Ndugu wana jf. Nani anastahili katika hili mtendaji wa kijiji au polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu wana jf. Nani anastahili katika hili mtendaji wa kijiji au polisi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by buhange, Nov 19, 2011.

 1. buhange

  buhange JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 23, 2011
  Messages: 494
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Wadau! na wana_JF

  Nimekaa na kutafakari sana juu ya mashwara kadhaa ktk mfumo wa utawala wa serikali yetu. Mathalani utamaduni wa nchi hii ni kupeleka vyuo vya ualimu wale wote wenye daraja la tatu, la nne na hata daraja "0" kama unakigogo wa kukukingia gamba. Matokeo yake ni kuwanyanyasa na kuwatisha wawapo ktk uwanja wa ajira, mara tutakutimua ukigoma,tutakupeleka kijijini ukaanzishe shule mpya n.k

  Kilio hiki kipo pia kwa ndugu zetu "Watendaji wa vijiji" a.k.a ma' VEO. Kiukweli wanamazingira magumu ukiachilia mbali mshahara wao wa laki moja na usheee! mazingira yao ya kazi hayawapatii furusa ya hata kumiliki RUNGU kama siraha ya kujilinda. Tunajua wazi kwa ma' VEO na WEO's hawa ndio hasa washughulikiao kesi za uhalifu maeneo yetu ya vijijini iwe Wizi(uporaji au unyang'anyi), mambo ya ugoni, na ukusanyaji michango.

  Hivi leo hii mtendaji mwadilifu akiwa na migambo wake anakamata majambazi tena wenye silaha za hatari, halafu baada ya kuwafikisha polisi jioni unakutana nao mtaani wakiwa huru, Nini definition ya usalama wa VEO na MIGAMBO wake wasio na silaha zaidi ya MARUNGU?

  Mfano, "mwanzoni mwa mwaka huu lilitokea tukio la kinyama huko mkoani TABORA, wilaya ya URAMBO, tarafa ya KALIUA kijiji cha ZUGI MULOLE(KM. 34) ambapo mtendaji wa kijiji hicho alikutwa nje ya nyumba yake nyakati za asubuhi akiwa ameuwawa kinyama na watu wasiojulikana kwa kujinjwa na kichwa chake kutenganishwa na mwili zaidi ya yote kichwa kilikutwa kikiwa kimetobolewa macho yote".

  Sasa kama watu wenye mamlaka ya kumiliki silaha kama Polisi huwa wa mwisho kujitokeza katika kila matukio ya uhalifu kama ujambazi, halafu watu wenye majukumu muhimu kama ma-VEO wakiachanizwa ili makubwa yawakute, nani mwenye haki ya kupewa haki ya kumiliki silaha, MTENDAJI WA KIJIJI au POLISI watumiao silaha zao ktk kutawanya walipa kodi wakati wakiwa ktk maandamano yao ya kudai haki?

  Na Je! nani ana haki ya kulipwa mshahara mkubwa, MWALIMU au WAKUU WA WILAYA na MIKOA aina ya kina BENDERA,MECK SADIKI NA MULONGO?

  Maoni yenu wadau tafadhari!
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Unataka kusema hao VEO's wakipewa silaha wana uwezo wa kupambana na majambazi!.
   
 3. h

  hubby Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona mfalme **** amerudi.
  kilakitu ratili moja......
  Shabash.!!!!!!
   
Loading...