Ndugu Rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndugu Rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TANURU, Feb 15, 2010.

 1. T

  TANURU Senior Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ambavyo imefanyika kwa ugonjwa wa Malaria siku ya Jumamosi (13/02/2010), tunaomba na kupendekeza pia matatizo haya makubwa katika taifa letu nayo yatanganzwe rasmi kama majanga ya kitaifa:-

  1. Uduni wa ufahamu wa Wakulima wetu katika matumizi ya mbegu bora, mbolea na ukulima wa kisasa.

  2. Uhaba wa KUTISHA wa Madawati katika shule zetu za msingi na sekondari. Ni aibu kubwa kwa watoto wetu kusoma wakiwa wamekaa chini

  3. Uhaba mkubwa wa vitabu toka ngazi ya shule za msingi mpaka chuo kikuu

  4. Ufaulu duni na usiokubalika wa Wanafunzi wetu katika masomo ya Hisabati na Sayansi

  5. Uhaba wa walimu bora hasa kwa masomo ya Hisabati na Sayansi kwa shule za msingi na sekondari.

  6. Mamilioni ya Watanzania wenzetu wasio na ujuzi na utalaam wowote ambao ni muhimu sana katika kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuboresha maisha yao
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,235
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Umefanya nini kusaidia jamii yako kupiga hatua za kimaendeleo unafikiri raisi ni kila kitu kama wewe umeshindwa kuonyesha njia unategemea nini
   
 3. T

  TANURU Senior Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shy,

  Asante kwa changamoto yako. Masuala niliyoyataja hapo juu yanamuhusu Rais moja kwa moja pamoja na viongozi wenzake katika ngazi mbalimbali za uongozi katika taifa letu. Naomba tusidharau nafasi ya Rais katika kuibalisha nchi kwa kasi.

  Kuhusu nini nimefanya, naomba nikutaarifu kuwa nguvu zangu nimezielekeza zaidi kwenye elimu na kilimo. Kwa upande wa elimu nashirikiana kwa karibu na uongozi wa shule moja ya msingi ya serikali katika kuhakikisha kuwa tunatoa wanafunzi bora zaidi na hiyo shule yetu inapanda kitaaluma na ndani ya miaka minne inakuwa moja ya shule 100 bora za msingi hapa nchini toka kati ya shule bora 750 kwa sasa. Idadi ya shule zetu za msingi mpaka Julai 2009 hapa nchini ni 15727 za serikali zikiwa ni 15301 wakati za binafsi ni 426.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...