Mhoja
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 207
- 24
Napenda kuishauri Time ya Uchaguzi iwatumie Viongozi wa Dini katika kusimamia zoezi la uchaguzi siku ya Jumapili. Kwa haya malumbano yanayoendelea ya kukaa mita 200 kutoka kwenye kituo au kwenda nyumbani baada ya kupiga kura yanaweza yakaisha.
Naamini kila eneo lina Viongozi wa Dini kama vile Shehe, Imam, Ustadhi, Padre, Mchungaji, Katekista, Mwinjilisti, Nabii au Mtume. Uwepo wa Viongozi hawa utawafanya wapiga kura wawe na Imani na usalama wa kura zao.
Si vema tukasubiri mambo yaharibike ndiyo tukawatumia Viongozi wa Dini kupatanisha au kuombea amani irejee tena. Muda bado unatosha kuwaomba Viongozi wa Dini waweze kusaidia, maana wapiga kura wengi naona hawana imani na Mawakala.
Mungu ibariki Tanzania!!!!!