NEC wanajitekenya wenyewe na Polisi

NEC wanajitekenya wenyewe na Polisi

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,400
Hivi ni sheria inayowataka watu kukaa mita 100 au ni tume ndio inawataka watu wakae mita 100 na kama ni sheria tume au police wanatoa wapi mamlaka ya kuwakataza watu walioamua kusimama kwa amani ili kuangalia kila kinachotokea hatua yoyote ya kuwaondoa watu waliosimama mita mia moja kwa amani kinyume na sheria inavyotaka ni kuipoteza amani yetu na hili tume na police ICC itawahusu baada ya uchaguzi hatuko tayari kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi kama mnavyotaka nec na police
 
Wametumwa na ccm hao. Huoni kinana kakurupuka sasa anahamasisha watu kutokaa mita mia kulinda kura zao
 
Tokea lini mwizi akafurahia mwenye mali kuweka ulinzi mkali katika mali yake?..Sisi wapumbavu,malofa na mbumbumbu tutapiga kura zetu kwa mpumbavu na lofa mwenzetu Edward Ngoyai Lowassa na kisha tutakaa mita 200 kulinda kura zetu.ONYO:Mwizi yeyote atashughulikiwa!
 
vyama vyote vilisaini mbele ya tume ukipiga kura hustahili kukaa mita mia miatano ni kuondoka eneo husika kwani vyama vyote vina mawakala kwenye vituo vya kupiga kura
 
Hivi ni sheria inayowataka watu kukaa mita 100 au ni tume ndio inawataka watu wakae mita 100 na kama ni sheria tume au police wanatoa wapi mamlaka ya kuwakataza watu walioamua kusimama kwa amani ili kuangalia kila kinachotokea hatua yoyote ya kuwaondoa watu waliosimama mita mia moja kwa amani kinyume na sheria inavyotaka ni kuipoteza amani yetu na hili tume na police ICC itawahusu baada ya uchaguzi hatuko tayari kwenda kinyume na sheria ya uchaguzi kama mnavyotaka nec na police

Hapo penye mita 100 utakaposimama na kukusanyika ni kiwanja au eneo la baba yako au mama yako? kama
Ni eneo la watu ambalo wewe si mmiliki wala halimilikiwi na chama chako Kwenda kukaa eneo la mtu ni uvunjaji wa sheria.Polisi kuzuia mikusanyiko lengo ni kuzuia viashiria vyote vya uvunjaji sheria ikiwemo kwenda kujikusanya eneo la mtu bila ridhaa yake.

Ole wako mita mia hiyo uje kukusanyika eneo langu patachimbika.Nitawapiga nondo za vichwani liwalo na liwe vibaka wakubwa nyie.

Wewe ulinde kura hao mawakala wenu wa vyama walioko ndani ya chumba cha kupiga kura wanafanya kazi gani? Kama hamuwaamini shauri yenu.Lakini kukusanyika mita mia natoa onyo mapema.Msije kusanyika kwenye eneo langu.Na watu kibao wameshapeleka onyo kwa tume na polisi kuwa wahakikishe hao watu hawakusanyiki maeneo yao.

Nakuonya hizo mita 100 zaweza sababisha ukavunjwa miguu na polisi kama wenye eneo wataamua kuwapigia polisi waje wawaondoe eneo lao.Ukikusanyika eneo ukaona polisi wanakuja na mabomu ujue wenye maeneo yao wamewaambia polisi kuwa eneo lao limevamiwa na watu kinyume cha sheria.
 
vyama vyote vilisaini mbele ya tume ukipiga kura hustahili kukaa mita mia miatano ni kuondoka eneo husika kwani vyama vyote vina mawakala kwenye vituo vya kupiga kura

Soma hata kacertificate ka sheria katakusaidia.
Ni hivi; mkataba baina ya mtu na mtu au taasisi na taasisi hauwezi kupingana na sheria iliyowekwa kihalali.
Suala la kukaa mita mia moja ni suala la kisheria si makubariano hayo kaka vipi wewe!!!?
 
Hapo penye mita 100 utakaposimama na kukusanyika ni kiwanja au eneo la baba yako au mama yako? kama
Ni eneo la watu ambalo wewe si mmiliki wala halimilikiwi na chama chako Kwenda kukaa eneo la mtu ni uvunjaji wa sheria.Polisi kuzuia mikusanyiko lengo ni kuzuia viashiria vyote vya uvunjaji sheria ikiwemo kwenda kujikusanya eneo la mtu bila ridhaa yake.

Ole wako mita mia hiyo uje kukusanyika eneo langu patachimbika.Nitawapiga nondo za vichwani liwalo na liwe vibaka wakubwa nyie.

Wewe ulinde kura hao mawakala wenu wa vyama walioko ndani ya chumba cha kupiga kura wanafanya kazi gani? Kama hamuwaamini shauri yenu.Lakini kukusanyika mita mia natoa onyo mapema.Msije kusanyika kwenye eneo langu.Na watu kibao wameshapeleka onyo kwa tume na polisi kuwa wahakikishe hao watu hawakusanyiki maeneo yao.

Nakuonya hizo mita 100 zaweza sababisha ukavunjwa miguu na polisi kama wenye eneo wataamua kuwapigia polisi waje wawaondoe eneo lao.Ukikusanyika eneo ukaona polisi wanakuja na mabomu ujue wenye maeneo yao wamewaambia polisi kuwa eneo lao limevamiwa na watu kinyume cha sheria.

Ungetumia akili tu usingeandika ngonjera kama hizi
 
vyama vyote vilisaini mbele ya tume ukipiga kura hustahili kukaa mita mia miatano ni kuondoka eneo husika kwani vyama vyote vina mawakala kwenye vituo vya kupiga kura

Hapo we unazungumzia makubaliano binafsi ambayo hayako kisheria sisi tunazungumzia mita 100 ambazo ziko kisheria na kwa nini wazivunje hilo bao la mkono hatutakubali
 
Hivi Tanzania Kuna polisi wangapi ili waweze kukaa kila kituo ili wavunje sheria inayowataka watu kukaa mita Mia?
 
Hapo penye mita 100 utakaposimama na kukusanyika ni kiwanja au eneo la baba yako au mama yako? kama
Ni eneo la watu ambalo wewe si mmiliki wala halimilikiwi na chama chako Kwenda kukaa eneo la mtu ni uvunjaji wa sheria.Polisi kuzuia mikusanyiko lengo ni kuzuia viashiria vyote vya uvunjaji sheria ikiwemo kwenda kujikusanya eneo la mtu bila ridhaa yake.

Ole wako mita mia hiyo uje kukusanyika eneo langu patachimbika.Nitawapiga nondo za vichwani liwalo na liwe vibaka wakubwa nyie.

Wewe ulinde kura hao mawakala wenu wa vyama walioko ndani ya chumba cha kupiga kura wanafanya kazi gani? Kama hamuwaamini shauri yenu.Lakini kukusanyika mita mia natoa onyo mapema.Msije kusanyika kwenye eneo langu.Na watu kibao wameshapeleka onyo kwa tume na polisi kuwa wahakikishe hao watu hawakusanyiki maeneo yao.

Nakuonya hizo mita 100 zaweza sababisha ukavunjwa miguu na polisi kama wenye eneo wataamua kuwapigia polisi waje wawaondoe eneo lao.Ukikusanyika eneo ukaona polisi wanakuja na mabomu ujue wenye maeneo yao wamewaambia polisi kuwa eneo lao limevamiwa na watu kinyume cha sheria.
Nyumba yenyewe ya kupanga eneo utalitoa wapi? Hatoki mtu, tunafuata sheria ya Uchagui ukipiga kura unaruhusiwa kukaa mita 100.NEC haohao walisema matokeo yatabandikwa baada ya kura kuhesabiwa ili kuondoa wasiwasi miongoni mwa wapiga kura nani atayaona ikiwa watu wataamuliwa kurudi nyumbani? Mawakala wapo ndiyo lakini lengo la kubandika nini? Maana mawakala tayari wanamatokeo tayari.
 
