Ndugu wa mume kiboko aisee

Ndugu wa mume kiboko aisee

Tatizo la extended family ndio hilo mi nikioa ni wife na watoto tu ki ulayaulaya

Kuwa makini na wanawake ndugu yangu, atapenda akuweke mbali na ndugu zako ila ndugu zake ni poa wakija. Nadhani huo ni mkakati ili aweze kukutawala vizuri.
 
hahahahhaha naamini kwamba kila mtu ananafasi yake na hata kama yangu ni 20% ni ok hata yeye hawezi jilinganisha na baba yangu wakatika 50/50 never huyo ndio anayejua alimtoa wapi si tumekutana ukubwani lol.hiyo kujifanya ana share kwenye familia nyingine ndio tatizo.inaonyesha na wewe ndio katabia chenu ndugu wa mume nonono

hapa ulivyo eleza wala aujaonesha kosa la mama zaidi ya kumcheka na kumshangaa kumsubiri mwanae! hivi tatizo la huyo mama ni lipi? hivi uoni mumeo ana tatizo kumpita mama yake mzazi kama hamjui? hivi kweli hata ungekuwa mzazi wa huyo ungejisikiaje? sawa na kubali kuna mama wakwe wana matatizo lakini kwa hapa sijaona zaidi ya wewe kuonesha jinsi unavyo kerwa na mama mkwe hata kama aja kukosea! lakini ujafanya jipya sana chini ya jua!
 
hahahahhaha naamini kwamba kila mtu ananafasi yake na hata kama yangu ni 20% ni ok hata yeye hawezi jilinganisha na baba yangu wakatika 50/50 never huyo ndio anayejua alimtoa wapi si tumekutana ukubwani lol.hiyo kujifanya ana share kwenye familia nyingine ndio tatizo.inaonyesha na wewe ndio katabia chenu ndugu wa mume nonono

hapa ulivyo eleza wala aujaonesha kosa la mama zaidi ya kumcheka na kumshangaa kumsubiri mwanae! hivi tatizo la huyo mama ni lipi? hivi uoni mumeo ana tatizo kumpita mama yake mzazi kama hamjui? hivi kweli hata ungekuwa mzazi wa huyo ungejisikiaje? sawa na kubali kuna mama wakwe wana matatizo lakini kwa hapa sijaona!
 
najua sana na ninao mawifi lakini sisi sio wagonjwa wa akili namna hiyo hakuna wifi yangu anayejuta hata mmja kwanza kwenda tu kwao hapo mbezi ni mara moja kwa mwaka tena nikitoka kwenye shughuli zangu.kuna wifi mmja alikuja nkasikia aliingia chumbani kwangu hgal wakamwambia humo ni marufuku kuingia akasema naingia ni chumbani kwa kaka yangu akawa anatembea ndani kwangu na kanga moja au kitenge bila kitu kama mama mwenye nyumba hehehehe sidhani kama anatamani te a kuja hapa tena .

mmmh pole kwa yaliyokusibu hata ulimfanyaje? maana hatamani tena kuja kwako.....
 
Yaani umesema kweli. Mimi bwana mama mkwe huwa nampa nafasi kubwa hata ya kuongea na mwanae tena huwa akija nakua mbali nao kabisaa. Tukikaa pamoja nikihisi nawanyima nafasi basi hua naanzisha safari ya mbali ili kuwapa nafasi. jamani sisi tulioolewa ni vema tujue kua na sisi tutakua mama wakwe siku moja hivyo tuwatendee mama wakwe kama ambavyo na sisi tungependa kutendewa. Mimi mama mkwe wangu huwa nampenda sana na hivi hatuongei lugha moja ndio kabisaaaa huwaacha peke yao wajinafasi. Mazungumzo yao hayanihusu na nimempa mama mkwe rukhsa ya kuchukua chochote atakacho mradi kiwe ndani ya uwezo wangu tena ana uhuru kwangu kuliko hata kwa binti zake.

nimeipenda hii................ Mzazi ni mzazi jamani hata yeye ana hamu ya kukaa na mwanae na kuzungumza, sometimes anahitaji hata kudeka kidogo kwa mwanae, na kama mama kawaida huwa na hofu juu ya mwanae mpaka amuone kumbuka mtoto kwa mama hakui. Ukizingatia kama ni mkwe amekuja tu hapo kwa muda muache abond na mwanae hadi achoke yeye na akiondoka usiache kumkumbusha mumeo ampigie simu kila mara. Mambo mengine sio ya ku-mind.
 
Mimi huwa watu wengine wananishangaza sana!!kuna tatizo lolote kama mtu anafanya kitu na hakikudhuru??mama mkwe kakaa zake sebuleni anamsubiri mwanae,kama hakuna madhara yoyote kwako is it a big deal??kuna haja ya kumcheka mpaka unakaa chini??kuna haja ya kumzimia taa??mbona wewe ndo unatafuta uchokozi!?tuache mambo ya ajabu jamani!!tuache kukariri!!mama mkwe ni sawa na mama yako na sioni ubaya wa alichokifanya hapo!!wewe ndo unaonekana una wivu..kama na wewe ulihitaji kumsubiri mumeo ungeunga tela hapo na sio kujidai unashangaa..nimenote kitu kimoja kwa wanawake wa kitanzania wengi wao wanapenda mambo ya "u~mama mkwe na u~wifi "bila kujua kuna kipindi na yeye atakua wifi au mama mkwe!!ishini na ndugu za mume vizuri kama ni ndugu zenu vile..sikatai kila mtu ana mapungufu yake ila hicho kisiwe ndo kigezo cha kuanza kuonana wabaya!tuchukuliane vizuri na naamini ukijua kuishi na watu vizuri hakuna kitakachokupa presha!!

Asante, nimependa mawazo yako sana, umenena. MUNGU AKUBARIKI
 
mzaa chema anampenda mwanae acha pondea wewe mbona unakosa uvumilivu wa muda tu
 
Chezeya mama mkwe weye!!! hakawii kusingizia kuumwa ili apelekwe hospitali, au kususa kula akisubiri kula na mwanae. Mwanae akirudi yuko safi na kishapata nyama choma mtaani.

ha haaa, taratibu pacha, mama mzaa chema huyo, lol!
 
Kuna wanawake wengine kumbe ni shida? Bora mama yako asikutembelee kabisa nyumbani kwako.. Unaweza kupewa laana kumbe mkeo anamfanyia visa..
 
Sishangai.Kwenye ndoa changa, mwanamke akiona mama mkwe kawasili anapoteza confidence kabisa.anahisi mama mkwe atasema kitu ambacho kitaigharimu ndoa yake.
 
Ni kweli kuna mama wakwe wengine ni balaa kwa ukorofi ....lakini hapa sioni kosa lake, ni kumsubiri mwanae arudi tu?
Nilitegemea Nivea afurahie kampani ya mama mkwe,wakae pamoja kumsubiri baba mwenye nyumba.
 
Last edited by a moderator:
Nivea, story yako ni ya upande mmoja ila pia mumeo naye yaonekana anamkwepa mama yake. Kuna jambo na kuna walakini. Mtu huwezi kumpita mama yako mzazi sebuleni kwa salaam za hi! Hata siku moja! Imagine ingekuwa mama yako? Usije chekelea hapo pengine mama amegundua kitu kilichojificha kwa mumeo na kumkanya wewe unashabikia wakati hujui? Au labda anataka kuwaaga nyie mnajifanya mko busy? Kuna namna nyingi wazee huwa wanahitaji kuchukuliwa. Kuna binti hivihivi kama wewe akawa anamnanga mama mkwe kumbe mama alimbamba mwanaye mjini akitokeq gesti. Sasa mtoto aibu. Bqsi siku ya siku binti alimtolea mbovu mama mkwe ndipo mama mkwr akamweleza kuwa siku zote unaniona hapa namsubiri mumeo nataka niobgee naye jambo na ananikwepa na jambo lenyewe ndio hili. Binti aligwaya! Mama mkwe kumbe alishapaki vitu na aliondoka usiku uleule.
Kwa hiyo binti punguza munkari. Wapo wazee wenye matatizo na kuna namna ya kuwachikulia. Huyo ni mama mzazi wa mumeo. Hajaja kuchukua penzi lako. Kuwa mature na umwonyeshe kuwa pendo la mwanaye bado lipo na linawatosha wote. Mwanaye atamjali na atakujali na wewe. Usiharibu uhusiano wenu mapema. Safari bado ndefu ktk ndoa.
Nivea anateswa na ndoa changa.Wivu bwana, hadi kwa mama mkwe??????????????????
 
Last edited by a moderator:
ha haaa, namchekaga mama yetu akija kwako yaani kwanza unashukuru kakubali kuja, ila uwe na nauli tayari tayari otherwise ataenda kukata tiketi ya kurudi kwake kwa hela yake. hataki kabisa kukaa nyumbani kwa watoto.
Ukimwambia likizo anasema nyie watoto ndo mnapaswa kuja likizo nyumbani kwangu, siyo mimi kuja kwenu. yaani msipojipanga unaweza usionane naye hata miaka kadhaa, na hivi simu zinatudanganya mnaweza ongea kila siku basi siku zinakatika tu.
Inakuwaga sheshe mtu akijifungua kwetu, tunamwomba aje kutusaidia maana yeye ni nesi, anakuambia anayehitaji msaada wangu aje kujifungulia kwangu.....unalo?
Ila wifi yetu atapata raha sana, no mama mkwe/mawifi troubles...... kwa raha zake mwenyewe
c.c. Nivea
 
Last edited by a moderator:
Mimi naukubali ule msemo wa ni nani anammiliki mwanaume sio mama ila ni mkewe lolz.. Kama usipo enjoy kuwa na mwanao wa kiume kabla hajaoa imekula kwako!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mama ni mama tu hata ukiwa mkubwa kiasi gani. Nyerere alikuwa nanitwa na mama yake Butiama na alikuwa anatii mara moja!! JK akikataa kutii amri yake alikuwa anagoma kula mpaka mwanae aje!!
 
Sioni tatizo hapa! Wewe tu ndo ambae hujiamini! Sasa kama umechoka na kazi zako za siku nzima unasubiri nini kwenda kulala upumzike?! Akija ukamfungulie?!

Mara nyingi wazee huwa usingizi hawana sana tatizo liko wapi akiamua kumsubiri?!

Tatizo lenu ninyi wanawake ni kutaka kujilinganisha na wazazi, hilo haliwezekani! Kujilinganisha ni kujionea bure, unajua kabisa kila mmoja ana umuhimu wake kwa wakati wake.

Kaamua kumsubir mwanae sio tatizo. Maisha ya mijini kazi kutwa nzima na weekends vile vile mihangaiko muda hata wa kuongea nae hana,akaona amsubiri walau apate muda wa kuongea nae kipindi hiki alichowatembelea!

Kama wanaongea kwa kunong'onezana tatizo lako nini kama sio uwezo mdogo wa kujiamini?! Unadhani wanakusema?! Humuamini mmeo kiasi cha kufikiri anaweza kukusema vibaya na mzazi wake?!
Give them space. Huo ndio utu, haikusaidii kutaka kujua kila kitu, kwani hata mmeo huwa anakuambia kila kitu chake?! Fikiria tu.

Sio lazima kila anachoongea na mama yake wewe ujue kisa wewe ni mkewe! Sio lazima!

Jiamini, amekuoa wewe akaacha wazazi wake kuja kujenga familia na wewe! So unayo nafasi yako kwake! Kubwa tu!

Mama yako akija huwa inakuaje? mnaongea kiasi gani?

Mambo ya kuropoka kuwa kama wanaona mnafaidi eti walale na watoto wao utachuma laana bure wewe mwanamke!
Fikiri kabla hujatamka!

"Mwanamke mjinga huivunja nyumb yake kwa mikono yake mwenyewe" (Bible sikumbuki mstari)
 
Back
Top Bottom