Ndugu yangu anataka aolee kwenye mji wangu

Ndugu yangu anataka aolee kwenye mji wangu

bush crazy

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
773
Reaction score
1,087
Poleni na kazi wakuu!

Nimebahatika kuwa na mji wa kawaida wenye apartment. sasa kuna ndugu yangu naishi naye anampango wa kuoa mwakani ameniomba aishi hapa hapa kwenye moja ya apartment hata baada ya kuoa. sasa wakuu hii ipo sawa?
 
Mwache aoe tu,
Kwani akioa wewe binafsi unapata shida gani?

Si unaona yule mjukuu wa Malkia sijui Prince Hurry alipomwoa Mergan Markle amehama kwa bibi yake ameanza kukitegemea?

Sometimes mtu akioa mke anaweza kumfungua akili so be humble,
 
Na akizingatia ni ndugu yake
 
Poleni na kazi wakuu!

Nimebahatika kuwa na mji wa kawaida wenye apartment. sasa kuna ndugu yangu naishi naye anampango wa kuoa mwakani ameniomba aishi hapa hapa kwenye moja ya apartment hata baada ya kuoa. sasa wakuu hii ipo sawa?
Kwamba hawezi kupanga kwenye nyumba karibu na ya kwako? Tatizo nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona suali lako hujaliweka wazi kwa mambo mengi tu. Kwa mfano umesema ndugu yako anakaa na wewe katika apartment hiyo, lakini hukusema kama anachangia rent, bills, chakula n.k. Pia hiyo apartment ina vyumba vingapi? wewe uko single au una mke na watoto? Huyo ndugu yako anapanga kukuaa hapo baada ya ndoa kwa muda gani? Ukiweka bayana haya naona utaweza kujibiwa vizuri, vyenginevyo watu watakujibu kwa kuenda na assumption zao.
 
Kama anajiweza kujimudu kivyake muache tu. Labda kama anakutegemea kwa kila kitu ndipo utafanya maamuzi.
Zingatia undugu na kipato chake. Naamini hadi kufikia maamuzi ya kuoa, anaweza kujimudu kwa chakula na mambo mengine.

Kuna jamaa aliolea mke wake kwa babake mdogo, akawa anachangia sana chakula na mambo mengine ya nyumbani. Watu na ndugu walimsema vibaya sana ila hata hakujali.

Baadae alitoka kwenda mjini, akafanikiwa. Akampeleka na mke wake mjini. Wakafanikiwa vizuri.
Baadae yule babake mdogo akafilisika kabisa.

Yule kijana alifikiria Wema aliofanyiwa na yule baba, akaumia sana. Akamsaidia kwa kumpa pesa za biashara na kukomboa nyumba yake iliyokuwa ikitakiwa kupigwa mnada.

Kama unaona atakuwa mzigo kwako, bora umshauri asioe.

Tafakari, chukua hatua.
Zakuambiwa changanya na zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom