Ndugu wafariki kwa shoti ya umeme

Ndugu wafariki kwa shoti ya umeme

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Watu wawili wa familia moja, Zulfa Chami na Zuhura Chami wamepoteza maisha, baada ya kupigwa shoti ya umeme na kamba ya kuanikia nguo katika eneo la Pasua, Manispaa ya Moshi.

Zulfa (24) na Zuhura (28) wamefikwa mauti hayo leo wakati wakianika nguo.

Habari zilizopatikana kutoka eneo la tukio na baadae kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi, Hamisi Issah zinaeleza kuwa ndugu hao wa familia moja walifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa shoti ya umeme.

"Ni kweli ni mtu na dada yake wamefariki dunia leo kati ya saa 3:00 na 3:30 asubuhi katika eneo la Pasua Manispaa ya Moshi", amesema Kamanda Issah.

Chanzo - Nipashe
 
So sad!
Nadhani si kamba bali waya. Inaelekea kulikuwa na leakage ya umeme kati ya mfumo wa umeme wa nyumba husika, bati pamoja na waya wa kuanikia nguo.
Hapa ndipo tunapoona umuhimu wa kufunga circuit breakers zenye viwango vidogo sana vya leakage current (0.03mA) kwa ajili ya protection na kuhepuka ajali kama hizi.
Poleni sana wafiwa!
 
Zulfa nilisoma naye kifo hiki hatari kabisaView attachment 1033104
IMG-20190225-WA0015.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwanini tunapenda kutumia kamba za waya padala ya plastic material nyingine nadhan tanesco wawe na kitengo maalum cha kukagua au ushauri kuhusu miundo mbinu ya kamba au makaro ya nyumbani tupunguze hii problem
Umeandika vizuri sana dada. Inabidi iwe hivyo ili kupunguza madhara kwa jamii.
Wengi wa waathirika wa matukio kama haya hawana ABC kuhusiana na mambo ya umeme.
 
Back
Top Bottom