Ndugu zetu hawa hawajaiona Christmass.Mungu ibariki Tanzania

jsenyinah

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
249
339
Heri ya Xmass ndugu zangu.

Ndo tunatoka ibadani, misa ya kwanza! Baadae nikasema nizunguke zunguke mtaani kuona kuna nini, hali ikoje na shamrashamra za sikukuu zimekaeje!

Nikapita kijiji cha Chekereni Wilayani Moshi Vijijini,njia kuu ya Moshi - Dsm.

Cha ajabu,na tofauti na miaka mingine, nimeshuhudia nyomi ya watu wakiwa mashambani wakimwagilia, kupalilia na kupiga dawa vitunguu vyao na mazao mengine. Ni siku ya kawaida kabisa kama siku zingine.

Watu hawajaenda makanisani, hawako majumbani mwao kusherekea sikukuu ya kuzaliwa mwokozi wao Yesu Kristo. Wapo busy majarubani wakiendelea na shughuli zao kama kawaida,licha ya kwamba karibu wote n wakristo.

Dah
 
Maisha yalivyo magumu lazima ujiongeze maana Sikukuu haina ladha kama huna Pesa.
 
Kwa hiyo huna jibu?

Kama.hujui basi unachoshelehekea hukijui
 
Back
Top Bottom