Ndugu wa mume kiboko aisee

Ndugu wa mume kiboko aisee

Sioni tatizo hapa! Wewe tu ndo ambae hujiamini! Sasa kama umechoka na kazi zako za siku nzima unasubiri nini kwenda kulala upumzike?! Akija ukamfungulie?!

Mara nyingi wazee huwa usingizi hawana sana tatizo liko wapi akiamua kumsubiri?!

Tatizo lenu ninyi wanawake ni kutaka kujilinganisha na wazazi, hilo haliwezekani! Kujilinganisha ni kujionea bure, unajua kabisa kila mmoja ana umuhimu wake kwa wakati wake.

Kaamua kumsubir mwanae sio tatizo. Maisha ya mijini kazi kutwa nzima na weekends vile vile mihangaiko muda hata wa kuongea nae hana,akaona amsubiri walau apate muda wa kuongea nae kipindi hiki alichowatembelea!

Kama wanaongea kwa kunong'onezana tatizo lako nini kama sio uwezo mdogo wa kujiamini?! Unadhani wanakusema?! Humuamini mmeo kiasi cha kufikiri anaweza kukusema vibaya na mzazi wake?!
Give them space. Huo ndio utu, haikusaidii kutaka kujua kila kitu, kwani hata mmeo huwa anakuambia kila kitu chake?! Fikiria tu.

Sio lazima kila anachoongea na mama yake wewe ujue kisa wewe ni mkewe! Sio lazima!

Jiamini, amekuoa wewe akaacha wazazi wake kuja kujenga familia na wewe! So unayo nafasi yako kwake! Kubwa tu!

Mama yako akija huwa inakuaje? mnaongea kiasi gani?

Mambo ya kuropoka kuwa kama wanaona mnafaidi eti walale na watoto wao utachuma laana bure wewe mwanamke!
Fikiri kabla hujatamka!

"Mwanamke mjinga huivunja nyumb yake kwa mikono yake mwenyewe" (Bible sikumbuki mstari)
kwiwkiwkiwwkwiwkwiwkwiwkwiwki umetokwa povu kweli kweli hivi kuuliza ni ujinga?
 
Sishangai.Kwenye ndoa changa, mwanamke akiona mama mkwe kawasili anapoteza confidence kabisa.anahisi mama mkwe atasema kitu ambacho kitaigharimu ndoa yake.
ndoa ina miaka zaidi ya 10 ni changaeee??
 
usimcheke mamamkwe wako anakufundisha namna ya kumtreat mwanaume ajisikie kupendwa,hata siku nyingine ataona aibu kuchelewa kurudi homu kwani atakua anakuhurumia akijua wife anamsubir
sio hawa wanaume jiji la dasalama kabisaa
 
Haya mambo bwana nlikuwa naskiaga tu kwa watu sasa nayashuhudia live nacheka sana alafu namkumbuka Nicas Mtei mimi nashangaa mbona mama mzaa chema halalii mimi nauchapa nkisikia mume wangu kaja naenda fungua mlango akichelewa mama hatoki sitting room sasa jana jamaa anamuuliza mama yake unafanya nini hapa mama saa4 hii hujalala anajibu''siwezi kulala mpaka urudi'' niliangua kicheko mpaka nikaanguka kuna jirani yangu mmja nae aliniambia mama yake mkwe toka alipokuja ndani ya nyumba na ndio mwisho wa kula na mumewe kwani mama anangangana kula na mtoto wake na atamsubiri hali mpaka arudi hahaha .kweli kuishi na watu tabu mara nyingine anamwita mwanae chemba kunong'oneza.mna matatizo gani ndugu wa mume?? Mnaona twafaidieee humo vyumbanieee mkome laleni nao basi

Mungu akujalie na wewe upate mkwe kwa wanao.....na urudi hapa utujulishe the taste........
 
