Ndugu zangu naomba ufafanuzi, Hivi ndivyo inavyopaswa Kuwa?

Linamo

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
9,976
24,490
Naomba hiki nachokiandika hapa kisitafsiriwe kama chuki baina ya wakristo dhidi ya ndugu zetu waislamu ila ni katika kuelimishana tu na kuwekana sawa.

Muda huu niko kwenye daladala natoka tabata naenda posta kwenye siti ya jirani kakaa dada mmoja kavaa mavazi ya heshima sana baibui na nikabu na miguuni kavaa soksi hivyo hata vidole vyake vya miguu havionekani ila kilichonifanya niandike thread hii ni kucha bandia alizobandika huyu dada katika vidole vyake vya mikono ni ndefu sana akiwa kazipaka rangi ya kijani.

Na usoni akiwa amepaka manjano kama nilivyosema mwanzo kavaa nikabu ila bado inaonekana kupitia nafasi ya macho.
Naomba kujua hili huyu dada yuko sawa?

Vazi alilovaa na kucha bandia alizobandika?
 
Baadhi ya picha za mikono yake.
 
Attachments

  • 1425462361434.jpg
    1425462361434.jpg
    44.7 KB · Views: 1,293
Sio kucha bandia tu hata oriji hazitakiwi ktk uislamu.

Kucha zinatakiwa zikatwe, kufuga kucha ni uchafu, ukilala kucha zinakukuna sehemu mbali mbali hasa kwenye nyuchi.
 
Hivi ndivyo anavyoonekana kwa juu
 
Attachments

  • 1425462499085.jpg
    1425462499085.jpg
    22.1 KB · Views: 1,140
Sio kucha bandia tu hata oriji hazitakiwi ktk uislamu.

Kucha zinatakiwa zikatwe, kufuga kucha ni uchafu, ukilala hujui kucha zinakukuna sehemu mbali mbali hasa kwenye nyuchi.

Asante kwa ufafanuzi.
 
Mkuu hukufanikiwa kupata namba za huyo demu ?, kama vp nirushie kwa PM ili nimkanye hiyo mitabia yake mana hata mimi ni muislam
 
Nafsi yake haijajaliwa kujazwa na mafunzo ya dini yake,bali mazingira aliyonayo(environmental influence/driving factors) ndo yanamfanya afate baadhi ya taratibiu za dini ikiwemo kuvaa Hijab.
 
Nafsi yake haijajaliwa kujazwa na mafunzo ya dini yake,bali mazingira aliyonayo(environmental influence/driving factors) ndo yanamfanya afate baadhi ya taratibiu za dini ikiwemo kuvaa Hijab.

Nimekuelewa ila mkuu hii inaleta picha gani kwa wanaomtazama? Je haileti tafsiri tofauti kuhusu dini yenu pale watu wanapomtazama?
 
Nimekuelewa ila mkuu hii inaleta picha gani kwa wanaomtazama? Je haileti tafsiri tofauti kuhusu dini yenu pale watu wanapomtazama?

Nikusahihishe kidogo,mie si wa Dini hiyo.Coming to the point..obvious si picha nzuri na wengi wao wako hivyo.Hayo mavazi wengi wao wanavaa kwa shinikizo la Imani bali si msukumo wa utashi wao wenyewe kwa kuzingatia mafunzo ya Dini.
 
Duh unawezaje kumpiga mtu picha kwenye daladala? Sasa hivi nitskuwa makini mtu akiinua simu namcheki anafanya nini!
 
duu utandawazi huu usifanye kitu ukijua upo peke yako, haya sasa dada wa watu hata hajui kama amepigwa picha
 
Nimekuelewa ila mkuu hii inaleta picha gani kwa wanaomtazama? Je haileti tafsiri tofauti kuhusu dini yenu pale watu wanapomtazama?

Ndugu yangu dini ya uislam haingalii mtu anafanya nini lakini mafundisho ya dini yanasemaje ambayo ni Quran na hadithi tu, Kwa hiyo hata akiwa imamu wa msikiti ikiwa anayoyafanya ni kinyume na quran na hadithi huwa anafanya makosa. Hayo mavazi yake huyo dada hayaamaanishi kuwa yupo sahihi kwa matendo yake yote ila amejaribu kufuata baadhi ya sharia na kupuuza nyengine hilo ni kosa lake yeye binafsi sio uislam ulomuamrisha hivyo na ndio maana hata wewe ukashangaa kwa kumuona kachanganya mambo.
 
Aise wewe ni noma kwa udukuzi, mipicha hiyo sidhani hata jirani yako katambua. back to topic Kiukweli wengi wao waavaa hivyo si kwa utashi wao bali msukumo wa kifamilia na jamii yao kwa minajili ya kidini, mimi binafsi huwa nawaogopa na hunitisha sana hasa hao wafunikao gubigubi,
 
Siku hizi hata wakristo wanavaa sana wakiwa wanaenda kwenye michepuko ya sehemu ambazo wanaogopa kujulikana. Mtoa mada tunaomba uhamasishe wenzio ili mahakama ya kadhi hitambuliwe na katiba ili tuwa wajibishe watu wenye tabia hiyo.
 
Nikusahihishe kidogo,mie si wa Dini hiyo.Coming to the point..obvious si picha nzuri na wengi wao wako hivyo.Hayo mavazi wengi wao wanavaa kwa shinikizo la Imani bali si msukumo wa utashi wao wenyewe kwa kuzingatia mafunzo ya Dini.

Ubarikiwe mkuu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom