Maoni tofauti Rais Samia akiteua Vigogo wapya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Uteuzi wa viongozi watano wakiwemo wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) uliofanywa jana na Rais Samia Suluhu Hassan, umewaibua wadau mbalimbali wa kia-siasa baadhi wakipongeza na wengine wakidai hauna tija kwa kuwa wamerudishwa watu walewale.

Jana Rais Samia alimteua Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Mbarouk Salim Mbarouk kuwa makamu mwenyekiti wa NEC kwa kwa kipindi cha pili. Vilevile, katika uteuzi huo alimteua tena Balozi Omary Ramadhan Mapuri kuwa mjumbe wa tume hiyo kwa kipindi cha pili huku akimteua Dk Zakia Mohamed Abubakar kuwa mjumbe wa Tume hiyo.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, uteuzi wa wajumbe hao unaanza kesho Julai mosi. Pamoia na hao pia alimteua aliyekuwa Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Benjamin Magai kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Pia Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali
(TGFA), Profesa Idrissa Mshoro naye aliteuliwa kwa kipindi cha pili.

Wapongeza, wakosoa
Baada ya uteuzi huo, wadau mbalimbali walitoa maoni tofauti baadhi wakipongeza na wengine wakidai hauna tija kwa kuwarudisha watu walewale waliokuwa wajumbe wa Tume ilivonyooshewa kidole kwa namn a ilivyoendesha uchaguzi uliopita.

Hata hivyo, Profesa Mohammed Makame Haji wa Zanzibar alisema anaamini watu walioteuliwa wanaweza kufanya kazi inayotakiwa kwa kutenda haki kwa kuzingatia misingi ya kisheria muda wote.
"Jaji Mbarouk ni mzoefu amekuwa akisimamia shughuli za kisheria kwa muda mrefu na amekuwa akipanda ngazi kwa hatua, tangu alipoanza hadi kuwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, hii imethibitisha uwezo aliokuwa nao," alisema.

Alimwelezea Balozi Mapuri kuwa ni mtu mwenye uzoefu wa kutosha hasa mabadiliko historia na mwelewa katika ugha wa kidiplomasia, akiwa ametumikia nafasi nyingi za kisiasa kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara.

"Kwa nafasi yake katika Tume anaweza kuwa na mchango mkubwa katika kusimamia kwa kuwa amebobea katika maeneo hayo, alisema. Kuhusu Dk Zakia, Profesa Haji alisema naye ni mtu aliyetumikia nafasi mbalimbali na mara mwisho alikuwa makamu mkuu wa Chuo Kikuu Zan-zibar, na kwa kuwa nafasi hiyo inahitaji watu wenye maono, inamfaa kuwatumikia Watanzania.

"Uwepo wao utasaidia kwa kuwa wote hao wana uwezo wa kusoma mabadiliko ya jamii inayohusi-ka lakini ni watu wanaojua mabadiliko mbalimbali ya siasa zetu kwa kuzingatia mahitaji yetu,"alisema Profesa Haji.

Wakati msomi huyo akisema hivyo, Mkurugenzi Mtendaii wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Bob Wangwe alikuwa na mtazamo tofauti akisema uteuzi huo unamsikitisha kwa kuwa umewarudisha watendaji walewale ambao katika uchaguzi mkuu uliopita walikuwa wananyoshewa kidole kwa kuuharibu.

"Hali hivo inaonyesha Rais alifurahia kilichotokea katika uchaguzi uliopita, binafsi nilikuwa nategemea yafanyike mabadiliko makubwa ya watendaji kwa kuingiza wapya ili kurejesha nidhamu na weledi na kuwaaminisha Watanzania kuhusu mwenendo wa uchaguzi ujao," alisema Wangwe. Hi ni mara ya pili mjadala wa kisiasa kama huo kuibuka kuhusu uteuzi wa ama watendaji au wajumbe wa NEC, baada ya kufanywa na Rais Samia.

Februari 26, 2023 Rais Samia alimteua Ramadhan Kailima kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, akichukua nafasi ya Dk Wilson Mahera aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Tamisemi. Kabla ya Dk Mahera, nafasi hivo iliwahi kushikwa na Dk Athumani Kihamia ambaye alichukua wadhifa huo Julai 2018 kutoka kwa Kailima aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu.

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa kauli yake kwenye kampeni 2020 alisema kwa hali yoyote ni lazima ccm ishinde.

Hali yoyote tuliiona ilivyofanya kazi.

Na sasa ni maandalizi kwa hali yoyote ccm ishinde 2025. Hayo ndio maandalizi.

Tanzania ya watu milioni 60 haina watu wengine zaidi ya hao ambao wametumika zaidi ya miaka 30.
 
Ni lini wasomi vijana katika taifa hili wataamunika na kukasimiwa madaraka? Je serikali yetu ina succession plan?

Sent using Jamii Forums mobile app
Yani huyo Omary Mapuri tangu nipo shule ya msingi ni kiongozi, nimesoma O level & A level pamoja na chuo kikuu sasa nina watoto jamaa bado anateuliwa tu.

Halafu hao ndio wanasema kila siku vijana mkajiajiri WTF?
 
Yani huyo Omary Mapuri tangu nipo shule ya msingi ni kiongozi, nimesoma O level & A level pamoja na chuo kikuu sasa nina watoto jamaa bado anateuliwa tu. Halafu hao ndio wanasema kila siku vijana mkajiajiri WTF?
Pamoja na kwamba uzee ni dawa lakini uzee sio antibiotic dawa ambazo ni mult purpose! Hawa kina Mapuri ni panadol tu kwasasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kauli yake kwenye kampeni 2020 alisema kwa hali yoyote ni lazima ccm ishinde.
Hali yoyote tuliiona ilivyofanya kazi...
Muongo, hakusema hivyo. Alisema hata chama kile kikishinda, CCM ndio itakayo tangazwa mshindi. Huyo mama anajifanya mtu wa mungu kumbe ni zuga tu

Ata ile kauli yake kuhusu Tundu Lissu kuwa hai baada ya le shambulizi ni za tata sana
 
Hoja kubwa ya wakosoaji ni jinsi tume hii hii ikiwa na watendaji hawa ilivyoharibu uchaguzi wa 2020. Tukiwa tunaelekea 2024 kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na 2025 kwenye uchaguzi mkuu kuwarudisha walewale walioharibu inaweza ikaleta tafsiri ya matayarisho ya uporaji wa uchaguzi tena.

Sidhani kama unaweza kuleta mabadiliko Kwa kutumia njia Ile ile iliyoharibu, inaonyesha dhamira ya uongozi wa CCM kutokuwa tayari kuleta uchaguzi huru
 
Back
Top Bottom