Chezeya mama mkwe weye!!! hakawii kusingizia kuumwa ili apelekwe hospitali, au kususa kula akisubiri kula na mwanae. Mwanae akirudi yuko safi na kishapata nyama choma mtaani.
ha haaa, kudeka ndo zao, lol!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nivea wewe unasema hiyo ya kumsubiria, mbona hiyo ndogo, mm wa kwangu alikuwa anamfulia mwanae nguo zake kuwa mm sitakatishi, nikamwachia akadhani labda nitalalamika akaona kimyaaaaaaa, akaanza kupika yeye akadhani nitalalamika akakuta kimyaaaaaaa, akaanza akija mume wangu yeye ndiyo wa kwanza kwenda kupokea mizigo anachambua anaangalia kaleta nn , lakini nashukuru Mungu mume wangu anamuelewa mamaye, so haikunipa tabu kukaa naye. so mtu kama huyo wewe mwangalie kama picha, ikifika muda wa kula, wewe jishindilieeeeee, ukimaliza nenda kalale, akirudi mamaye atamfungulia na kula naye. siku akiondoka utarudia nafasi yako. Mwachie mwanae. MUUNGWANA NI VITENDO SI KELELE UTAONEKANA UNAMCHUKIA MAMA WA MWENZIO KUMBE WALAAAAAAAAA!!!!!!
 
nimeipenda hii
 
Haya mambo bwana nlikuwa naskiaga tu kwa watu sasa nayashuhudia live nacheka sana alafu namkumbuka Nicas Mtei mimi nashangaa mbona mama mzaa chema halalii mimi nauchapa nkisikia mume wangu kaja naenda fungua mlango akichelewa mama hatoki sitting room sasa jana jamaa anamuuliza mama yake unafanya nini hapa mama saa4 hii hujalala anajibu''siwezi kulala mpaka urudi'' niliangua kicheko mpaka nikaanguka kuna jirani yangu mmja nae aliniambia mama yake mkwe toka alipokuja ndani ya nyumba na ndio mwisho wa kula na mumewe kwani mama anangangana kula na mtoto wake na atamsubiri hali mpaka arudi hahaha .kweli kuishi na watu tabu mara nyingine anamwita mwanae chemba kunong'oneza.mna matatizo gani ndugu wa mume?? Mnaona twafaidieee humo vyumbanieee mkome laleni nao basi
Naomi na Ruthi Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi, akaondoka mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda pamoja na mke wake na wanae wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu. 2Mtu huyu aliitwa Elimeleki, mkewe aliitwa Naomi, na hao wanawe wawili waliitwa Maloni na Kilioni. Walikuwa Waefrathi kutoka Bethlehemu ya Yuda. Wakaenda katika nchi ya Moabu wakaishi huko.3Elimeleki mumewe Naomi akafa, Naomi akabaki na wanawe wawili. 4Nao wakaoa wanawake wa Kimoabu, jina la mmoja aliitwa Orpa na wa pili aliitwa Ruthi. Baada ya miaka kumi, 5Maloni na Kilioni pia wakafa, basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.6Aliposikia huko Moabu kwamba BWANA amewasaidia watu wake kwa kuwapa chakula, Naomi na wakweze wakajiaandaa kurudi nyumbani. 7Yeye na wakweze wawili, wakaondoka pale walipokuwa wakiishi na kushika njia kurudi nchi ya Yuda.8Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, “Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. BWANA na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki pamoja na mimi. 9BWANA na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani kwa mume mwingine.”Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa 10wakamwambia, “Tutarudi pamoja na wewe nyumbani kwa watu wako.”11Lakini Naomi akasema, “Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine, ambao wataweza kuwaoa ninyi? 12Rudini nyumbani binti zangu, mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana, 13je, mngesubiri mpaka wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa BWANA umekuwa kinyume nami!”14Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake akaenda zake, lakini Ruthi akaambatana naye.15Naomi akamwambia, “Tazama, mwenzako anarejea kwa watu wake na kwa miungu yake. Rudi pamoja naye.”16Lakini Ruthi akajibu, “Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 17Pale utakapofia naminitafia hapo na papo hapo nitazikwa.BWANA na aniadhibu vikali, kama kitu kingine cho chote kitanitenga nawe isipokuwa kifo.” 18Naomi alipotambua kwamba Ruthi amenuia kufuatana naye, hakuendelea kumsihi tena.19Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawakewakashangaa wakasema, “Huyu aweza kuwa niNaomi?”20Akawaambia, “Msiniite tena Naomia, niiteni Marab, kwa sababu Mwenyezi Mungu amenitendea mambo machungu sana. 21Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? BWANA amenitendea mambo machungu, Mwenyezi Mungu ameniletea msiba.”22Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthi Mmoabi, mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom