Nilibahatika kuishi mkoani Kagera miaka ya themanini,kwa wahaya kuna ndoa zile za lazima yaani kijana anamwinda dada mahali halafu anamkamata akiwa na vijana wenzie, kisha anampeleka kwake,yule dada akishalala kwa usiku mmoja tu nyumbani kwa kijana kwa jadi ya kihaya huyu tayari ni mkewe. sasa kwa vile nilikuwa mtoto sikuwahi kuuliza haya maswali yangu,naomba wahaya mnisaidie
1. je na mdada alikuwa akijua kuwa anakaribia kubebwa?
2. nini maana yake maana wengi wao walikuwa ndani ya maandalizi ya kuwaoa haohao lakini ghafla anakatisha anambeba mdada hii sikuwa naelewa kabisa maana yake.
3. je ndoa hizi zilikuwa zinadumu?
4. je hii jadi ipo mpaka leo na nini maana yake?