Ndugu zangu wananitenga

Ndugu zangu wananitenga

Pole mkuu, kuliko huyo mtoto kukaa nyumbani, mpeleke hata hizi shule za serikali maana elimu siku hizi ni bureee...
Hili limekua tatizo
Mtu anamuacha mtoto akae nyumbani eti kwa vile hana ada.
Na aibu ya kumpeleka shule ya serikali.
Wapeni watoto haki zao jamani
 
hiyo ni fursa itumie, ingawa sijabaini sawa sawa jinsia yako but whatever unatakiwa uamke utafute, hao unaowalalamikia sio wazazi wako.
 
Duh

Huyu mtu sio mzima to begin with!

Kuzaa wazao wao,kulea walee wengine on their behalf?

Does not make sense whatsoever!
 
Pole
Ukijua kuzaa jua na kelea pia!! Fanya kazi kwa juhudi vibarua ni vingi msomeshe mtoto
 
Tumezaliwa watatu wa kwanza ni wa kiume, wa pili mimi na watatu ni wa kike hawa wawili wananitenga na kunibagua hawanithamini wala kunijali kananiita hopeless huyu kaka yetu hana kazi na mimi sina kazi.

Huyu kaka yetu anasomeshewa watoto wake wote watatu, mimi ninaye mmoja, kwa sasa yuko nyumbani kisa sina ada niliona msaada kwa mdogo wangu ananijibu kirahisi kuwa ana madeni mengi ya kuyalipia najisikia vibaya kutengwa na ndugu zangu ila naamini Mungu hajanitenga.
Huyo mtoto hana baba au wewe ndio baba? ivi kweli ndugu zako ni jukumu lao kukusomeshea mwanao? sijui kama unajua tatizo unalo wewe sio ndugu, fanya kazi hata za ndani lea mtoto wako mkuu huu mda unao lalamika humu JF ufanyie kazi mwisho hata hela ya data utakosa ..
 
Kwanini ulilazimisha kupata watoto ukijua hali yako ya maisha bado hairidhishi? Au ulishinikizwa?
 
Tumezaliwa watatu wa kwanza ni wa kiume, wa pili mimi na watatu ni wa kike hawa wawili wananitenga na kunibagua hawanithamini wala kunijali kananiita hopeless huyu kaka yetu hana kazi na mimi sina kazi.

Huyu kaka yetu anasomeshewa watoto wake wote watatu, mimi ninaye mmoja, kwa sasa yuko nyumbani kisa sina ada niliona msaada kwa mdogo wangu ananijibu kirahisi kuwa ana madeni mengi ya kuyalipia najisikia vibaya kutengwa na ndugu zangu ila naamini Mungu hajanitenga.
Ww ni jinsia gani? Km ni mwanaume, mwanamke uliezaa nae yuko wapi umuoe muanzishe maisha kuliko kukaa nyumbani kutegemea ndg wakusaidie?

Ww ni mlemavu?
 
Huo ujumbe kwenye Avatar yako unakufanya Ubweteke, badirisha haraka sana nasisitiza badirisha for your own good!!
 
yaani watoto wako akusomeshee mtu mwingine.
 
Huyu ndugu naona ameshajitenga yeye mwenyewe tu. ukimsoma unamwona hayupo ok mentally kama kuna uwezekano hata huyo mtoto wake aliye naye ni bora kumchukua maana jamaa kiakili hayupo ok. kisandu alianza hivi hivi watu tukaonya mkatudharau sasa mnaona hali yake????????????
 
Deogratius Kisandu ni mtume wa kanisa la Nabii Tito
 
Back
Top Bottom