hayawezekani Tanzania.

  Watu sasa hivi wako ukingoni, wanahitaji kitu kidogo tu kiwasukume off the edge of the cliff halafu mambo yaharibike. Nchi inakatwa na kuliwa vipande kama keki?
   
 17. A

  August JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  halafu huyo jaji makungu anatakiwa kuelewa kwamba katiba sio msahafu kwamba hauwezi kubadilishwa ili kukizi haja za kiuchumi na za wakati huo?
   
 18. m

  miner Member

  #18
  Mar 18, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JKaangalie nini wakati NEC ni chombo cha serekali yake na ameagiza ndani ya chama chake lazima wanawake wawe 50 kwa 50 Nec lazima aongeze majimbo ili wakubwa watusifie tatizo la msingi hapa ni KATIBA ni jukumu letu Watanzania kusema hapana tunahitji Katiba itakayokidhi matakwa na uwezo wetu kama nchi na si watakavyo watawala ndio maana hata mawazo mema yanapuuzwa. Nec yenyewe ni tatizo, matakwa na vigezo pekee havitoshi kama hautaangalia uwezo wa nchi kujiendesha
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Sioni ishu hapa, wananchi wanaongezeka na majimbo lazima yaongezeke hili linaeleweka na dunia nzima, tatizo ni maviongozi magoi goi tunaowachagua kutoka haya majimbo na ni sisi wananchi, ni lini tutachagua viongozi wanaotufaa kwenye taifa, I mean mbunge ashindwe jimbo basi awe bora kwenye taifa basi!

  - Yaaani mtu huna macho, sasa hata akili nazo huna! Damn!

  Respect.


  FMEs!
   
 20. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  :confused:
  Wewe nawe Bwana!
   
Loading...