NEC: Hatujakiuka sheria kuruhusu wapigakura kutumia leseni, kitambulisho cha Taifa na Pasipoti

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Leseni za udereva, Hati za Kusafiria na Vitambulisho vya Taifa vitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Kata 43, utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu.


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima amesema wapiga kura wataruhusiwa kutumia vitambulisho hivyo kwa sharti ya kwamba picha, herufi na majina yaliyopo kwenye Leseni ya Udereva, Hati ya kusafiria na Kitambulisho cha Taifa yawe yanafana na majina na herufi zilizopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Kailima amesema ruhusa hiyo ya Tume ya matumizi ya vitambulisho hivyo imekuja kufuatia baadhi ya wapiga Kura kupoteza kadi zao za kupigia Kura na wengine kadi zao kuharibika kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuwanyima haki na fursa ya kupiga Kura katika uchaguzi huo.

Amesema hatua hiyo inazingatia matakwa ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu Namba 61, kifungu kidogo cha 3a na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kifungu Namba 62 (a) ambavyo vinaipa Tume mamlaka ya kuruhusu kutumika kwa utambulisho mwingine wowote utakao msaidia mpiga kura aliyejiandikisha kuweza kupiga kura iwapo hana kadi.
 
Mbona kaeleza vizuri na vifungu juu...
bado watu watataka kuleta manenomaneno.

kuna sababu nyingi kwa nini Tanzania ni maskini aisee.
 
Mi nachojua kuna watu kibao wamepoteza kadi wakulima, wafugaji n.k kama wana sifa na walijiandikisha ni wakati wao wakapige Kura uamuzi wa busara sanaaaaaaaa
 
Ngoja kwanza tuambiwe tumetumia vyote kwa mtu mmoja kuoiga kura na kadi zangu zote
 
Ataenda na kitambulisho chake, leseni, au hati ya kusafiria kituo cha kupiga kura ambapo patakua na orodha ya majina ya wapiga kura. Majina ya kwenye leseni na hati ya kusafiria yakifanana na kwenye hiyo orodha ikiwa ni pamoja na picha, basi ataruhusiwa kupiga kura
Sitoshangaa ikatokea idadi kubwa ya waliopotelewa na vitambulisho dhidi ya wenye hivyo vitambulisho vya mpiga kura
 
Sitoshangaa ikatokea idadi kubwa ya waliopotelewa na vitambulisho dhidi ya wenye hivyo vitambulisho vya mpiga kura
Lakini watahitajika kuwa na leseni au hati ya kusafiria.

Najua hofu iko wapi na hilo wala haliwezi kupingika.

Mimi nilikua naona ungefanyika mchakato wa kupiga kura kwa ku punch kwa dole gumba kama tufanyavyo huku maofisini. Ingesaidia sana juu ya hiyo hofu uliyonayo
 
Back
Top Bottom