Makamanda, kuna wizi wa vituo Hewa huo pia tunapaswa kutafta namna ya kuuzuia.

Lazima tuhakikishe sisi na mawakala wetu tunajua idadi kamili ya vituo halisi kwa kila kata na kijiji na kitongoji. Ili kuzuia kura za vituo hewa kupelekwa halimashauri kwa mkurugenzi.

Hivo tarehe 24 tuhakiki vituo halisi kwa idadi yake nakuwapa mawakala idadi halisi na namba za vituo halisi.
 
Huu nao ni ujinga ukae mita 100 sasa useme nalinda? Wana siasa hapo wanataka kutushindisha kwenye jua na sisi hapo na sisi tuwambie waje tushinde nao ndoo tutaamini tuko nao Kulinda.sio wajifiche
 
Nyumba yenyewe ya kupanga eneo utalitoa wapi? Hatoki mtu, tunafuata sheria ya Uchagui ukipiga kura unaruhusiwa kukaa mita 100.NEC haohao walisema matokeo yatabandikwa baada ya kura kuhesabiwa ili kuondoa wasiwasi miongoni mwa wapiga kura nani atayaona ikiwa watu wataamuliwa kurudi nyumbani? Mawakala wapo ndiyo lakini lengo la kubandika nini? Maana mawakala tayari wanamatokeo tayari.

Kwa sheria ya uchaguzi mlinzi wa kura ni wakala wa mgombea.Mlinzi wa eneo la kura ni jeshi la polisi.Sasa hako kajeshi kapya ka walinda kura kako kwenye sheria ipi ya nchi hadi karuhusiwe kukusanyika mahali kulinda kura?
 
Kama sheria ipo ya kukaa umbali wa mita 100, kwanini usitake watu wasisimame katika hizo mita 100? Una shida gani na watu kusimama hapo? Kwani umelazimishwa uende wewe kusimama? Waache wanaotaka kukesha hapo wakeshe, shida yako nini...au mna lenu jambo?
 
Huu nao ni ujinga ukae mita 100 sasa useme nalinda? Wana siasa hapo wanataka kutushindisha kwenye jua na sisi hapo na sisi tuwambie waje tushinde nao ndoo tutaamini tuko nao Kulinda.sio wajifiche

Mita 100 hata huoni kinachoendelea kule ndani!! Unawezaje kulinda usichokiona?

Mlinzi ni wakala wa chama husika.Kama chama hakimwamini tatizo sio wapiga kura wao wamepiga wamemaliza kilichobaki ni mgombea mwenyewe na wakala wake aliyemuweka ambaye wala hajachaguliwa na tume.

Kama hawaamini mawakala wao waseme.Na ni tatizo lao wasijaribu kusukumia wapiga kura eti wakeshe.Kwa nini mawakala wako wasikeshe ufanye kazi ya kukeshesha wapiga kura?

Wapiga kura tuelevuke.
 
Watanzania tutakaa mita 100 kama sheria inavyoelekeza kuhakikisha na hili kushuhudia kila kinachoendelea kwenye kituo chetu cha kupigia kura!
Na hatayetuzuia tutakabiliana nae hivyo aje na silaha za moto
 
Wana siasa walisha tuona sisi ni wapumbafu.mita 100 wengine tutapita nyumba zetu . halafu wengi wetu hatujui mita 100 ni umbalia kiasi gani. Kama mawakala wakiamua kufanya biashara wewe uliyo mita 100 huwezi kujua kinacho endelea kule ndani ni mbali sana
 
Katika karata amboyo ccm waliyobaki nayo ni hii, Mim nimeshawela alama, mita mia zangu kutoka chumba kura zinaishia kwenye ukuta wa bar, so sitatoka hapo mpaka kielewe
 
Back
Top Bottom