Ndugu yangu anataka kuniunganisha QNET, nipeni maswali ya kwenda kuwauliza

Mi kuna mtu ninaeheshimiana naye sana aliniambia amepata dili zuri ameona anishirikishe tutajirike pamoja. Nikaingia hasara ya mafuta kama elfu hamsini hivi kumfuata nikijua naendea utajiri. Nilipofika nikakuta watu wengine wanne na picha kibao ukutani watu wamepiga pembeni ya magari au nyumba zao.

Machale yakaanza kunicheza hapa nimeingia cha kike, niliposikia ‘good morning’ kwa sauti ya juu nikajua ndio wale wale. Wakati wanaanza kujitambulisha mimi simu ikaita nikatoka kwenda kupokelea nje na kutokomea. Sikutaka kuwapa muda hata wa kuanza kunipiga sound.
 
Vip mkuu ushakutana nao hao Alliance??
Maana mm kila wakieka vikao vyao wananitaarifu nihudhurie but cjawahi kwenda hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bora alliance wapo vizur kuliko hao matapel Wa Qnet coz Tena kampun Yao alliance imesajiliwa kisheria kabisa pia wana reseni ya biashara Harfu Mambo Yao na seminar zao zipo wazi kwa kila mtu na wala si mafichoni Kama hao Q.

Alliance ukiwa tu mchapakazi Ni rahis kutoboa kwasabab kule hakuna 4mln. Ukipata mda pia waweza kwenda kwenye seminar zao kuongeza maarifa zaidi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi walinifanyia hivyo na aliyenileta ni mtu wa karibu sana hata sikuamini kama angenifanyia huo ujinga. Waliniita hapa Mwenge opposite na mlimani city wana kiofisi chao, alafu hakuna bango wala nini ni kama nyumba ya mtu. Machale yalinicheza jamaa anavyonikaba hataki niongee hovyo na watu au kuwashirikisha kabla sijaelewa vizuri. Nikasema poa.
Nilishtuka pale nilipowaambia sina hiyo hela kwa sasa labda wakati mwingine, wakaja kunishawishi niuze gari au hata shamba maana hili dili linalipa. Kuanzia siku hiyo hata simu yake nilikuwa sipokei.

Baada ya muda kidogo nikaenda mkoani kusalimia ndugu zangu, nikakuta kuna shemeji yangu kalizwa ni muda mrefu tu anaugulia maumivu hajala hata senti tano, you can imagine. Alafuhuyo shemeji yangu ni mwalimu, fikiria maisha ya walimu yalivyo, hela kaenda kukopa, sasa hivi anafyekwa makato na hakuna cha dola wala nini.

Watanzania tujifunze kufanya kazi kwa jasho letu, jifunze kufanya savings na kuwekeza kwenye kitu ambacho una uhakika nacho. Wazungu wanasema when you carry your own water you will know the value of every drop. Heri uwekeze akiba zako hata kama ni buku tano, hata mbuyu ulianza kama mchicha. Tusipende mafanikio ya kupanda na lifti. Badala yake, panda ngazi, japo utatoa jasho utafika kwa uhakika.
Nawatakia siku njema
Mie niliitwa Jumatano iliyoisha Jijini Mwanza wana ofisi ina picha za magari ukuta mzima. Wako Buzuruga Shule. Hawataki uongee hizi habari zao hadharani. Kiingilio cha chini ni package ya Holiday 4.2m. Wamenishawishi nikakope bank ili ndani ya wiki 3 tayari inarudi. Mbaya zaidi swali wasilolipenda ni rafiki aliyekuunga ana muda gani kwa hawa qnet na yeye kafaidika kwa lipi?

Hawataki kulisikia kwa sababu tunajuana tunavyoishi. Ni waongo kuliko maelezo mtaani hapo wamebatizwa jina la F. Mason kwa sababu wako ofisini muda wote wanapiga makelele.
 
Kila nikifungua Uzi unaohusu Qnet nacheka peke yangu mpaka nimalize kusoma,nilikuta wameweka Picha ya Kigwangara eti alifungua sijui kitu gani akaitaja na Qnet basi wanazunguka na kapande ka gazeti dar nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha sikutaka kuweka comment yangu leo ila ngoja niiweke tu jamaa hawa ni hatari! Q- net ni kama DINI aisee cha ajabu wasomi wanashinda ata kupitia forums mbalimbali za biashara anayotaka kuingia mfano ata ukikosa jamii forum jaribu kuingia orrior forum au Quora lazima upate thread za kutosha kuhusu MLM business
 
Mi kuna mtu ninaeheshimiana naye sana aliniambia amepata dili zuri ameona anishirikishe tutajirike pamoja. Nikaingia hasara ya mafuta kama elfu hamsini hivi kumfuata nikijua naendea utajiri. Nilipofika nikakuta watu wengine wanne na picha kibao ukutani watu wamepiga pembeni ya magari au nyumba zao. Machale yakaanza kunicheza hapa nimeingia cha kike, niliposikia ‘good morning’ kwa sauti ya juu nikajua ndio wale wale. Wakati wanaanza kujitambulisha mimi simu ikaita nikatoka kwenda kupokelea nje na kutokomea. Sikutaka kuwapa muda hata wa kuanza kunipiga sound.
Nataka siku nirudi pale ofisi yao ya MIKOCHENI nikawakere kidogo kwa maswali maana nillikimbia semina ya 2 ya kwanza tu niliona inanipotezea muda ila alienipeleka ndio nlkua namheshimu sana sikutaka ajue nimekasirika that day coz alinivunjia ratiba ya kwenda kutafuta pesa kwa sababu ya kusikiliza salam ya primary GOOD MORNING! Ukiwaona utasema ni watu wa maana vile mara ooh eti Business Partner
 
