leez salu
Member
- Oct 2, 2013
- 35
- 8
Nna mpenzi anaitwa juma(sio jina halisi)tuko mikoa tofauti.Wikiend moja akaja kunisalimia. tukiwa wote akachukua simu yangu tukampigia kaka yake tukaongea vizuri nkatambulishwa ikapita.Namba mi sikusave.akaondoka kurudi mkoani kwake.siku 3 zikapita siku hiyo nimetoka chuo narudi hostel message inaingia namba ngeni message zenyewe zile za kutumiana ambazo mimi sizipendagi.Nkauliza nani mwenzangu message ikarudishwa muulize mumeo mimi nani,hapo nina uchovu na hasira za message nkamtumia message mbaya.Kumbe ni yule kaka wa mpenzi wangu.Akaiforwad message kwa mdogo wake ambaye ni mpenzi wangu.Mpenzi wangu akanijia juu huna adabu huna heshima hujui mi namtegemea huyo ndugu yangu. Nkamwambia samahani mi sikujua akanambia kuanzia leo mimi na wewe basi kama umeweza kutukana familia yangu hufai tena.Nkajaribu kubembeleza wap.Nkaomba msamaha kwa kaka mtu hanielewi.Anasema tu hufai kuwa mmoja wa familia yetu na huwezi kuongea na juma mpaka mimi niamue.Leo siku ya 7 sijawasiliana na mpenzi wangu kaniblock nkipiga simu namba busy.nkitumia simu nyingine akijua mimi anakata. Naombeni mawazo yenu nifanyeje.(copy from my frriend)