Kamundu mngoko
JF-Expert Member
- Jun 10, 2015
- 231
- 23
Katika hali isiyo ya kawaida NEC imetoa taarifa zinazokinzana kuhusu mita 200 ndani ya siku mbili mfululizo yani jana na leo.
Katika taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku jana tarehe 18, Oktoba Jaji Damiani Lubuva alitoa ufafanuzi kuwa wakati wa muda wa upigaji kura kumalizika wananchi wataweza kusubiri matokeo yao umbali wa mita 200, lakini hawataruhusiwa kusubiri matokeo hayo kabla ya muda wa wa upigaji kura kumalizika.
Leo tarehe19, Oktoba kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili usiku kamishna wa NEC akiongea kutoka Mtwara amesema baada ya kupiga Kura watu waende kwao, je tuamini kauli ya nani katika tume, kama tume imeshachanganyikiwa hata kabla ya uchaguzi, tunaiomba mahakama itoe tafsiri ya sheria husika, kwa sababu jambo hili lisiposhugulikiwa lina kila dalili ya kuleta machafuko ikiwa polisi watakubali kutumika ovyo na Serikali.