Nataka siku nirudi pale ofisi yao ya MIKOCHENI nikawakere kidogo kwa maswali maana nillikimbia semina ya 2 ya kwanza tu niliona inanipotezea muda ila alienipeleka ndio nlkua namheshimu sana sikutaka ajue nimekasirika that day coz alinivunjia ratiba ya kwenda kutafuta pesa kwa sababu ya kusikiliza salam ya primary GOOD MORNING! Ukiwaona utasema ni watu wa maana vile mara ooh eti Business Partner
 
Mi kuna mtu ninaeheshimiana naye sana aliniambia amepata dili zuri ameona anishirikishe tutajirike pamoja. Nikaingia hasara ya mafuta kama elfu hamsini hivi kumfuata nikijua naendea utajiri. Nilipofika nikakuta watu wengine wanne na picha kibao ukutani watu wamepiga pembeni ya magari au nyumba zao. Machale yakaanza kunicheza hapa nimeingia cha kike, niliposikia ‘good morning’ kwa sauti ya juu nikajua ndio wale wale. Wakati wanaanza kujitambulisha mimi simu ikaita nikatoka kwenda kupokelea nje na kutokomea. Sikutaka kuwapa muda hata wa kuanza kunipiga sound.
Nimecheka hadi machozi yani
 
milioni 4 mbali sana wangesema kiingilio laki 3 hapo wangetupata wengi Tu,
Mi aliyenipeleka tunaheshimiana Sana semina ya pili nilienda nikakomaa Sana tu kuwa hiyo M4 siwezi pata zaidi ya kukopa hapa kwenu nikaaga kuwa siku nikiipata ntakuja...

Ila wana mkwala eti good morning

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu!

Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu

Awamu ya kwanza!

Ilikuwa majira ya saa moja jioni ndugu yangu alinipigia simu na kuniita ofisini kwake huku akinisisitiza nisikose kwenda kuna issue muhimu anataka kuniambia! Bila kubisha nikamuitikia na kumwambia nitahudhuria wito huo kesho saa tano kamili asubuhi!

Kesho yake nikajiandaa na kwenda moja kwa moja ofisini kwake! Alinikaribisha sana na hatimaye akaanza kutiririka

"Ndugu yangu karibu sana, Mimi na wewe tunaheshimiana sana na nimependa jinsi unavyoendesha maisha yako! Hapa nimekuitia fursa, na Fursa hiyo ni mambo ya network market.....bila shaka ushawahi kusikia kuhusu network marketing!

Nikamwambia Ndio, ila nikajua anazungumzia uuzaji wa vitu mtandaoni mfano Alibaba.....

Akaendelea " Kuna kampuni inaitwa Qnet, Kampuni hii imetajirisha wengi sana,

(hapa akainadi mno)
Mwishoni akaniambia, nimeshakopa pesa kwa ajili ya biashara hii, hivyo nataka nikishafanikiwa kujiunga na wewe nikuunge! Nikasema sawa!!! Baada ya siku kadhaa kupita akanipigia simu niende ili nikakutane na watoa elimu wa kampuni hii ya Qnet!

Hatimaye nikaenda! Nilikaribishwa vizuri nikaambia nisubiri nje, ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni..... baada ya muda nikaingia ndani nikatambulishwa kwa staff wao pale ofisini, Wakasalimiana GOOD MORNING, HUYU MBELE YENU NI Mr. X, Kaletwa na Huyu Mr Y, Nikakaribishwa na kutambulishwa watu wote niliowakuta pale!

Nikapelekwa chumba kingine kwa ajili ya kupewa mafunzo kuhusu Qnet!

Walinieleza Qnet ni nini, Chimbuko lake, waanzilishi na shughuli zao na kikubwa ni wadhamini wa Manchester City, na Ligi ya mabingwa wa Africa na mchezo wa mbio za magari formula one!

Kisha wakanipa elimu jinsi ya kupata dollar 200$

Wana Jf mambo ni mengi nilielezwa, na mimi nimepitia nyuzi mbalimbali humu Jf kuwa Qnet ni utapeli tu! wadau wengi wameielezea kiundani Qnet in negative ways!

Kesho naenda kupata mafunzo awamu ya pili, Ndugu zangu nipeni maswali na hoja za msingi nikawahoji hawa watu......

Yapo maswali niliyowauliza nitayaleta na majibu yake baadae!

ila kwanini wanasalimiana Good morning hata kama ni usiku ni kwamba kampuni ilipitisha salamu moja muda wote na kwa mataifa yote!

Karibuni!




Sent using Jamii Forums mobile app
Tupe mrejesho mkuu
 
IMG_2138.png

Pyramid schemes

ni mfano wa biashara ambao huajiri wanachama kupitia ahadi ya malipo au huduma kwa kusajili wengine katika mpango huo, badala ya kusambaza uwekezaji au uuzaji wa bidhaa. Kama kuajiri huzidisha, kuajiri inakuwa haiwezekani haraka, na wanachama wengi hawawezi kupata faida; kama hivyo, mipango ya piramidi haiwezi kudumishwa na mara nyingi ni haramu.
 
Back
Top Bottom