NEAR DEATH EXPERIENCE: ( Hali inayompata Binadamu anapokaribia Kufariki Dunia)

Education Mentor

JF-Expert Member
Oct 26, 2016
392
1,000
NEAR DEATH EXPERIENCE: ( Hali inayompata Binadamu anapokaribia Kufariki Dunia)

Near Death experience ni scientific topic ijapokuwa ina maudhui ya kiimani

Ni muda kidogo umepita tangia nilipokutana na tukio hili limeacha alama ambayo siwezi kusahau sina lengo la kutisha mtu lakini kusudi langu ni kukupa kitu ukaelewa ni kwa jinsi gani muhimu sana kama kijana kutengeneza mahusiano yako na Mungu kuwa mazuri wakati wote yaani wakati wa furaha na shida na aina mbalimbali za maisha na changamoto tunazopitia. Kitaaluma mimi ni Mwanasaikolojia nna shahada ya kwanza.

Labda nianze kutafsiri msamiati near death experience ni nini? Ni ni hali au uzoefu unampata mtu anapokaribia kuuacha mwili au mauti.

Huwa napenda sana na ni sehemu ya maisha yangu kumsikiliza sana mhubiri mmoja hapa nchini kuna siku moja nilikuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo kutokana na nyakati nilizokuwa napita sababu tofauti na wanasaikolojia wengine mimi binafsi nimejikita katika kuamini uwepo wa Mungu kuwa ni yupo. Na huwa clients wangu mara nyingi “cure word” natumia mistari nadharia za Psychodynamic na classical conditioning pamoja na vitabu vya neno la Mungu na huwa inafanya kazi kama healing word.

Lakini zama hizi yalinikuta magumu sana na nilielemewa nikafikiria hata kuachana na career au taaluma pamoja na Mungu kilichokuwa kichwani pangu “Kumtumikia Mungu hakuna Faida”

Sababu nilitazama wale ambao waliendesha maisha yao nje na Mungu halafu nikajiangalia na mimi nikapanga kuachana na Mungu na kuachana na Saikolojia kwa kuchana cheti changu cha shahada sababu niliona haina faida.

Sasa siku moja wakati namsikiliza Mhubiri huyo alitumia mstari Malaki 3:14

14 Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? 15 Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. 16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. 17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. 18 Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.

Hii mistari ilinikaa sana niliyowekea weusi. Nakumbuka nikapata hadi msukumo wa kutoa sadaka kwa ajili ya somo lile.

Muda ukaenda sana baada ya hapo nikasahau kabisa nikaamua nianze maisha upya lakini sikukichana cheti na hata ukaribu sana na Mungu ukapungua na na Taaluma nikawa nimeipiga chini kabisa.

Nakumbuka kuna siku moja nikawa naumwa na nilichukulia easy sana na ni kawaida nikaenda maabala nikapimwa nikaonekana na maralia kama watanzania wengi kila mtu anafahamu malaria ni dawa gani atatumia mara baada ya kuumwa.

Lakini haikuwa kawaida kichwa kilikuwa kinaniuma saana na hakitaki kuachia ikabidi nirudi maabala ile nikachomwa sindano za diclopa kutuliza maumivu wakati dawa za malaria zinaendelea kufanya kazi. Kwa wakati huo kikapoa sana lakini kikarudi baadae kwa kuzidi. Ikabidi niende hospitali za Serikali kufanya check up nyingine hakukuwa na kipya wakawa wamechukua vipimo vyote wakakuta clear. Nkarudi nyumbani tena usiku huo kufika saa 9 usiku nkashtuka sababu jioni ile nilipatwa na unafuu nikala kidogo lakini muda huo naamka sikuwa naumwa kichwa tena wakati huu nikawa natapika sana tangia saa 9 usiku hule hadi kufikia saa tatu asubuh sikulala tena hivyo nikaishiwa nguvu sababu hamna kilichokuwa kinapita si Maji wala Chakula. Ikabidi ndugu zangu na Mother wanipeleke Hospitali tena nilivyofika nikalazwa tena kwa masaa kadhaa wakachukua vipimo wakaamua kunipa Transfer kwenda Hospital ya Sinza.

Wakati huo kuna kitu nilikuwa sijagundua yaani sababu ni kipya sikufahamu nilidhani ni sababu ya uchovu wa akili na kushindwa kulala tangia saa tisa usiku sababu kitaaluma ni mwanasaikolojia nikatafsiri kitaaluma tu ni hali ya uchovu wa akili tu unanipata. Nilikuwa naona vitu ambavyo si rahisi kuviona yaani kama maluweluwe tu.


NEAR DEATH EXPERIENCE INANIPATA

Sasa wakati nipo nahamishiwa sinza ndipo kuna vitu ambavyo vilinifunza sana na kunipa uzoefu kuhusu near death experience au mtu anapokaribia kufa au mwili kujitenga na roho anapatwa na hali gani?

1. Miguu kuishiwa nguvu na kushindwa kutembea inakamatwa na Ganzi (Mf. Mwangalie Kuku na wanyama walioumwa hadi kufa miguu huwa haifanyi kazi tena) hii pia ni hadi kwa Wanadamu tu. Na kuanza kupatwa na ubardi

2. Ganzi huwa inaanza kutembea mwili mzima na unaisikia kabisa

3. Sehemu za mwili zinaanza kupatwa na ubaridi mkali kila sehemu

4. Viungo vya mwili hasa mikono huwa inafanya involuntary movement yaani vinaanza kunyooka hasa hiki jirani na kidole gumba

5. Kuanza kuona giza yaani mfano wa kufumba macho wakati macho yako yapo wazi

6. Kukata Kauli wengi wanasemaga mwanadamu anapokaribia kufa hufikia hawezi kuongea tena ila nachokikumbuka ganzi ilikuwa katika mdomo hasa ulimi kwahiyo hunapoteza uwezo wa kutamka kabisa

7. Taarifa inayofika wakati huo (si ya woga au kusema ni uwoga) unafahamu kabisa sasa ndio ninakufa hakuna kinajojificha kabisa.

8. Sehemu inayobakia yenye joto ni kifuani tu (huwa najiuliza sana ktk saikolojia niliwahi soma siku za nyuma nafsi ya mtu inaishi katika ubongo wa mbele) lakini to that moment kifuani ndio palikuwa pana struggle sana huku ganzi ikipambana kufikia hapo lakini katika logic ya kawaida sababu ya moyo hupo hapo ukipatwa na ganzi inamaana shughuli zote za mwili zinasimama rasmi

9. Namna mwili unapokuwa unapambana kutafuta joto ndipo kuna movement flani huwa inaufanya ambao watu waliofariki wanajikuta miili yao inakaa kwa namna flani au kama kukakamaa. (mfano mmoja Angalia wanaokufa maji)

10. Kufika point hiyo ulimwengu wa kuota unaamia katika uhalisia unakuwa ni kama unayeota katika fikra lakini hupo hai unaona kabisa na fikra yako inafanya mrejesho kwa haraka haraka kuhusu maisha yako hadi hapo ulipofikia halafu unajiuliza ulikamirisha wito wako? Au nini umefanya muhimu kwa muda wako wote ulioishi duniani (Wito) Tafsiri nyepesi hakuna mwanadamu anayezaliwa bure hapa au yupo yupo tu. Kila mwanadamu anakazi maalum anaifanya awe Mwanajeshi, Mwalimu, Nesi, Daktari, kufanya biashara Fundi au taaluma yoyote ukiacha tu zile za uchungaji, upadri ua za dini nk ambazo wengi udhani ndio za kumtumikia Mungu.

11. Nakumbuka nimewekwa katika kitanda vya wagonjwa na akilini nishajua nini kipo mbele yangu na nikawa nishaikubali hali ile kwa wakati huo kwahiyo nilikuwa tiyari nimetulia tu nawaangalia Mother yangu na Grandmother wangu wakati huo walivyokuwa wame panic sana na hawajui wanafanya nini unaona akili zao zimehama kabisa

12. Nikapelekwa emergency room nikaonana na daktari mmoja aliponiona wakati huo movement ya kifuani nahema kwa nguvu sana kifuani akamtoa mother nje sababu alikuwa analia sana akawa ananiuliza maswali na mimi nikawa namjibu kwa chini pembeni alibakia mdogo wangu wakiume sababu mpaka wakati huo yeye ndie aliebakia jasiri.Na nikawa namuona daktari akilisogeza pazia la kijani karibu kama nilivyoeleza mwanzoni kitaaluma ni mwanasaikolojia kuna namna ya kumuelewa mtu kwa kumuangalia usoni ukaelewa kitu “Psychology of facial expression” ijapokuwa inahukumu sana hivyo ni method sipendagi kuitumia. Daktari alijua ninakufa muda ule kwa namna tafsiri nilioipata usoni pake.

NILIPONA VIPI?

Baada ya haya yote pengine kila anayesoma uzoefu niliopitia anepata kufahamu nilipona vipi na namna gani niliweza kupona. Nadhani ndio dhamira kubwa ilionisukuma kuandika hili wakati hatua hizo 12 zinanikuta nakumbuka sababu kila roho inatoka kwa Mungu niliuliza hivi nakufa hapa nakwenda wapi? Ndio swali hilo nikaona palepale eneo la hospitali chini pakiwa panafunuka kitu kama shimo ni peusi sana. Halafu saa hiyo nikasikia katika fikra zangu an mawazo Natakiwa niwepo bado duniani wakati ulikuwa bado kuondoka. Option to remain ktka Mwili (kuishi) au Leave body and go to hell forever. Jinsi nlivyotoka siku hiyo ilirudi siku ile ambayo nilitoa sadaka baada ya mhubiri Yule kufundisha kuhusu hipo siku

Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati ya yeye amtumikiaye Mungu na yeye asiyemtumikia.NIMEJIFUNZA MENGI SANA KATIKA SIKU ILE

Ukiwa una utaratibu wa kutoa Sadaka Kwa Mungu katika Kanisa au watu wenye mahitaji maalum hipo siku sadaka yako itasema kitu kwa niaba yako mbele za Mungu sababu siku hii tu ndio ilifunguka katika muda ule na si siku nyingine nilizokuwa nasikilizaga mahubiri

Mungu huwa hawatupi wanao mcha yeye hata wanapopita katika mazingira magumu sana ya kimaisha huwa haimaaniishi kawatupa au kuwaacha kaza Moyo tu hipo siku utabainisha kati wachaji na wale wasio wachaji. Sababu kama nisingekuwa na mcha siku ile ukweli nisingepona kabisa na nilishajua hilo.

Sasa ni namna tofauti Mungu anaweza kukupitisha ukafahamu tofauti ya wachaji na wasio mcha sio lazima hiwe kama njia niliopitia mimi

Kifupi ilinichukua muda sana kupona ugonjwa ambao hadi leo sikuufahamu kabisa ijapokwa madaktari waliniambia ni “Blood infection” lakini ukweli nilipona pasipo kumeza dawa yoyote baada ya kufahamu wapi shida ilipoanzia.

Ahsante nawasilisha japokuwa yapo mengine mengi tu ambayo siwezi yaweka wazi sana kwa sababu binafsi ambayo niliyapitia siku hiyo.
 

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
19,867
2,000
Huu ujumbe ni Mzuri sana, unatukumbusha kuwa, kuwa na uhusiano mzuri na Mungu na kutenda mema ni jambo zuri na la muhimu sana.

Kikubwa Binadamu anapaswa ajiulize : Je akishakufa na kuzikwa atakwenda wapi?
 

immu bin masoud

Senior Member
Jun 4, 2017
162
250
Hauwez kujua mtu akikarbia kufa anajskiaje, b'coz wanaojoa hio habar niwameshakufa. Hilo niwenge lamalaria tuu
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
30,323
2,000
Story yako inaelimisha na kuonya sana..
Nawaonya na kujionya mimi kua tusiwapite watu wenye uhitaji eg Wagonjwa, ombaomba, wazee, wafungwa n.k Tuwape msaada kivyovyote vile tulivyo jaaliwa.

Pia tupendane sisi kwa sisi na kumpenda MUNGU MUUMBA WETU
NA HIYO NDIO DINI YA KWELI..

Amen Mungu atuongoze tufike Paradiso salama wotee viumbe wake.

Ameeeen.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
25,102
2,000
Hiyo ni vile wengi tunachukulia kifo kinavyotakiwa kua.

Vipi wanaolipuliwa kwa mabomu, ganzi hua wanaisikia wapi? Anayeliwa na chui?

Je anayejiua atakua na near death experience kama ya mgonjwa wa pumu?
 

dagii

JF-Expert Member
Dec 23, 2013
3,921
2,000
Nimesoma nimepata kitu nimegundua sadaka ni ibada tosha wapendwa hasa kwa wahitaji sio kwa walee wazee wa hammer
 

Avatar

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
11,023
2,000
duuh nimeisoma kwa adabu kubwa sana hii thread ikiniacha nikitafakari mengi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom