Ndugu yangu hanisaidii chochote chuoni, maisha yameniwia magumu

Yusomwasha

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
2,092
838
Natumai mko salama ndugu zangu,

Mimi ni mwanafunzi wa chuo hapa arusha ila napitia kipindi kigumu sana hapa chuoni cha kukosa hata pesa ya matumizi.Maisha yameniwia magumu sana nimekopa mpaka basi mwenzenu wazazi wangu ndo hivyo tena ni watu wanaotegemea kilimo tu tena cha msimu.

Baba yangu hajishughulishi na kazi yoyote ile kazi zote anafanya mama nyumbani, maisha huku yamekuwa ni magumu pesa ya matumizi imeniishia ndugu zangu sina jinsi nimeshinda na njaa na sasa hivi naenda kulala sijala chochote.Maisha yamegeuka mwiba kwangu najiuliza why me?Kwanini mungu ni mimi tu?Nipo semester ya pili ila nashindwa kununua hata notes za darasani

Naombeni ushauri wa mawazo, msaada maana hata sijui nitaishije

Naomba mnisaidie hata kwa kazi zozote za jumamosi na jumapili nipo tayari kufanya nipate cha kujikimu huku chuo.

ahsanteni
 
Anza na kutafuta shughuli eneo karibu na wewe...ikibidi nenda nyumba ya ibada then watatokea wasamaria wema.

Njoo PM nitakupa food for thoughts.

Ila ukiomba ushauri humu uwe mvumilivu.... watu wenye kejeli ndio wametoka kazini muda huu.

Be strong matatizo hayo y atapiga.
 
Unapokopa unategemea kurudisha kwa njia gani? Na ugumu iko katika mahitaji ya kila siku au ada? Hapo Ar kuna watu wafua nguo za wanafunzi wanaoishi hostel au nyimba binafsi kufua na kupiga deki, jaribu kuanzia na hao. Yatapita haya na elimu yako itakusaidia aidha kuwa na biashara au kazi nzuri.
 
Unapopitia ndo wengi waliofanikiwa wamepita humo humo. Next time ukipata hela nunua mchele wa kutosha muda wote utakaokuwa shuleni say miezi 3 basi nunua hata wa mwezi then uwe na ratiba ya kupika mwenyewe hata kama hawaruhusu hostel tafuta namna huwa ipo haikosekani.
 
Mmmmmmhmn......ila dhambi sana.......masiki mtoto wa watu anasoma kwa shida utadhani sio nchi yake hii halafu mapumbavu machache yanatafuna pesa za serikali kiasi kwamba yanachukua hadi ambazo zingesaidia wasiojiweza kama huyu masikini........
Sina cha kukushauri ila nakwambia tu mwambie MUNGU ......maana kuna muda pakutokea hakuna hadi inabidi utegemee muujiza wa MUNGU tu utokee ndio na wewe upone
 
Natumai mko salama ndugu zangu,

Mimi ni mwanafunzi wa chuo hapa arusha ila napitia kipindi kigumu sana hapa chuoni cha kukosa hata pesa ya matumizi.Maisha yameniwia magumu sana nimekopa mpaka basi mwenzenu wazazi wangu ndo hivyo tena ni watu wanaotegemea kilimo tu tena cha msimu.

Baba yangu hajishughulishi na kazi yoyote ile kazi zote anafanya mama nyumbani, maisha huku yamekuwa ni magumu pesa ya matumizi imeniishia ndugu zangu sina jinsi nimeshinda na njaa na sasa hivi naenda kulala sijala chochote.Maisha yamegeuka mwiba kwangu najiuliza why me?Kwanini mungu ni mimi tu?Nipo semester ya pili ila nashindwa kununua hata notes za darasani

Naombeni ushauri wa mawazo, msaada maana hata sijui nitaishije

Naomba mnisaidie hata kwa kazi zozote za jumamosi na jumapili nipo tayari kufanya nipate cha kujikimu huku chuo.

ahsanteni
Bwana mdogo humu usije ukajidai unadanganya na ukazani hawatajua. Una thread yako moja inasema " Mke wangu anataka kuwa mweupe, atumie kipodozi gani kisicho na kemikali "? ... VIPI MKE ANAENDELEAJE?
 
Bwana mdogo humu usije ukajidai unadanganya na ukazani hawatajua. Una thread yako moja inasema " Mke wangu anataka kuwa mweupe, atumie kipodozi gani kisicho na kemikali "? ... VIPI MKE ANAENDELEAJE?
Hahaha kweli watu hawakuachi hivi hivi
 
Bwana mdogo humu usije ukajidai unadanganya na ukazani hawatajua. Una thread yako moja inasema " Mke wangu anataka kuwa mweupe, atumie kipodozi gani kisicho na kemikali "? ... VIPI MKE ANAENDELEAJE?
Hawa madogo siku hizi wana mambo mengi harafu akili fupi. Anapewa hela ya kujikimu anadandia mengine. Nina madogo wa hivi wamenichosha ni full maigizo kila siku.
 
Ni kweli ni.mimi nilipost hiyo habari ya vipodozi ila kiukweli alikua ni mke wa rafiki yangu aloniomba nije kumsaidia kuomba ushauri humu kuhusu vipodozi
Ila kiukweli hata mungu ni shahidi kwa niliyoyazungumza hapa maisha nayopitia chuo kwa sasa ni.magumu.sana jamani
 
Loh aiseee nilishataka kum PM anipe namba nimtumie hata buku ten aione kesho walau....dah. watu kama hawa watafanya wengine wenye shida wasipate misaada.

Ndio mkuu vijana akili sijui wanampa nani
Hata uongo pia unahitaji akili sasa wenye shida za kweli watazidi kukosa nafasi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom