Ndugu wanavyoweza kuwa adui wa kutajirika kwako

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
10,433
13,416
Baada ya kusoma kwa kuunga unga kwa msaada wa ndugu jamaa na marafiki nilifanikiwa kufaulu chuo kikuu na kumaliza kwa grade nzuri by then kazi enzi za mkapa zilikuwa bwerere, nikakamatia kazi nikaanza kuishi maisha niliyokuwa nayaona kwa bongo muvi nikakopa ka gari nikapanga sinza ,kamata pisi kali (badae nilijua malaya wa mjini) sikuwa pimbi (mi ni chuganian ila wacha dar iitwe dar .Basi nkaacha kaya nkajiunga na vijana wanywa bia daily sinza ukweli kazi yangu haikuwa na mshahara mkubwa ila nature yake inakusogeza sana na matajiri ni mambo ya consultancy .

Twende kwenye topic basi mizinga ya ndugu ilianza kwa kasi kwa kweli nilikuwa sina jinsi nilijitoa balaa nikijipa moyo mimi bado mdogo muda wa kuwa serious bado hii mitaji ya laki 5 hadi mil 1 haipungui hata 20 mil wote ukimkopa anafungua genge la nyanya badae anakaa miezi sita anaomba laki mbili umuongezee laki mbili auze na samaki wa kukaanga etc ila kila akiota kukuwa ananigeuza mm bank basi bwana ikatokea nikaanza kuwakatalia nikiwaambia kakopeni bank mimi hapo imetosha sijui walinipiga kipapai kazi ikaota magugu.

Mchezo ukaanzia hapo kila mtu ananisema niliendekeza totoz demu akanitema kuchunguza malaya anaejiuza ,basi pango likanishinda kuna rafiki anaishi kwa nyumba yake ya urithi uswazi akaniambia we usijali hamia kwangu niamini mimi hakuwa hata mshikaji kiivyo .basi muhuni nkachoka balaa ile kushinda mtaani nkapata washikaji wa kula nao viloba uzuri pa kulala uhakika mchana nashinda stationery nasaidia kutype by then computer skill zilikuwa adimu kitaa basi nikajiunga na udalali wa nyumba na vyumba ukichanganya na usomi muda mfupi nkapanga mahali survey mwenge japo rafiki yangu alinisihi nisiende mitaa hiyo ntarudia mastarehe .

Maisha yalikuwa ya kubangaiza hadi mwaka juzi nilipo umiza kichwa nikaja na idea yangu ya siri ya kupata hela .Asee tangu hapo nimekuwa na roho mbaya najishangaa yaani nimejenga in short time bila kumuarifu hata ndugu mmoja hata namba yangu hawana kuna siku mmoja aliniunga kwa whatsup group ya familia nkamuuliza umetoa wap namba yangu nikajitoa ,toka hapo asee naona nyota ya utajiri ileeee, Ndugu walioniita teja wanasema nauza dawa za kulevya cha ajabu muhu hata pombe nimeacha nawaprove wrong sana mwakani nampango wa kuhama bongo baada ya corona nihamie zangu kenya maana ridhiki yangu na tajiri wangu ni wa huko .

Ushauri : SAIDIA NDUGU LAKINI ELEWA HATA BILL GATES ANA NDUGU MASIKINI KUWA NA KIASI ,UMASIKINI WAO NI JUKUMU LAO KULITATUA WEWE UNAPASWA USAIDIE KWA KIASI TU ,MAISHA YAO SIO YAKO,NDO MAANA HAWAAMUI MATUMIZI YAKO WALA WEWE HUAMUI YAO ,WAPENDE NDUGU HASA WAKATI WA MAGONJWA ,KESI NA NJAA.MAMBO YA KUTAFUTA UTAJIRI NI MAMBO YA MMOJA MMOJA .KUMBUKA WANAO HATA KAKA YAKO WA DAMU AWE BILL GATES HAWATARITHI HATA BUKU .
 
Safi kabisa!

Kuna baadhi ya Koo ni Kama zina laana ...jitahudi usirudishe mawasiliano nao labda wazazi. All the best
 
Unadhani ni wapi ulitumia pesa nyingi hadi ukayumba kati ya kuwasaidia ndugu au kula tungi na totoz?

Hilo dili la siri ungetufunulia na wenzio sasa...
 
Wabongo wakipata chaka la kupiga hela huwa hawasemi abadani!! Hata ubembelezwee vipi husemi

Ndo nashangaa akina ONTARIO wanaoita watu et njoo kwenye mishe fulani upige pesa
 
Wabongo wakipata chaka la kupiga hela huwa hawasemi abadani!! Hata ubembelezwee vipi husemi

Ndo nashangaa akina ONTARIO wanaoita watu et njoo kwenye mishe fulani upige pesa

Kwajinsi wabongo tulivyo na roho mbaya na ya kwanini Bora kutosema tu mkuu...
Alafu wabongo wengi tunapenda Sana shortcut...unahis ukipewa deal.utaliweza Sasa...huna lolote mradi usikie tu..lols!
 
Unadhani ni wapi ulitumia pesa nyingi hadi ukayumba kati ya kuwasaidia ndugu au kula tungi na totoz?

Hilo dili la siri ungetufunulia na wenzio sasa...
Nikisha lisema linakuwa sio dili tena ,ntabidi nirudi nlikokuwa
 
Wabongo wakipata chaka la kupiga hela huwa hawasemi abadani!! Hata ubembelezwee vipi husemi

Ndo nashangaa akina ONTARIO wanaoita watu et njoo kwenye mishe fulani upige pesa
Tatizo linakuja hata wewe ukiitwa kwenye fursa hio huna commitment yeyote

Mimi Wala jamaa naofanya nao kazi hawwajui natoa wapi hela japo mshahara wangu wanaujua

Wanaona vitu tu baadhi vingine wala hawavijui Basi kwakuwa walianza kazi muda mrefu Wana ku underrate sana huwa nawazoom tu

Kuna siku nitayeyuka ghafla bila kuwaaga nasepa huko mkoani kula Bata wao wakiendelea na kuganga njaa na Tambo zao

Mbongo usimpe mchongo mnafiki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo wakipata chaka la kupiga hela huwa hawasemi abadani!! Hata ubembelezwee vipi husemi

Ndo nashangaa akina ONTARIO wanaoita watu et njoo kwenye mishe fulani upige pesa
Njia ya kugundua deal la kupata pesa ya kishoga kuliko zote ni kusubiri mpambanaji aliezigundua kwa gharama ya kuteseka uswahilini miaka saba kwa kukwambia ww bure ,umiza akili ugundue lako .hata ikibidi kusema ntaanza na ndugu kisha marafiki etc sio ww
 
Tatizo linakuja hata wewe ukiitwa kwenye fursa hio huna commitment yeyote

Mimi Wala jamaa naofanya nao kazi hawwajui natoa wapi hela japo mshahara wangu wanaujua

Wanaona vitu tu baadhi vingine wala hawavijui Basi kwakuwa walianza kazi muda mrefu Wana ku underrate sana huwa nawazoom tu

Kuna siku nitayeyuka ghafla bila kuwaaga nasepa huko mkoani kula Bata wao wakiendelea na kuganga njaa na Tambo zao

Mbongo usimpe mchongo mnafiki sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda mm naishi dunia yangu ,mi navyojua hela ni kama kugundua siri ya kutibu korona ,je nimwambie mtu mwingine? mbona watu wanapenda urahisi hivyo mi huwa nakuja na utafiti wangu naunganisha dots nakuja na wazo kabambe ,mfano kuna kipindi wahindi walikuwa wananunua magamba ya miti flani ya kutengenezea quneni ile dawa ya malaria ,basi watu kibao wakawa wanaenda congo kuchukua mimi nilipoiona nikasema inamaana tanzania nkanunua sampo kama kilo 30 nkawa natumia watu maporini kilipita kimya baada ya mwaka akaja mbabe mmoja akanambia ipo kibao kigoma mapori ya kibondo basi muhuni nikaenda wooow mzigo huu hapa nawalipa wanakijiji tshs 4000 kwa kunikusanyia gunia mimi naliuza 120,000 kwa mhindi ,sasa kaka ulitaka nikuambie oya kuna mchongo wa hivi inamaana wakijua wengine hawatakaa waende kongo na dili lang litakufa so mchongo wa hela ni siri ya kazi ngumu ya kujimyima na bidii alayo matunda alietoa jasho tuuu.
 
Ni kweli hapa pana ukakasi sana na bahati mbaya unapojibana na kuwapa chochote wao ndio wanazidi kuona kuwa unazo za bure bure.
Mm nishasema siwezi maliza shida za watu hivyo huwa nina kiasi ninachotenga kwa dharura kikiisha hicho hapati mtu isipokuwa wazazi wangu tu walionilea.
 
Back
Top Bottom